Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kumaliza mgogoro wa wagombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku akiwa ofisini kwake.
Mgombea
Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, Jastine Monko akizungumza na
waandishi wa habari nje ya jengo la CCM Mkoa wa Singida baada ya
kumaliza tofauti zao.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa
habari nje ya viwanja vya CCM Mkoa wa Singida, mara baada ya kikao cha
maridhiano baina yake na wagombea wenzake saba kumalizika na kuondoa
tofauti zao.
Wagombea
wa Ubunge Singida Kaskazini wakipanda gari kuendelea na mchakato kwa
kuomba kura kwa wananchi baada ya kumaliza kikao na Katibu wa CCM Mkoa
Mary Maziku.(PICHA ZOTE NA HILLARAYSHOO, SINGIDA).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
Hatimae
mgogoro uliokuwa ukifukuta kwa wagombea saba wa nafasi ya Ubunge Jimbo
la Singida Kaskazini kutaka kugomea kuendelea na mchakato wa kura za
maoni umemalizika na sasa wagombea hao wanaendelea na zoezi.
Hatua
hiyo ya wagombea saba kutaka kugomea ilidaiwa ni kutokana na mgombea
mwenzao Lazaro Nyalandu kukiuka taratibu za mchakato huo, na hivyo
kuonekana kana kwamba anabebwa na viongozi wa Wilaya ya Singida
vijijini.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana , Katibu wa CCM Mkoa wa
Singida Mary Maziku alisema baada ya kikao cha kuwakutanisha pande zote
mbili , kila moja alikuwa na malalamiko yake, lakini baada ya kikao cha
pamoja cha zaidi ya saa moja, walimaliza suala hilo.
Maziku
alisema kuwa kilichotokea ni siasa za kupakana matope, kuchafuana ,
kudharauliana na kejeli za hapa na pale miongoni mwa wagombea hao.
Aidha
alisema baada ya kusikiliza malalamiko ya wagombea saba Justine Monko,
Yohana Sintoo, Amos Makiya, Alon Mbogo, Sabasaba Manase, Michael Mpombo
na Mungwe Athuman,dhidi ya Nyalandu ambaye nae alikuwa na malalamiko
yake, walikubaliana kimsingi kuondoa tofauti zao kwa kuwa wote ni wana
CCM.
“Hawa
saba walikuwa wakimlalamikia Nyalandu lakini na yeye alikuwa
akiwalalamikia hawa, sasa baada ya ya kukaa pamoja tumeona hakuna haja
ya kuendelea na malumbano kwa kuwa wote wameonekana kuwa na makosa
madodo madogo ambayo hayana mashiko bali ni siasa za kawaida kwenye
chaguzi mbalimbali.” Alisistiza Maziku.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Waziri
wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema hana tatizo na mgombea
yeyote na kwamba madai ya wagombea wenzake kumlalamikia ni dalili za
kuanza kushindwa.
“Mimi
niwaambie waandishi wa habari nimefanya mambo mengi katika Jimbo hili
la Singida Kaskazini na wananchi watanipima kwa kazi sio maneno, na nina
uhakika wa kupata zaidi ya aslimia 90 ya kura za maoni.”Alijigamba
Nyalandu huku akionesha kujiamini sana.