Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amezitaka halmashauri za Mkoa wa
Singida kuacha kulalamika kukosa mapato bali watumie vizuri rasilimali
nyingi zilizopo, ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuongeza mapato yao.
Dkt
Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akifungua mafunzo ya
kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa
jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za
mkoa wa Singida.
Amesema
Mkoa una fursa nyingi katika sekta ya kilimo, utalii, ufugaji, madini
na uvuvi ambazo bado hazijatumiwa vizuri na halmashauri katika kukuza
uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Singida.
“Singida
ina zalisha Vitunguu vingi na bora nchini, ina zalisha viazi zitani
vingi na vyenye ubora, singida pia ni mzalishaji mkubwa wa alizeti na
mafuta ya alizeti huku tukiwa na viwanda zaidi a 120 vya kusindika
mafuta ya alizeti, katika sekta ya utalii tuna vivuti vngi ikiwemo bwawa
la kuongelea ‘swimming pool’ lililojengwa na mjerumani na lipo katikati
ya pori lakini vyote hivi hatujavitumia vizuri,” amesisitiza Dkt
Nchimbi.
Dkt
Nchimbi ameongeza kuwa halmashauri zinapaswa kutotumia mafunzo hayo
kulalamika bali mafunzo hayo yawajengee uwezo wa kutambua wapi kuna
pengo katika maendeleo ya jamii na kisha kuanisha fursa na mikakati ya
kuzitumia fursa hizo kuziba pengo hilo.
Aidha
amewataka kutumia fursa ya malengo na mitazamo waliyonayo ambayo
inaweza kuleta maendeleo pamoja na kuhakikisha kuwa mafunzo hayo
yanawajengea uwezo wa kubaini na kuitumia ajenda ya fursa na vikwazo
katika maendeleo kwa ngazi zote.
Dkt
Nchimbi amesema matarajio yake ni kuona kila mshiriki wa mafunzo hayo
ana mabadiliko ya tabia katika utendaji wake ambapo mabadiliko hayo
yanaweza kupimika aidha kwa macho au viashiria vingine.
Ameongeza
kuwa matarajio ya mengine ni kuwa na Singida mpya yenye takwimu sahihi
za bidhaa zote zinazozalishwa Mkoani Singida ili kuzitumia takwimu hizo
katika kupanga mikakati ya maendeleo pamoja na kutangaza fursa zote
zilizopo Mkoani hapa.
Dkt
Nchimbi ameeleza kuwa mafunzo hayo wamepatiwa ili kutatua changamoto
zilizopo na endapo kutaendelea kuwepo kwa changamoto hizo katika sekta
mbalimbali ikiwemo za kilimo, afya, maji, elimu, barabara na utawala
bora basi tumi nzima ya fursa na vikwazo itakuwa imeshindwa.
0 comments:
Post a Comment