Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dk. John Magufuli.
Kanisa
la Christian Mission Fellowship Tanzania, limesema ili Watanzania
warejeshe imani kwa serikali yao, kuna umuhimu wa anayegombea nafasi ya
urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, avunje
mfumo uliopo sasa ndani ya chama hicho.
Makamu Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Donald Mhango, akizungumzia
uteuzi wa CCM uliompa ushindi Dk. Magufuli, alisema mfumo unaotakiwa
kuvunjwa ni ule unaosababisha baadhi ya viongozi kujihusisha na ufisadi,
rushwa, kutowajibika ipasavyo kwenye nafasi za kazi, wanaosababisha
taifa hasara na kutowajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Askofu Mhango alisema Watanzania wengi wanatarajia Dk. Magufuli
,atatumia ujasiri alionao kuwaondoa madarakani wale wote wanaotuhumiwa
kuliingizia taifa hasara, hali ambayo imeendelea kudidimiza hali za
wananchi na kuendelea kuwa maskini.
“Naamini Dk. Magufuli ameinuliwa kwa kusudi maalum. Kikubwa
tunachotarajia afanye ni kuvunja mfumo wa serikali ili kurudisha imani
ya Watanzania ambayo siyo siri kwamba imetoweka. Kwa sasa taifa
limegawanyika vipande vipande, vikiwamo vya udini, ukabila na tofauti za
kiuchumi,” alieleza Askofu Mhando.
Alitaja sababu kubwa iliyowafanya wananchi kukosa imani kwa
serikali yao kuwa ni viongozi wengi kuhusishwa na kashfa mbalimbali za
kukosa uadilifu ikiwamo za rushwa na kutowajibika, kiasi cha baadhi yao
kushuhudiwa wakiitwa mizigo lakini wakiendelea kuachwa wabaki
madarakani.
Hata hivyo Askofu Mhando alisema ili serikali ya awamu ya tano
ifanikiwe kubomoa mifumo hiyo ya kiutawala, ni lazima kila Mtanzania kwa
imani yake amuombe Mungu ili aingilie kati
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment