MAZISHI YA BABA WA MBUNGE MARTHA MLATA JANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Mbunge Martha Mlata akifarijiwa na waliohudhuria mazishi ya baba yake mzazi. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania ‘CHAMUITA,’ Stella Joel na mwakilishi wa wasanii wa filamu, Dokii.



Baadhi ya wabunge na ndugu wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya kaburi la baba mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida ambaye pia ni msanii wa nyimbo za injili, Martha Mlata.

MWENYEKITI UVCCM SINGIDA ASIMAMISHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida limemsimamisha uongozi Mwenyekiti wao wa mkoa, Martin Labia Lissu kwa madai ya kushindwa kutoa utetezi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Katika kikao chake kilichofanyika jana kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Singida na kuhudhuriwa na wajumbe 24 wa baraza hilo kwa kauli moja wameridhia hatua hiyo na kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Joseph Saenda aliwaambia waandishi wa habari kuwa kikao kilikuwa na agenda moja ya kumwita mbele ya baraza mwenyekiti wao, Lissu.
Alisema baraza baada ya kujadiliana kwa pamoja, wajumbe hawakuridhishwa na majibu ya utetezi wake, kwani hakuonesha kukiri kufanya makosa mbele ya wajumbe wa kikao.
“Baada ya mjadala wa muda mrefu baraza limemsimamisha uongozi, kwa mujibu ya katiba ya UVCCM ibara ya 78 (i) na kutoa mapendekezo ya kumvua uongozi kwa ngazi ya juu yenye mamlaka hayo kikatiba,” alisistiza.
Mei 17 mwaka huu, wajumbe wa baraza hilo kwa kauli moja walidai kutokuwa na imani na uongozi wa mwenyekiti huyo kutokana na kutumia vibaya madaraka yake na kuwa mtovu wa nidhamu na kudharau viongozi wa juu wa chama.
Saenda aliorodhesha tuhuma zilizokuwa zikimkabili Mwenyekiti huyo kuwa ni kushindwa kuitisha vikao tangu achaguliwe mwaka 2012 na kushindwa kushiriki ziara mbalimbali za viongozi ndani ya chama. Mwenyekiti huyo pia alikuwa akituhumiwa kuwa mchonganishi kati ya viongozi wa UVCCM na chama na kushindwa kufanya kazi zake na badala yake kujikita zaidi kwenye kampeni za mmoja wa wagombea nafasi ya urais mwakani.
Meneja wa duka jipya la huduma kwa wateja la Vodacom lililopo Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam, Swaum Manengelo akifungua mlango kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo uliofanyika juzi.
Chanzo:Tanzania Daima 

KIGODA ATAKA TAFITI ZITUMIKE KUTUNGA SERA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda
Watafiti nchini wametakiwa kuwasilisha matokeo ya tafiti zao serikalini, ili zitumike katika kutengeneza sera zinazohusiana na maendeleo ya watu.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uendelezaji wa ujasiriamali  na biashara ndogo na za kati, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Hotuba ya Dk. Kigoda ilisomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo.

Dk. Kigoda, alisema kuna tafiti nyingi zimefanywa na wanataaluma tofauti, lakini hazijaisaidia jamii kwa vile zimehifadhiwa kwenye makabati ndani ya taasisi wanazozifanyia kazi badala ya kuziweka wazi kwa jamii ikiwamo kuziwasilisha serikalini.

Aliwataka watafiti, wajasiriamali, wanataaluma  na wakurugenzi wa mashirika zaidi ya 150 wanaoshiriki mkutano huo wa siku mbili, kufanya majadaliano na tafiti ambazo zitaleta mawazo yaliyo na umuhimu kwa Watanzania.

“Haya mambo ya tafiti yana mambo mengi, sasa na ninyi myaangalie hayo, mkae chini na kutafakari na kuleta mawazo ambayo yatawasaidia Watanzania, kwani mnaweza kufanya tafiti zisiwe na faida kwa mazingira ya Tanzania, lakini yakawa ni mazuri kwa mazingira ya nchi nyingine,” alisema.

Dk. Kigoda, alisema mchango wa biashara ndogo ndogo ni mkubwa na muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa na kupunguza umaskini, hivyo serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili wajikomboe kiuchumi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Profesa Yunus Mgaya, alisema kila mwaka shule ya biashara ya chuo hicho (UDBS), inaandaa mkutano kama huo, ili kuwakutanisha watafiti kutoka vyuo vikuu mbalimbali pamoja na wajasiriamali.

Alisema lengo la mikutano hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu na kusaidiana kwenye masuala ya kitaalamu.

Profesa Mgaya, alisema serikali ni lazima iwe na sera za kuwasaidia wajasiriamali, na ndiyo maana wamekuwa wakiishirikisha kwenye mikutano yao kwa kuwa mchango wa wafanyabiashara wadogowadogo ni mkubwa na unatoa ajira kwa watu wengi.
 
SOURCE: NIPASHE

MWANAFUNZI MLEMAVU MIKONO YOTE MIWILI AOMBA MSAADA WA JK

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC08466
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Julius Charles (12) ambaye anatumia mguu wa kulia kuandika kutokana na kutokuwa na mikono.Pia anatumia mguu huo kutandika kitanda chake.
DSC08477
DSC08482
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Olivary Kamilly, akimsaidia mwanafunzi Julius Charels Kumvalisha soksi baada ya kutoka darasani.
DSC08497
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wailaya ya Ikungi, Julius Charles, akitandika kitanda chake kwa kutumia mguu wake wa kulia ambao pia anautumia katika kuandika.
DSC08506
Matroni wa mabweni ya kulala wanafunzi walemavu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Modesta Macha, akiwa na wanafunzi wa darasa la sita Julius Charels.
DSC08508
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Julius Charles,akichukua daftari lake kwa ajili ya kulihifadhi kwenye mfuko wake. Julius anatumia mdomo kwa vile hana mikono.
Na Nathaniel Limu, Ikungi
MWANAFUNZI wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Julius Charles (12) ambaye hana mikono ameiomba serikali imsaidie kupata mtu atakaye mhudumia ili aweze kusoma kwa uhuru zaidi aweze kufikia lengo lake la kusoma hadi chuo kikuu.

Julius amesema amefikia uamuzi huo wa kuomba kupatiwa mtu wa kumhudumia kutokana na kutokuwa na mikono.

Amedai ulemavu huo, umesababisha pamoja na mambo mengine atumie mguu wake wa kulia kuandika na kutandika kitanda.

Julius amefafanua zaidi kwa kusema ulemavu wake huo vile vile, unasababisha ashindwe kuoga,kufua nguo zake na kwamba anapata taabu kubwa wakati wa kujisaidia chooni.
"Kutoa madaftari na kalamu ndani ya mfuko,natumia mdomo wangu.Pia kwa vile sina mikono natumia mdomo kuchukua chakula kutoka kwenye sahani",amesema.

Julius anasema binafsi anamshukuru na kumpongeza rais Kikwete,kwa moyo wake wa kuwajali walemavu wa aina mbalimbali.

"Nina imani kwamba kama ningeonana na Rais Kikwete kwa jinsi anavyowajali walemavu mimi mwenye uchu mkubwa wa kujisomea ataweza kunisaidia kupata mtu wa kunihudumia.Hata hivyo,sikati tamaa kusaidiwa na Rais wetu Kikwete.Akisoma habari hii kwenye Mtandao huu,nina hakika atanisaidia ili ndoto yangu ya kufika chuo kikuu siku moja iweze kuwa kweli",amesema Julius.

Kwa mujibu wa mwalimu wake,Ana Mjema, Julius kwenye mitihani mbalimbali huwa anashika nafasi ya tatu au ya nne.

Amesema mwanafunzi huyo asiye na mikono,kwa kutumia mguu wake ana mwandiko mzuri kuliko wanafunzi wasio na ulemavu.Pia ana kasi katika kuandika.

(Picha zote na Nathaniel Limu).

MO ATAKA MADHEBEBU DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC_0575
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.
Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.
DSC_0467
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila vikwazo",amesema.
Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya dini",amesema.
Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.

MH. MOHAMMED G.DEWJI (MO) AMWAGA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 127 KWENYE TAASISI ZA DINI ZAIDI 80 JIMBONI KWAKE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
DSC_0025
Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.
DSC_0029
Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
DSC_0133
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
DSC_0171
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
DSC_0237
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
DSC_0262
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
DSC_0287
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.
DSC_0314
Jengo la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko ya Saruji 50.
DSC_0713
Mheshimiwa Mohammed Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.
DSC_0729
Mbunge MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0738
MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara ambao umeitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.
DSC_0750
Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.
DSC_0336
Watoto wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0343
Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.
Kwa picha zaidi bofya hapa

KINANA AWASILI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndugu Lazaro Nyalandu katika kijiji cha Kaskazi mkoani Singida,Katibu Mkuu atakuwa kwenye ziara ya siku nane mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana na mafundi kupandish bati wakati wa ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Mgando,Singida
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa CCM mkoa wa Singida na Kundi la akina mama wajasiriamali wa Itagata kuelekea kwenye mkutano wa hadhara  baada ya kufungua shina la akina mama hao wa Itagata,Singida.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa bwawa la maji la Itagata,Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Itigi mkoani Singida .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Itigi na kuwaambia  CCM ipo imara na kuwaambia wananchi hao muungano  wa vyama vya siasa unaofahamika  kama UKAWA ndio utahitimisha maisha ya baadhi ya vyama vya siasa nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma barua ya wakazi wa Tura ambao wanahitaji kujengewa kivuko kwenye reli ili kuwasaidia kwenda kuchota maji bila matatizo kwani kwa sasa wanapata tabu,Katibu Mkuu alisimama Tura kuwasalimu wananchi na kisha kuendelea na safari kuelekea Singida.

AJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 16 MLIMA SENKENKE MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza. 

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
Dk Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam (34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
Kwa mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.

Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.
Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.


Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.

Waandishi wa habari wapewa changamoto ya ubunifu, kujituma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Nathaniel Limu, Singida
WAANDISHI wa Habari mkoani Singida, wamehimizwa kuondokana na uandishi habari wa mazoea na badala yake wabadilike na kuwa wabunifu ili kazi yao iweze kukidhi viwango vya wakati uliopo.
Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni na mwandishi wa habari mkongwe, Eda Sanga wakati akizungmza kwenye semina ya Uhabarisho wa Mfuko wa Habari Tanzania (Tanzania Media Fund TMF) kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida.
Amesema waandishi wa habari ule wa business as usual, haufai umepitwa na wakati unadumaza maendeleo ya mhusika.
amesema uandishi wa habari kwa sasa umetakiwa mwandishi wa habari ujitume, uwe mbunifu, ufanye uchunguzi wa kina ili ukiandika habari watu wakupongeze au wakusifu.
pics 3“Ninyi mnapaswa katika kutekeleza majukumu yenu muiangalie Singida kwa upana wake. Ni kero gani zinawasibu wananchi. Nini kifanyike ii kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kero hizo”
  Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida,wakifuatilia mada   zilizokuwa zinatolewa na maafisa kutoka Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) juu ya kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na mfuko huo.Picha na Nathaniel Limu.
pics 1Afisa kutoka Mfuko wa Waandishi wa Habari Tanzania (TMF) Alex Kanyambo akitoa mada yake juu ya umuhimu wa vilabu vya waandishi wa habari kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na TMF.Wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa TMF,Japhet Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Seif Takaza.
Kwa hali hiyo, aliwataka kujitathimini juu ya utendaji wao wa kila siku na wahakikishe habari zao zisiwe na upande moja mbali ziwe ‘balanced’.
pics2Mwandishi wa habari mkongwe nchini,Eda Sanga akizungumza kwenye semina ya uhabarisho juu ya shughuli za Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyohudhuriwa na waandishi wa habari mkoa wa Singida.
Awali Afisa Habari wa TMF makao makuu,Japhet Sanga amewahimiza waandishi wa habari nchini kujenga utamaduni wa kuomba uwezeshaji wa fedha kutoka TMF ili pamoja na mambo mengine kuongeza uzoefu zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
Akifafanua, amesema TMF inatoa ruzuku ya fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi ambazo zinaibua mambo mengi mapya na hasa kero zinazowakabili wananchi wakiwemo wa vijijini.
“TMF tunaamini kwamba kwa vyo vyote habari za uchuguzi zitamwezesha mwandishi husika kujifunza mambo mapya kwa hiyo atakuwa amepanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi”.,amesema.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa