Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya,Ahmed Msangi (wa tatu kulia)
akishiriki mchakamchaka muda mfupi kabla mwenge wa uhuru kukibidhiwa kwa
uongozi wa mkoa wa Singida, katika kijiji cha Rungwa tarafa ya Itigi
wilaya ya Manyoni.
Na Nathaniel Limu, Singida
WAKAZI
wa Manispaa ya Singida,wamehimizwa kulima zao la mtama linalohimili
ukame kama inavyoelekezwa na uongozi wa mkoa ili waweze kuondokana na
uhaba wa chakula katika kipindi chote cha mwaka.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
Kitaifa,Rachael Stephen Kasanda kwa nyakati tofauti wakati akizungumza
na wananchi wa Manispaa ya Singida katika maeneo yaliyotembelewa na
mwenge huo.
Amesema
zao la mtama ni zao la asili na limepewa kipao mbele na serikali ya
mkoa kwa hivyo wakulima hawana budi kuongeza bidii katika kupanua
mashamba ya zao hilo ili waweze kujitosheleza kwa chakula na kupata
ziada ya kuuza wajipatie kipato.
“Kijiji
chenu mnakiita Mtamaa,sijui linatokana na zao linalohimizwa sana na
mkuu wa mkoa,Dk.Parseko Kone,au lina maana tofati.Lakini ukweli unabaki
pale pale kuwa zao la mtama,ni zao pekee litakalo hakikisha mkulima
hakabiliwi na njaa kabisa”,alifafanua.
Mkuu
wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Fatuma Toufiq, (kushoto)
akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi leo ili uweze
kukimbizwa kwenye halmashauri ya manispaa ya Singida.
Katika
hatua nyingine, kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru, amesema upo
umuhimu mkubwa mtala wa elimu wa sasa ukafafanua zaidi juu ya mwenge,
ili vizazi vya sasa na vijavyo viwe na ufahamu mkubwa waweze kuuenzi.
Amesema
mtama wa sasa unataja tu uwepo wa mwenge wa uhuru bila kufafanua
zaidi,kitendo kinachochangia kizazi cha sasa kipate wakati mgumu katika
kujua umuhimu wake.
“Muasisi
wa nchi hii,mwalimu Julius Nyerere,aliamua kuwasha mwenge wa uhuru muda
mfupi baada ya Tanganyika kupata uhuru,kwa lengo kuangaza mahali hakuna
upendo, pawepo na upendo, mahali hakuna matumaini, yawepo
matumaini”,amesema.
Akifafanua
zaidi amesema kwa vile mwenge wa uhuru haukutolewa ufafanuzi au kueleza
umuhimu wake kuwepo,kunachangia baadhi ya Watanzania wachache, kuanza
kumdhihaki mwalimu Nyerere bila aibu.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Ng’aida manispaa ya
Singida,waliofanikiwa kupata nafasi adimu ya kugusa Mwenge wa uhuru
uliozindua vyoo bora katika shule hiyo.
“Uzoefu
unaonyesha kuwa makundi mbalimbali ya kanda za
wafanyakazi,yanashikamana wakati wa raha na wa taabu.Lakini nashangazwa
na Chama cha walimu Tanzania (CWT),walimu wamekaa kimya wakati mwalimu
mwezao hayati Julius
Nyerere,akidhihakiwa ovyo hadharani na ndani ya bunge,bila wao kutoa tamko”.amesema kiongozi huyo kwa masikitiko.
Rachael
amesema wakati walimu Tanzania wamekaa kimya wakati mwenzao pamoja na
kuwa amefariki dunia miaka mingi,lakini wakiitwa kushiriki maandamano
yasiyo na tija yo yote, haraka wanashiriki na kupoteza muda wao mwingi.
Kiongozi
wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Rachel Stephen Kasanda, akizindua
rasmi choo bora cha shule ya msingi manispaa ya Singida.
Kiongozi
wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu, Rachel Kasanda,
akizungumza na wananfunzi na wazazi/walezi wa shule ya msingi Ng’aida
manispaa ya Singida.Kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Moja
ya vyoo bora vya shule ya msingi Ngaida manispaa ya Singida
vilivyozinduliwa jana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,
Rachel Kasanda ambaye alihimiza kuwepo kwa maji ya kutosha kwa ajili ya
matumizi ya vyoo hivyo.(Picha na Nathaniel Limu).
0 comments:
Post a Comment