Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akifungua hafla ya uzinduzi wa bodi
ya maji bonde la kati. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Aqua Resort Vitae mjini hapa. Kulia ni Mwenyekiti mpya wa bodi ya
maji bonde la kati, Eng.Samson Babala na kushoto ni Naibu Katibu
TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo.
Naibu
Katibu Mkuu TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo, akitoa nasaha zake kwenye
hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya maji bonde la kati uliyofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Aqua Resort Vitae mjini hapa. Wa kwanza kulia ni
Mwenyekiti mpya wa bodi ya maji bonde la kati, Eng.Samson Babala, wa
pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na kushoto ni
Mwenyekiti mstaafu bodi ya maji bonde la kati, Eng.Mwanaasha Ally.
Mwenyekiti
mstaafu wa bodi ya maji bonde la kati, Eng.Mwanaasha Ally, akitoa
nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya maji bonde la kati
iliyofanyika mjini hapa jana.Kushoto walioketi ni Naibu Katibu Mkuu
TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo, katikati ni Mkuu wa mkoa wa Singida,
Dk.Parseko Kone na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti mpya bodi ya maji bonde
la kati, Eng.Samson Babala.
Baadhi
ya wajumbe wa bodi ya maji bonde la kati waliohudhuria hafla ya
uzinduzi bodi hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua resort
vitae mjini hapa.(Picha na .Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa mkoa wa Singida, ameuhimiza uongozi mya wa bodi ya maji bonde la
kati kufanya maandalizi ya kina yatakayowezesha kupata mbinu na njia za
kisasa za kusimamia na kugawa maji,ili kuepusha migogoro ya maji.
Dk.Kone
ametoa rai hiyo wakati akizindua bodi ya nne ya maji bonde la
kati.Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae
Hoteli mjini hapa.
Alisema
Tanzania inalenga kwenda kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025,mojawapo ya vichocheo vikubwa katika kufikia malengo hayo,ni
mapinduzi ya kilimo na viwanda ambavyo yatahitaji maji mengi na ya
kutosha.
Dk.Kone
alisema pamoja na kilimo na viwanda kuhitaji maji ya kutosha,pia
ongezeko la watu na shughuli zao mbalimbali zikiwemo za
kiuchumi,zinazitaji kiwango kikubwa cha maji.
“Kutokana
na uhitaji huo mkubwa wa maji,uwezekano wa kutokea kwa migogoro
itakayotokana na uhitaji wa maji,ni mkubwa.Nina taarifa kuwa tayari
migogoro hii imeanza kuongezeka hasa katika maeneo ya mikoa ya Manyara
na Arusha.Bodi hii ni lazima isimamie kikamilifu masuala haya kwa
ukamilifu na ufanisi mkubwa”,alisema.
Katika
hatua nyingine,mkuu huyo wa mkoa alisema maamuzi mengi duniani ambayo
ni pamoja na yanayohusu maji,yanafanywa na wanasiasa au na viongozi
ambao ni wanasiasa.
“Kwa
hiyo katika utendaji kazi wenu,hamna budi kushirikiana na wanasiasa na
viongozi wengine wa serikali katika ngazi za kitaifa,mikoa,wilaya,kata
na vijiji,ili kutatua changamoto za maji kwa pamoja”,alisema.
Aidha,Dk.Kone
ametoa rai kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, katika bajeti
ya maji watoe kipaumbele katika utunzaji na usimamizi wa rasilimali za
maji, ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za maji kwa wingi.
“Bila
takwimu za muda mrefu na sahihi,usimamizi wa rasilimali za maji utakuwa
ni mgumu sana na unakuwa sio wa kisayansi”,alifafanua Dk.Kone.
Awali
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng.Emmanuel Kalobelo,
alisema majukumu ya msingi ya bodi ya maji za mabonde,ni
kusimamia,kupanga na kuendeleza rasilimali za maji zilizoko katika
mabonde.
“Bodi
hizi zikifanya kazi zake vizuri,Watanzania tutakuwa na uhakika wa
uatikanaji endelevu wa maji,kwani bodi hizi ni lazima zitayarishe miango
ya usimamizi wa rasilimali za maji katika mabonde.
Akifafannua
zaidi, Eng.Kalobela,alisema bodi za maji za mabonde zinaaswa
kushirikiana na wadau wengine kutatua migogoro ya utunzaji wa maji
inayojitokeza katika maeneo yao.
Kwa
mujibu wa Naibu Katibu Mkuu huyo, Tanzania ina mabonde tisa, ambayo ni
bonde la Pangani, Ruvuma, waMi ya kusini, Rufiji, Wawi/Ruvu, Ziwa
Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na bonde la kati.
Na Mo Blog