Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Haikuwa bahati yake. Safari ya Wema Sepetu kuelekea bungeni imefikia tamati.
Hiyo
ni baada ya kushindwa kuwashawishi wanachama wa CCM mkoani mkoani
Singida kumpa dhamana ya kuwawakilisha kwenye viti maalum vya ubunge.
Wema
ameshindwa kupita kwenye kura za maoni za ubunge huo kwa kupata kura 90
tu. Aliyeongoza kwenye kinyang’anyiro hicho ni Aysharose Mattembe
(311), Martha Mlata (235) na Diana Chilolo (182).
Wema amekubali kushindwa na kudai kuwa ushiriki wake umempa ujasiri zaidi.
“Nilivyoamua
kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii
nimekosa, ila dunia bado inazunguka,” ameandika kwenye kwenye Instagram.
“Nawapongeza
walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki
kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo. Nawashukuru pia wote
mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu
upya,” ameongeza.
“2015
ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things
loading.. Most of all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi na
nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo
kwanza inaanza.”
0 comments:
Post a Comment