Home » » Watoto 4000 kupatiwa chanjo katika Wiki ya Chanjo - Parseko Kone, Singida‏

Watoto 4000 kupatiwa chanjo katika Wiki ya Chanjo - Parseko Kone, Singida‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC07952
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizindua utoaji wa chanjo kimkoa katika hospitali ya St.Calorus iliyopo kijiji cha Mtinko. Jumla ya watoto 3,999 wanatarajiwa kupatiwa chanjo mbalimbali.
DSC07953
DSC07970
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza na wakazi wa tarafa ya Mtinko wilaya ya Singida, muda mfupi baada ya kuzindua zoezi la chanjo kimkoa lililoanza jana na linatarajiwa kumalizika Aprili 30 mwaka huu.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu-Mo Blog
JUMLA ya watoto 3,999 mkoani Singida wanaositahili kupata chanjo mbalimbali,wanatarajiwa kupatiwa chanjo katika kipindi cha wiki ya chanjo iliyoanza aprili 24 hadi 30 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa ngazi ya kimkoa uliofanyika katika hospitali ya St.Calorus kijiji cha Mtinko.
Mkuu huyo wa mkoa,amesisitiza kuwa ni muhimu sana kuhakikisha kila mtoto,anapata chanjo zote kwa wakati,ili kukidhibiti milipuko ya magonjwa mbalimbali.
"Magonjwa yanayolengwa na mpango wa chanjo wa taifa,ni kifua kikuu,donda koo,kifaduro,polio,surua,pepo punda,homa ya ini,homa ya uti wa mgongo,kichomi na kuhara",alifafanua.
Dk.Kone alisema ili lengo la utoaji chano hizo liweze kufikiwa, ni lazima wataalam,wasimamizi wa chanjo wabadilike kwa kubuni mbinu mpya za kuhamasisha wananchi kuwapeleka watoto wote wanaostahili kupatiwa chanjo mbalimbali kwenye vituo vya kutolea huduma.
"Kwa ujumla,kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha mtoto wake,mtoto wa jirani,au mtoto ye yote yule,anapata haki ya kupewa chanjo,ili kumzuia aspatwe na maradhi ambayo yanazuilika kwa chanjo na asiwe hatari kwa wengine",alisema.
Awali kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Mussa Kamala alisema zoezi hilo litaendeshwa katika vituo 186 vya huduma ya chanjo mkoani Singida.
Alisema walengwa ni watoto wote walio na umri wa chini ya mwaka mmoja na ambao hawajapata au hawajakamilisha chanjo.
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo mwaka huu,ni "chanjo ni jukumu letu sote".

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa