Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo hapo jana alifanya ziara kwenye machimbo ya
Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na Wafanyabiashara na Wachimbaji wa
Madini hayo ambapo aliwahakikishia ushirikiano wa dhati wa kufikia malengo
waliyojiwekea.
Alitembelea
maeneo ya machimbo ya Madini ya Jasi na Viwanda vidogo vya uongezaji thamani ya
madini hayo ikiwemo viwanda vya kusaga madini ya Jasi ambayo unga wake
unasafirishwa nje ya Mkoa huo, viwanda vya kutengeneza chaki vilivyopo Itigi na
kiwanda cha utengenezaji wa mapambo ya majumbani kilichopo Singida Mjini.
Naibu
Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwenye ziara ya siku Tatu ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya uchimbaji wa madini Mkoani humo ili kujionea shughuli
zinazofanywa kwenye maeneo hayo na kuzungumza na wachimbaji wa madini ili kubaini
changamoto zinazowakabili kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake.
Kwa
mujibu wa wachimbaji wa madini hayo, Madini ya Jasi hutumika kwa matumizi
mbalimbali ikiwemo kutengenezea chaki, hospitalini kwa watu waliovunjika na
kutengeneza viungo bandia, kutumika kutengenezea saruji, urembo majumbani,
hutumika kama insulation kwenye
majengo makubwa kwa kuwa Jasi huzuia moto, kutengenezea midoli na masanamu,
kutengeneza meno bandia na pia hutumika kama mbolea
0 comments:
Post a Comment