Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14
milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation
mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi
choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida,
chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi
wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali,
uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi wa Doris Mollel
Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye
hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni,
kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na
Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation
mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia)
wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
Mwakilishi wa MO Dewji mkoani
Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel
Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo
bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni
na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo la choo bora chenye matundu
nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa
ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation
kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini
Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri
ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa
hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya
kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa
MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa,
yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni
465.
Alisema uzoefu unaonyesha kwamba
mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia
viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora
vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi ,
kujiendeleza kielimu.
Akifafanua, alisema shule ya msingi
ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya
wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel
Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation
kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Doris Mollel (Miss
Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya
elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa
kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi
Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel
Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru
kufungiwa.
“Nitumie nafasi hii pia kulipongeza
shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo
bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa
wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.