Kaimu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini, Gerald Muhabuki Zephyrin,akizungumza na Modewjiblog juu ya uchaguzi ubunge jimbo la Singida mjini.(Picha na Gasper Andrew).
Na Nathaniel Limu, Singida
PINGAMIZI
lililowekwa na Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA),jimbo la
Singida mjini, dhidi ya mgombea wa CCM Mussa Ramadhan Sima kuwa fomu
zake haziko sawa kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za
uchaguzi,limetupiliwa mbali kwa madai kwamba halina mashiko.
Akizungumza na mwakilishi wa Modewjiblog
ofisini kwake, kaimu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida
mjini,Gerald Muhabuki Zephyrin, alisema kuwa CHADEMA iliwasilisha
pingamizi kwamba barua ya kumthibitisha Sima kugombea ubunge kupitia
tiketi ya CCM, imesainiwa na mtu ambaye hakubaliki kisheria.
Akifafanua,
alisema mgombea wa jimbo la Singida mjini kupitia CHADEMA, Msindai
Mgana Izumbe, amelalamikia barua hiyo kuwa imesainiwa na Mary Maziku,
kwa madai sio katibu halisi wa mkoa wa Singida.
Gerald
alisema katika kujiridhisha kama kweli Maziku sio mtu stahiki wa
kumuthibitisha mgombea wa CCM kwenye nafasi ya ubunge jimbo la Singida
mjini,aliwasiliana na makao makuu CCM Lumumba jijini Dar-es-salaam,na
kujibiwa kwa barua kwamba Maziku ndiye katibu wa CCM mkoa wa Singida.
“Mgombea
Msindai ambaye alikuwa mwenyekiti CCM mkoa hadi kumalizika kwa mchakato
wa kura za maoni,katibu wake wa mkoa kwa wakati huo, alikuwa Mary
Chatanda ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mary Maziku kipindi cha
mchakato wa kura za maoni unaendelea.Maziku ndiye aliyesaini barua ya
kumthibitisha Sima”,alifafanua zaidi.
Katika
hatua nyingine,Gerald ambaye ni mkuu wa idara ya utumishi na utawala
manispaa ya Singida,amesema kuwa aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la
Singida mjini,Victoria John Msusu kupitia UPDP,ameeguliwa kwenye
kinyang’anyiro hicho baada ya kushindwa kutimiza masharti ikiwemo
kushindwa kuwasilisha fomu kwa wamadai na kushindwa kulipa ada ya fomu
shilingi 50,000.
Msimamizi
amewataja wagombea wa ubunge wa jimbo la Singida mjini waliopitishwa na
chama kwenye mabano kuwa ni ni pamoja na Sima (CCM),Jeremia Paulo
Wandili (ACT Wazalendo),Msindai Mgana Izumbe (CHADEMA) na Mwanamvua John
Haji (CUF).
Alisema
kampeni zimeishaanza vizuri kwa amani na utulivu mkubwa na amewaoomba
wagombea kufanya kampeni kwa ustarabu na kuzingatia kanuni,taratibu na
sheria za uchaguzi.
“Matarajio
ya wananchi wa jimbo la Singida mjini,ni kwamba oktoba 25 mwaka
huu,wapige kura kuwachagua viongozi wanaoamini watawaletea maendeleo ya
kweli na si vinginevyo”, alisema Gerald.
0 comments:
Post a Comment