Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa.
Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA
ya wanafunzi 2,006 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
huu mkoani hapa bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Afisa Kazi Sekretariati mkoani Singida,Jacob
Elias wakati akitoa taarifa ya usajili wa wanafunzi kidato cha kwanza
mwaka huu mbele ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)
kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi
Stadi (VETA) mjini Singida.
Amesema
wanafunzi hao ambao bado hawajaripoti hadi sasa ni sawa na asilimia 19
ya wanafunzi wote 10,802 waliofaulu mtihani wa taifa wa kumaliza shule
za msingi.
Akifafanua,Jacob amesema wilaya ya Manyoni inaongoza kwa wanafunzi 585 ambao hawajaripoti kuanza kidato cha kwanza hadi sasa.
“Manyoni
inafuatiwa na Wilaya ya Ikungi ambayo wanafunzi 503 hawajaripoti kuanza
kidato cha kwanza hadi sasa.Iramba 318, Manispaa ya Singida 270,
Singida vijijini 238 na Mkalama 92″, amesema Jacob.
Amesema
kila Halmashauri na Manispaa zinapaswa kuweka mikakati bora na sahihi
ili kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu, ajulikane yupo wapi aweze
kufuatiliwa na kuanza masomo.
Kuhusu ajira ya walimu wapya,Jacob amesema mkoa umepangiwa walimu wapya 469 nwa shule za msingi na 636 wa shule za sekondari.
“Kwa
upande wa walimu hao wapya wa sekondari,sanaa imepangiwa walimu 129
wenye diploma na 418 wenye digrii.Sayansi wenye diploma ni 36 na digrii
53″,amesema.
Jacob
amesema kutokana na mchanganuo huo, walimu wa sayansi na hisabati ni 89
na hili bado ni janga kubwa kwa mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Amesema
walimu hao wachache,watumiwe kikamilifu ili waweze kuzalisha
wanasayansi wengi watakaopelekea kupata walimu wa kutosha wa sayansi
kimkoa na kitaifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment