Kaimu
kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobius Sedoyeka,
akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mauaji ya watu wawili
wakazi wa wilaya ya Ikungi akiwemo mmoja kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mama mzazi wa muuaji. Salumu Juma mkazi wa
kijiji cha Makotea, amemuawa Faraja Emmanuel, kwa madai kuwa ana
mahusiano ya kimapenzi na mama yake.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA
mmoja na mkazi wa kijiji cha Makotea wilaya ya Ikungi mkoa wa
Singida,Salumu Juma (37) amefariki dunia baada ya kushambuliwa vibaya na
Faraja Emmanuel kwa tuhuma ya kuwa na mahusiano ya mapenzi na mama
yake.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida,ACP Thobius Sedoyeka amesema
tukio hilo limetokea aprili 19 mwaka huu saa saba mchana huko katika
hospitali ya misioni ya Makiungu wilaya ya Ikungi.
Amesema
siku ya tukio,mtuhumiwa Salumu alimvia njiani Faraja na baada ya
kumvamia alimshambulia kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili na
kisha kumvunja miguu yote miwili.
“Salumu
baada ya kutimiza azma yake hiyo alimwacha Faraja akiwa amezirai na
yeye kulimbilia kusikojulikana wasamaria wema waliweza kumwokota Salumu
na kisha kumkimbiza katika hospitali ya Makiungu ambapo alifariki akiwa
anaendelea kupatiwa matibabu”,alifafanua zaidi,Sedoyeka.
Amesema
uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Salumu ametenda kosa hilo baada ya
kuchukizwa na tabia ya Faraja kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama
yake mzazi.
“Kwa sasa tumeanzisha msako mkali wa kumtafuta Salumu ili amweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katika
tukio jingine,Sedoyeka amesema kuwa Joram Joseph (36) mkulima na mkazi
wa kijiji cha Msimii kata ya Sepuka wilaya ya Ikungi,amefariki dunia
baada ya kuchomwa kisu shingoni na bega la kushoto na baba yake mzazi
Joseph Benjamin (61).
Amesema tukio hilo limetokea Aprili 21 mwaka huu saa moja usiku huko katika kijiji cha Msimii Sepuka.
Kaimu
kamanda huyo amesema chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na Joram
kumtukana matusi ya nguoni baba yake mzazi.Joramu inadaiwa kutoa matusi
hayo kutokana na kulewa pombe ya kienyeji kupindukia.
“Baada ya mauaji hayo,mtuhumiwa mzee Joseph aliweza kujisalimisha mwenye katika kituo cha polisi cha Sepuka”,amesema Sedoyeka.
Mo Blog
0 comments:
Post a Comment