Hili ni bango utakalokutana nalo ukiwa unaelekea uwanja wa ndege wa Singida uliopo maeneo ya Sabasaba. Hii ni ofisi ya wahudumu wa uwanja wa ndege wa Singida.Maandhari ya uwanja wa ndege wa Singida unapoingia.Hapo ndipo ndege zinapotuwa na kupaa.Helicopter ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Singida.PICHA KWA HISANI YA CHUMA B...
Azimia Na Kulazwa Hospital Baada Ya TFD Kukamata Bidhaa Bandia Dukani Kwake...!
Kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati(TFDA), Aberl Deule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya zoezi la kukagua bidhaa katika maduka ya wilaya ya Manyoni.
Moto ukiwa umewaka kuteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano ambazo ni sumu na zile ambazo muda wake wa kutumika umekwisha.Bidhaa hizo zilikamatwa na TFDA katika baadhi ya maduka ya wilaya ya Manyoni.
Bidhaa ambazo zina sumu na zilizokwisha muda wake zilizokamatwa na TFDA kabla hazijateketezwa kwa moto.
Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati, Aberl Deule (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa muuza duka wa Manyoni mjini.
...
Martha Mlata Aendesha Harambee Ya Kuchangia Ujenzi Wa Msikiti Singida
Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida,Martha Mlata (wa pili kushoto) akipokelewa na waumini wa msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa kitongoji cha Mbuyu Senene kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama,akipokelewa na waumini wa msikiti huo.,
Imamu wa msikiti wa Nuru Salama Unyankindi mjini Singida,Yahaya Mahiki akitoa nasaha zake kwenye hafla ya harambee ya kuchangia kumalizia ujenzi wa msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa kitongoji cha Mbuyu Senene kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama.
Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Martha Mlata akihutubia waumini wa kiislamu wa kijiji cha...
Inasikitisha : Watu watatu wa familia moja wafariki Dunia kwa kuangukiwa na nyumba
Mwandishi wetu, Singida Yetu
WATU watatu wa familia
moja wamefariki duniani mkoani Singida baada ya kuangukiwa na nyumba.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Singida kamishina msaidizi Linus Sinzumwa amesema tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 10 alfajiri wakati wanafamialia hao wakiwa
wamelala.
Amewataja waliokufa kuwa
ni baba wa familia hiyo Ramadhani Amrani (25) mkewe
Mariam Kondo (23) na mtoto wao Amrani Ramadhani mwenye
umri wa miezi saba wote wakazi wa eneo la Tambuka-Reli katika halshauri
ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Kamanda Sinzumwa amesema
siku ya tukio wanafamilia hao walikuwa wamelala kwenye nyumba yao
waliyojenga kwa tofali mbili na kuezeeka kwa miti na udogo mwezi mmoja
uliopita.
Hata ...
UHABA WA NYUMBA NA UPUNGUFU WA WALIMU WA SAYANSI KIKWAZO KIKUBWA KWA ELIMU KATA IPEMBE MKOANI SINGIDA.
Moja ya Majengo ya Shule yaliyojengwa na Mh. Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini.Na. Nathaniel LimuKata ya Ipembe jimbo la Singida mjini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba za kuishi walimu zipatazo 72 katika shule zake tatu ikiwemo moja ya sekondari.Akitoa taarifa yake ya utekelezaji mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida, diwani wa kata hiyo Twalib Kihara amesema shule ya msingi Ipembe inakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi walimu 23, wakati shule ya msingi Sumaye, pia ina upungufu wa nyumba 20.Kihara amesema shule pekee ya sekondari ya kata hiyo, inahitaji nyumba za kuishi walimu 30, kwa sasa...
ABIRIA ZAIDI YA 40 MKOANI SINGIDA WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI KUZIDIWA NA MZIGO.
Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kufa baada ya basi dogo aina ya Costa lenye namba za usajili T.333 BNK lililokuwa linatoka Singida mjini kwenda kijiji cha Ilunda wilayani Iramba, kupinduka katika eneo la kituo cha mabasi cha zamani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuzidiwa na uzito wa mizigo iliyokuwa imepakiwa.Picha mbalimbali zinazoonyesha basi hilo kupinduka.(Picha na Nathaniel Limu).Picha na Mo B...
HIKI NDICHO KIJIJI AMBACHO KIPO KATIKATI YA NCHI YA TANZANIA. TAZAMA HAPA

Hapa ndio Sukamahela maeneo ya Manyoni, mkoani Singida, ambapo ndipo katikati kabisa ya nchi ya Tanzania. Alama yake iko kuleeee juu ya miamba hapo chini ambako ukaindalia kwa makini juu ya mwamba uliochomoza kulia pana alama kama ya nyani aliyesimama inayoashiria hivyo. PICHA NA MICHUZI B...
APENDEKEZA MAGARI 10 TU MSAFARA WA RAIS
Fidelis Butahe, Manyoni
MKAZI wa Kata ya Kintinku, Wilaya ya Manyoni, Hadija Ismail (58) amependekeza
Katiba Mpya iwe na kifungu kinachosema misafara yote ya viongozi hususan
Rais iwe na magari yasiyozidi 10 ili kupunguza gharama za
uendeshaji.
Hadija alisema kuwa fedha zinazotumika kugharimia magari zaidi ya 30
yanayokuwa katika msafara mmoja wa Rais, zinaweza kujenga madarasa na kuwalipa
fedha ya ziada walimu wanaoishi vijijini.
Akizungumza wakati akitoa maoni juu ya Katiba Mpya juzi, Hadija alisema
Katiba Mpya inatakiwa kueleza wazi suala hilo, kwa kuwa fedha za walipa kodi
ndiyo zinazotumika kuendeshea magari hayo.
“Rais msafara wake unatakiwa kuwa na magari 10 tu, msafara wa Waziri Mkuu na
Makamu wa Rais unatakiwa kuwa na magari matano matano,”...