Mbunge  wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida,Martha Mlata (wa pili kushoto)  akipokelewa na waumini wa msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa  kitongoji cha Mbuyu Senene kijiji cha Iguguno wilaya ya  Mkalama,akipokelewa na waumini wa msikiti huo.,
Imamu  wa msikiti wa Nuru Salama Unyankindi mjini Singida,Yahaya Mahiki akitoa  nasaha zake kwenye hafla ya harambee ya kuchangia kumalizia ujenzi wa  msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa kitongoji cha Mbuyu Senene  kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama.
Mbunge  wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Martha Mlata akihutubia waumini wa  kiislamu wa kijiji cha Igiguno wilaya ya Mkalama juzi waliohudhuria  hafla ya harambee ya kuchangia umalizaji wa msikiti wa Almasijidi  Muhidin Baytuhal.Kulia ni katibu wa wananwake wa msikiti huo Mama  Mariamu na kushoto ni diwani wa kata ya Iguguno Bi Lyochi.
Baadhi  ya waumini wa kiislamu waliohudhuria hafla ya kuchangia umalizaji wa  msikiti wa Almasijidi Muhidin Baytuhal wa kitongoji cha Mbuyu Seenene  wilaya ya Mkalama.Harambee hiyo ilikusanya zaidi ya shilingi milioni nne  ambazo ni fedha taslimu na ahadi.
                       (Picha zote na Nathaniel Limu).
0 comments:
Post a Comment