Wajumbe baraza la katiba wataka nafasi ya mgombea binafsi iondolewe kwenye katiba mpya

WAJUMBE wa baraza la maoni ya Katiba mpya katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wamependekeza kuondolewa kwa kipengele cha mgombea huru katika nafasi za udiwani, ubunge na Raisi. Wajumbe  hao wamesema kuwa ni vyema wagombea wote wa nafasi hizo wakatokana na vyama vya siasa, ili kupunguza uwezekano wa kumuingiza madarakani kiongozi ayesiyekuwa na maadili mazuri. Wakizungumza kwenye kikao cha  baraza  la maoni ya katiba mpya wilaya ya Ikungi mkoani Singida leo,  baadhi ya wajumbe wamesema  wagombea wanaotokana na vyama vya siasa hupigiwa kura za  maoni na kuchunjwa kwenye vikao kabla ya  kuwepewa tiketi ya kuwania nafasi husika. Wamesema kitendo cha kuruhusu mgombea huru,  kinaweza kusababisha watu wenye ushawishi mkubwa wa kifedha kutumia vibaya...

Nyara za Serikali zawafikisha polisi

JESHI la Polisi Mkoa wa Singida, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma ya kumiliki nyara za Serikali kinyume na sheria. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela aliwataja watu wanaoshikiliwa kuwa ni Esinasi Stephano (36) mkazi wa Kijiji cha Chikuyui. Alisema mtuhumiwa alikamatwa kwa kosa la kumiliki meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo tano na thamani ya zaidi ya Sh milioni 4.4. Alisema mtuhumiwa huyo, alikamatwa juzi jioni baada ya raia wema kutoa taarifa polisi. Alimtaja mtuhumiwa wa pili kuwa ni, Mwanandi Amani (34) mkazi wa Kijiji cha Mitundu ambaye alikamatwa na mkia wa tembo, meno mawili ya ngiri, mafuta ya samba na sare moja ya Jeshi la Polisi. Alisema mtuhumiwa huyo, alikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa juu ya umilikaji wake wa nyara za serikali kinyume...

HABARI YA KUSIKITISHA: MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AUAWA KIKATILI

Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kizega wilayani Iramba Bi. Mariamu Alphonce mwenye umri wa miaka kumi ameuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na kucharangwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kaka yake bwana Elibariki  Alphonce.  Akieleza kwa uchungu baba wa mtoto huyo bwana Alphonce Msengi amesema alipofika nyumbani kwake majira ya saa kumi na moja jioni alikuta damu nyingi na alipo angali vizuri alimuona mtoto wake Mariamu Alphonce akiwa amekatwakatwa kwa mapanga na tayari alikuwa ameshafariki. Bwana Msengi baada ya kuona hivyo alipiga yowe na walikuja majirani na watoto na wakamwambia...

Magunia ya mkaa 311 yaliyovunwa kinyemela yakamatwa Singida

WAKALA wa huduma za Misitu  nchini  katika  halmashauri ya wilaya ya Singida,amefanikiwa kukamata magunia ya mkaa 311 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 5.2 milioni, ambayo yamevunwa kinyume na sheria. Meneja wa wakala huyo wilayani Singida bwana Hashimu Kativo, amesema magunia hayo wameyakamata  mapemawiki hii katika msako mkali unaoendelea wa kuwakamata wafanyabiashara na watu wengine wanaouza  mazao ya misitu na nyuki kinyume na sheria za  nchi. Amesema  magunia hayo yamekamatwa katika kijiji cha Tupendane kata ya Mang’onyi baaada ya kukuta magunia hayo yakiwa yamekusanywa  bila kuwa na kibal cha kuvuna wala leseni ya kununua na kuuza mkaa. Hata  hivyo amefafanua kuwa wamiliki wa mkaa huo waliweza kutoroka kwenda kusikojulikana. Bw...

Yunde ashinda kwa kishindo kugombea Uenyekiti wa halmashauri ya Ikungi mkoani Singida.

Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Joseph Rudisha akitoa mwongozo kwenye mkutano wa uchaguzi wa kuchagua mwenyekiti na makamu wake wa halmashauri ya wilaya hiyo mpya.Wa kwanza kulia ni mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti Celestine Yunde. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi, Hassan Tati akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa nafasi za mwenyekiti na makamu wake wa halmashauri ya wilaya mpya ya Ikungi. Mkutano huo ulifanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.Wa kwanza kulia ni mgombe wa nafasi ya mwenyekiti Celestine Yunde na kushoto ni mgombe wa nafasi ya makamu mwenyekiti, Alli Nkhangaa. Mgombea...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa