Mbunge wa jimbo la Singida mashariki Mh. Tundu Lissu akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya nafasi ya udiwani kata ya Iseke tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi uliofanyika katika kijiji cha Iseke.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Iseke tarafa ya Ihanja waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya udiwani kata ya Iseke uliofanywa na chama cha CHADEMA.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya udiwani wa kata ya Iseke tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mgeni rasmi katika kampeni ya uzinduzi wa nafasi ya udiwani kata ya Iseke tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi Mh. Tundu Lissu, ameashindwa kuuza sera za CHADEMA na badala yake ametumia muda na nguvu nyingi kuhimiza sera yake ya ‘katazo’ la wananchi kuchangia maendeleo yao .
Mh. Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA, alipanda jukwaani huku akiwa mabeba makabrasha ya michanganuo ya bajeti ya serikali ya kuanzia mwaka wa fedha wa 2010/2011 hadi 2013/2014.
Akisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha iseke, Mh Tundu Lissu aliweka wazi kuwa “Mimi sitaki kabisa kuzungumzia habari za Amosi Mghenyi ambaye ametusaliti kwa kuhama CHADEMA na kurejea CCM. Amosi kisiasa ni mfu, kwa hiyo siwezi kupoteza muda wangu kuzungumiza mambo ya mfu”.
Amesema ufunguzi wake utajikita zaidi katika kuwaelimisha wananchi wa kata ya Iseke kwamba serikali inayo fedha nyingi na za kutosha kugharamia maendeleo ya wananchi.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, amesema kwa mfano katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, mkoa wa Singida, ulipewa zaidi ya shilingi milioni 903 za undeshaji wa shule, lakini zilizotumika ni zaidi ya shilingi milioni 464 na kubaki zaidi ya shilingi 438.2.
Amesema fedha hizo zaidi ya shilingi 438.2 zilizobaki, hazijaainishwa zilipelekwa wapi. “Kwa vyo vyote zitakuwa zimeishia kwenye matumbo ya mgambo na watendaji wa serikali ya CCM”.
Mh. Tundu ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma, amewataka wakazi wa kata ya Iseke, kumchagua Emmnuel Jackson Jingu awe diwani wao, ili waondokane na manyanyaso ya michango kama walivyojikomboa wakazi wa jimbo la Singida Mashariki.
Wagombea wengine wa nafasi ya udiwani kata ya Iseke ni Amosi Munghenyi wa CCM na Abdallah Kinyenje maarufu kwa jina la Petro wa CUF.
0 comments:
Post a Comment