Home » » Maziku amaliza mgogoro wa Nyalandu na wenzake, waendelea na mchakato kuomba kura kwa wananchi

Maziku amaliza mgogoro wa Nyalandu na wenzake, waendelea na mchakato kuomba kura kwa wananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KATIBU
Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mgogoro wa wagombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini.
maziku
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku akiwa ofisini kwake.
MONKO
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, Jastine Monko akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la CCM Mkoa wa Singida baada ya kumaliza tofauti zao.
nyalandu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya CCM Mkoa wa Singida, mara baada ya kikao cha maridhiano baina yake na wagombea wenzake saba kumalizika na kuondoa tofauti zao.
GARI
Wagombea wa Ubunge Singida Kaskazini wakipanda gari kuendelea na mchakato kwa kuomba kura kwa wananchi baada ya kumaliza kikao na Katibu wa CCM Mkoa Mary Maziku.(PICHA ZOTE NA HILLARAYSHOO,  SINGIDA).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
Hatimae mgogoro uliokuwa ukifukuta kwa wagombea saba wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kutaka kugomea kuendelea na mchakato wa kura za maoni umemalizika na sasa wagombea hao wanaendelea na zoezi.
Hatua hiyo ya wagombea saba kutaka kugomea ilidaiwa ni kutokana na mgombea mwenzao Lazaro Nyalandu kukiuka taratibu za mchakato huo, na hivyo kuonekana kana kwamba anabebwa na viongozi wa Wilaya ya Singida vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana , Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku alisema baada ya kikao cha kuwakutanisha pande zote mbili , kila moja alikuwa na malalamiko yake, lakini baada ya kikao cha pamoja cha zaidi ya saa moja, walimaliza suala hilo.
Maziku alisema kuwa kilichotokea ni siasa za kupakana matope, kuchafuana , kudharauliana na kejeli za hapa na pale miongoni mwa wagombea hao.
Aidha alisema baada ya kusikiliza malalamiko ya wagombea saba Justine Monko, Yohana Sintoo, Amos Makiya, Alon Mbogo, Sabasaba Manase, Michael Mpombo na Mungwe Athuman,dhidi ya Nyalandu  ambaye nae alikuwa na malalamiko yake, walikubaliana kimsingi kuondoa tofauti zao kwa kuwa wote ni wana CCM.
“Hawa saba walikuwa wakimlalamikia Nyalandu lakini na yeye alikuwa akiwalalamikia hawa, sasa baada ya ya kukaa pamoja tumeona hakuna haja ya kuendelea na malumbano kwa kuwa wote wameonekana kuwa na makosa madodo madogo ambayo hayana mashiko bali ni siasa za kawaida kwenye chaguzi mbalimbali.” Alisistiza Maziku.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema hana tatizo na mgombea yeyote na kwamba madai ya wagombea wenzake kumlalamikia ni dalili za kuanza kushindwa.
“Mimi niwaambie waandishi wa habari nimefanya mambo mengi katika Jimbo hili la Singida Kaskazini na wananchi watanipima kwa kazi sio maneno, na nina uhakika wa kupata zaidi ya aslimia 90 ya kura za maoni.”Alijigamba Nyalandu huku akionesha kujiamini sana.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa