Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida limemsimamisha
uongozi Mwenyekiti wao wa mkoa, Martin Labia Lissu kwa madai ya
kushindwa kutoa utetezi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Katika kikao chake kilichofanyika jana kwenye ofisi za CCM Mkoa wa
Singida na kuhudhuriwa na wajumbe 24 wa baraza hilo kwa kauli moja
wameridhia hatua hiyo na kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika kwa hatua
zaidi.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Joseph Saenda aliwaambia waandishi wa
habari kuwa kikao kilikuwa na agenda moja ya kumwita mbele ya baraza
mwenyekiti wao, Lissu.
Alisema baraza baada ya kujadiliana kwa pamoja, wajumbe
hawakuridhishwa na majibu ya utetezi wake, kwani hakuonesha kukiri
kufanya makosa mbele ya wajumbe wa kikao.
“Baada ya mjadala wa muda mrefu baraza limemsimamisha uongozi, kwa
mujibu ya katiba ya UVCCM ibara ya 78 (i) na kutoa mapendekezo ya kumvua
uongozi kwa ngazi ya juu yenye mamlaka hayo kikatiba,” alisistiza.
Mei 17 mwaka huu, wajumbe wa baraza hilo kwa kauli moja walidai
kutokuwa na imani na uongozi wa mwenyekiti huyo kutokana na kutumia
vibaya madaraka yake na kuwa mtovu wa nidhamu na kudharau viongozi wa
juu wa chama.
Saenda aliorodhesha tuhuma zilizokuwa zikimkabili Mwenyekiti huyo
kuwa ni kushindwa kuitisha vikao tangu achaguliwe mwaka 2012 na
kushindwa kushiriki ziara mbalimbali za viongozi ndani ya chama.
Mwenyekiti huyo pia alikuwa akituhumiwa kuwa mchonganishi kati ya
viongozi wa UVCCM na chama na kushindwa kufanya kazi zake na badala yake
kujikita zaidi kwenye kampeni za mmoja wa wagombea nafasi ya urais
mwakani.
Meneja wa duka jipya la huduma kwa wateja la Vodacom lililopo Sinza
Afrika Sana jijini Dar es Salaam, Swaum Manengelo akifungua mlango
kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo uliofanyika juzi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment