BITEKO ATANGAZA KIAMA KWA WALIOHUJUMU RUZUKU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SIMBA CEMENT YATOA MIFUKO 3000 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akitokea mifuko 3000  ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi leo katika anayeshughudia ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Mashariki leo katika anayeshughudia ni kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akimkabidhi Msaidizi wake,Abdallah Salimu mifuko hiyo mara baada ya kukabidhiwa anayeshughudia katikati nyuma ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea sehemu ya mifuko ya Saruji 3000 kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi katika kulia anaye shughudia ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akieleza mikakati ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye hayupo pichani ambaye alikwenda kiwanda hapo kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya Elimu Jimboni kwake Iramba Magharibi
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na vyombo vya habari mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya saruji ambapo alikishukuru kiwanda cha Simba Cement kwa kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake kuli ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swat
 Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement  Reinhardt Swat mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya Saruji kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya Elimu Jimboni Kwake

Sehemu ya Saruji mifuko 3000 aliyokabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba 

Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Simba Cement Reinhardt Swat wakitembelea kiwanda hicho kabla ya kukabidhiwa mifuko 3000 ya Saruji

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat kulia akimuonyesha eneo ambalo wanalotumia kwa shughuli za kiwanda Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema katika ambaye alitembelea kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho,Beny Lema 
Meneja wa Kiwanda cha Simba Cement Beny Lema akimuogoza Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kushuka ngazi mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kulia akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa ajili ya kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu kwenye Jimbo lake la Iramba Magharibi
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Jijini Tanga wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema kushoto akiwa na wafanyakazi wengine wa kiwanda hicho wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba katika akiwa na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia kushoto ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim wakiongia ukumbini kwa ajili ya kupata taarifa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga ambao nao waliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani katika makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdalla(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha) 

WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU HAWANA SOKO LA UHAKIKA LA KUUZIA ZAO HILO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Ni marobota ya tumbaku yaliyohifadhiwa kwenye moja ya ghala la chama cha Msingi Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni wakati wa uzinduzi wa soko la tumbaku lililofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Mitundu.
 
baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Itigi,wilayani manyoni Mkoani Singida wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kijiji cha Songambele,wakati wa mkutano maalumu wa baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida,Ally Minja(wa pili kutoka kushoto) akiongoza mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele.
 
 Mbunge wa jimbp la Manyoni magharibi,Yahaya Masare akichangia baadhi ya hoja kwa kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wenzake wa mkutano huo.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni,Jumanne Ismaili akiwasilisha salamu za chama kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Itigi,kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
 
WAKULIMA wa zao la tumbaku katika Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida hawana soko la uhakika la kuuzia zao hilo kutokana na Makampuni yaliyokuwa yakinunua zao hilo kushindwa kuendelea kwa sababu ya madeni makubwa yanayovikabili vyama vya msingi vinavyolima tumbaku katika Halmashauri hiyo.
Afisa Maendeleo ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo,Renatusi Mtatina aliyasema hayo kwenye mkutano maalumu wa Barazaa la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa ambaye alitaka kufahamishwa shilingi milioni 477 zitapatikanaji kwenye zao la tumbaku wakati serikali imeshusha ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi 3.
Aidha Mtatina alithibitisha kwamba ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri ya Itigi kwa mwaka huu bado haaijapata mnunuzi wa tumbaaku wala kampuni yeyote ile itakayonunua zao hilo na badala yake wakulima wataendelea kulima zao hilo na kwenda kuuza sehemu nyingine.
“Nia tunataraji kwamba watakuwepo wakulima ambao watalima lakini wanaweza wakauza sehemu nyingine lakini kwa Halmashauri ya Itigi hatujapata mnunuzi kwa hiyo patakuwa na changamoto kubwa katika kilimo cha tumbaku.”alisisitiza afisa huyo wa kilimo,umwagiliaji na ushirika.
Kwa mujibu wa Mtatina suala la matatizo ya vyama vya ushirika bado halijatatuliwa kwa sababu bado wana madeni makaubwa na ndiyo maana hawajapata mnunuzi wa zao hilo la tumbaku.
Katika swali lake la msingi,diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa alionyesha hofu ya kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri hiyo ya shilingi milioni 477 kutokana na serikali kushusha ushuru wa aina mbali mbali ya mazao,ikiwepo tumbaku,ushuru wa pamba pamoja na ushuru wa mazao mengineyo.
Kwa upande wake Mweka hazina wa Halmashauri hiyo,Charles Mnamba akitetea hoja hiyo alisisitiza kwamba katika msimu ujao uzalishaji wa kilimo cha zao la tumbaku utaongezeka zaidi ikilinganishwa na wa mwaka uliopita na utaweza kufidia kiwango cha ushuru wa asilimia mbili kilichopunguzwa na serikali.

MANYONI INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Aidha afisa elimu huyo alifa
 Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Moses Matonya(wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti,Jumanne Mlagaza wakiongoza mkutano wa baraza la Madiwani uliofanyika mjini Manyoni.
Na,Jumbe Ismailly MANYONI
HALMASHAURI ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta ya elimu ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa huku kukiwepo ongezeko la uandikishaji la asilimia 67 na hivyo kuchangia kuwepo kwa  msongamano wa wanafunzi madarasani.
Afisa elimu msingi wilaya ya Manyoni,Salumu Ikambi alisema kiasi hicho cha asilimia 67 za uandikishaji ni kikubwa kutokana na idadi ya wanafunzi  walioandikishwa kufikia 7,176 kati ya lengo la kuandikisha jumla ya wanafunzi 11,000.
Aidha afisa elimu huyo alifafanua kwamba wanafunzi hao 7,176 wakiwemo wavulana 3,734 na wasichana 3,442 ni wengi ikilinganishwa na wanafunzi 2,967 waliohitimu elimu ya msingi mwaka jana.
“Mwaka jana waliomaliza elimu ya msingi walikuwa 2,967 kwa idadi hiyo utaona karibu mara tatu ya wale ambao wameandikishwa mwaka huu.”alibainisha Ikambi.
Kwa mujibu wa Ikambi alizitaja baadhi ya changamoto wanazokaniliana nazo kuwa ni idadi ya vyumba vya madarasa vilivyokuwepo mwaka jana ndivyo hivyo hivyo vilivyo mwaka huu na idadi ya wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi 60 lakini walioandikishwa ni 200.
Hata hivyo alisisitza pia kwamba pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa lakini kuna maeneo mengine pia bado yanakabiliwa na upungufu wa walimu na kutoa mfano kuwa darasa lenye wanafunzi 200 haliwezi kufundishwa na mwalimu mmoja.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Ramlah Munisi alibainisha kwamba mpaka sasa ni asilimia 14 ya wanafunzi 2,018 bado hawajaripoti shule kuanza masomo yao ya kidato cha kwamba kutokana na sababu mbali mbali ikiwepo kubadili vituo kutokana na umbali wa kutoka wanapoishi hadi shule walizopangiwa.
Afisa elimu huyo hata hivyo aliweka bayana kuwa kwa mwaka 2018 Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilipokea wanafunzi 2027 waliojiunga na masomo ya kidato cha kwanza na kati yao,wanafunzi 9 wamepangwa katika shsule za vipaji maalumu.
Kwa mujibu wa Munisi mwenye dhamana ya kusimamaia elimu sekondari,wanafunzi 2,018 wamepangiwa shule za kata,ambapo kati yao 1,970 sawa na asilimia 82.5 wamesharipoti shuleni na asilimia 2.8 wameenda katika shule za watu binafsi.
Akifunga mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Moses Matonya aliwakumbusha madiwani wajibu wao wa kwenda kusimamia mahudhurio ya wanafunzi wa shule za msingi pamoja na sekondari.

WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba wakiwa kwenye viwanja vya mikutano ya Kijiji hicho wakipatiwa mafunzo na Kituo cha Msaada wa sharia kwa wanawake (WLAC) juu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji pamoja na madhara yake.
Bi Esther Kileee (aliyemshikilia mkono ni Afisa mtendaji wa kata ya Ndago) kwanza    akitoa ushuhuda wa kuacha kujishughulisha na vitendo vya ukeketaji baada ya kuokoka na kwamba kabla ya kuokoka alikuwa akinufaika na shughuli hizo kwa kumpatia kipato chake na alaikuwa akiwakeketa wanawake wasiopungua 50 kwa mwezi.
  Mwanasheria wa WLAC,  Abia Richard akiwasilisha mada kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Kata ya Ndago,wilayani Iramba ambapo pamoja na mambo mengine alisema katika kipindi cha wiki moja zaidi ya watu 1000 walipatiwa mafunzo na kati yao,wanafunzi ni 600 na watu wazima ni 500.
 Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard ajiteta jambo na afisa mtendaji wa kata ya Ndago, Abeli Philipo Shaluo.
Igizo linaloashiria mwanaume anayemnyanyasa mkewe kwa kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia.(Picha  zote Na Jumbe Ismailly)
Na Jumbe Ismailly- IRAMBA

KITUO cha Msaada wa sheria kwa Wanawake( WLAC) kimeanza kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili kwa kijinsia na ukeketaji pamoja na madhara yake kwa watoto wa shule za msingi za Nguvumali,Songambele na sekondari ya Ndago wilayani Iramba,Mkoani Singida ambapo katika kipindi cha wiki moja jumla ya wanafunzi 600 kutoka katika shule za msingi na sekondari walinufaika na mafunzo hayo.

Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa sheria na Wanawake (WLAC) Abia Richard aliyasema hayo kwenye mafunzo waliyotoa kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Tarafa ya Ndago,wilayani Iramba.

Aidha Mwanasheria huyo wa WLAC alifafanua kwamba katika kipindi hicho cha wiki moja zaidi ya watu 1000 wameshapatiwa mafunzo hayo ambayo kati ya hao wanafunzi wa darasa la tano mpaka la saba wa shule za msingi na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni 600 na watu wazima ni 500.

Akizungumzia sababu za kwenda kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi,Abia amezitaja kuwa  ni kizazi na taifa la kesho,jambo ambalo endapo wakifahamu madhara yake mapema watakapokuwa wakubwa itakuwa rahisi kuepukananavyo.Kwa mujibu wa Abia kituo cha msaada wa sheria na Wanawake na watoto kikifadhiliwa na The Foundation For Civil Society kimekuwa kikiendesha mradi wake wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa wanawake.

“Kwa hiyo tumefika katika wilaya ya Iramba,kata ya Ndago katika Kijiji cha Zinziligi kwa ajili ya kuongea na wanakijiji wa Zinziligi kujua ni aina gani ya ukatili wa kijinsia ambao unakumbana na wananchi wa Kijiji hicho pamoja na kupanga mkakati ni kwa namna gani wananchi hao wataepukana na ukatili huo”alisisitiza Mwanasheria huyo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndago,Abeli Philipo Shalua alithibitisha kwamba asilimia 85 ya wanawake ndiyo wanaonyanyasika sana kwa waume zao na kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka jana mpaka sasa kuna matukio ya ukatili wa kijinsia 13 waliyofanyiwa wanawake.

Naye Mchungaji wa Kanisa la EAGT Zinziligi,Rejina Matoke huku akinukuu maandiko matakatifu aliweka bayana kuwa kitu kinachouwa nyumba za familia nyingi na kushindwa kuendelea ni tamaa ya uzinzi kwani hivi sasa suala la uzinzi limekamata watu wengi.“Zinziligi imekamatwa na uzinzi nasema ile kweli halafu kuna magonjwa ya kutisha hapa,hata kama leo daktari ataleta kipimo watakaopona ni wachache,idadi kubwa hapa ni taabu tu,watu hawajiheshimu”alisisitiza Mchungaji huyo.
 

DC MLOZI: MADIWANI FUATILIENI MAKUSANYO KATIKA STENDI YA TABORA KUZIBA UPOTEVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KATIBU WA NEC IDARA YA SUKI, NGEMELA LUBINGA AMNADI MGOMBEA WA CCM JIMBOLA SINGIDA KASKAZINI LEO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa