Na Nathaniel Limu, Ikungi
VIJANA
 wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamehimzwa kuondokana na uvivu na 
badala yake waelekeze nguvu zao katika kilimo cha kibiashara cha viazi 
vitamu ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Changamoto
 hiyo imetolewa na mkulima na mfanyabiashara wa zao la viazi vitamu na 
mkazi wa kijiji cha Nkuninkana,Ibrahimu Kilu (34) wakati akizungumza na 
MOblog juu ya kilimo hicho cha viazi vitamu ambacho pia ni  zao la 
chakula.
Amesema
 kuwa zao la viazi vitamu ambalo miaka ya nyuma lilikuwa ni zao la ziada
 (halikupewa umuhimu unaostahili) hivi sasa zao hilo lina soko zuri 
ndani na nje ya nchi.
“Viazi
 vitamu kutoka wilaya yetu ya Ikungi vinakimbiliwa sana na 
wafanyabiashara kutoka mkoa wa Dodoma,Morogoro,Dar-es-salaam,Tanga na 
mikoa mingine nchini, pia kuna wafanyabiashara wanatoka Zambia na Comoro
 Kwa hali hiyo soko la zao hilo ni kubwa na linalipa vizuri”,alifafanua 
Ibrahimu.
Ibrahimu
 amesema toka aanze kulima zao hilo kibishara miaka mitano iliyopita 
limemwezesha kujenga nyumba bora na ya kisasa yenye choo ndani,amenunua 
pikipiki,anao mtaji wa kutosha na anasomesha watoto wake bila shida.
“Kilimo
 cha kibiashara cha viazi vitamu kina faida nyingi kinainua mhusika 
kiuchumi na pia uhakika wa kukabiliana na makali ya njaa unakuwepo.Mfano
 mzuri ni kwamba mimi msimu uliopita nililima uwele katika mashamba 
yangu yote na nilipata chakula cha kutosha kwa miaka miwili 
mfululizo”,amesema na kuongeza;
“Msimu
 huu,kwa sababu nina chakula cha kutosha mashamba yote nimelima viazi 
vitamu kwa lengo la kuboresha uchumi wa familia yangu matarajio ni 
kwamba natarajia kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi milioni tatu”.
Akifafanua
 zaidi, Ibrahimu amesema faida ya kilimo cha viazi vitamu ni kwamba 
msimu huu nikilima mashamba yote  viazi zao hilo la viazi hurutubisha 
ardhi kwa kiwango kikubwa na hivyo msimu ujao atakapolima uwele atakuwa 
na uhakika wa kuvuna zaidi ya lengo.
Wakati
 huo huo, wakulima hao wamelalamikia tabia ya wafanyabiashara 
kuwalazimisha kujaza viazi vitamu kwenye magunia aina ya rumbesa ambayo 
yana uzito wa zaidi ya kilo 130 ambao kisheria haikubaliki.
Kwa
 upande wake Afisa Kilimo na Mifugo wilaya ya Ikungi,Ayubu Sengo  
amesema wakulima wenyewe ndio wanaochangia biashara ya viazi vitamu 
ifanyike kwenye magunia ya rumbesa.
“Wakulima
 wetu kwanza ni watu wa ajabu kidogo na uvivu fulani upo ndani yao 
badala ya wao kuvuna viazi na kuvijaza kwenye gunia wao wanamwachia 
mnunuzi avivune kwa maana ya kuvichimba na kuvijaza kwenye magunia ya 
rumbesa na ndipo mkulima atalipwa kulingana na idadi ya magunia ya 
rumbesa”,alifafanua Sengo.
0 comments:
Post a Comment