Huyu ndiye Miss Singida 2014 Doris Mole (23) akiwa na mshindi wa pili Blath Chambo na mshindi wa tatu Lulu Abdul.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Doris
 Molel (23) Mwanafunzi katika chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere 
Jijini Dar es Salam anayesomea siasa na Maendeleo ya Jamii mwaka wa 
tatuametwaa taji la Miss Singida Redds 20014.
Katika
 shindano hilo lililofanyika jana kwenye ukumbi wa chuo ha Uhazili Mjini
 hapa Molel, mbali na kutwaa taji hilo alijinyakulia kitita cha shilingi
 laki tano.
Nafasi
 ya pili ilichukuliwa na Blath Chambo ambaye aliambilia kiasi cha 
shilingi laki tatu huku mshindi  wa tatu Lulu Abdul akipata shilingi 
laki mbili.
Shindano
 hilo lilipambwa na wasanii mbalimbali akiwemo mama wa mipasho na 
taarabu, Hadija Kopa na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava.
Mgeni rasmi mama balozi Seif Idd akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi laki tano Miss Singida.
Mapema
 mgeni rasmi Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar Assi Balozi Seif Iddy 
aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya ulimbwende hapa nchini 
kujitambua, kusoma na kujiwekea malengo maalum.
Aidha
 aliwataka wasidanganyike na kujiona kuwa wao ni bora na hivyo kufanya 
vitendo viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao ikiwa ni pamoja na 
kijiingiza katika mapenzi mapema.
Katika
 kumuunga mkono muandaaji wa shindano hilo Mkoani Singida, Bora Lemmy 
Mama Seif Iddi alimpatia kiasi cha shilingi laki sita ili aweze 
kuongezea washindi zawadi.
Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora ya Miss Singida 2014.
Majaji wakiwa Kazini kwa makini.
Miss Singida akipita mbele kusalimia mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa mshindi.
Miss Singida akicheza muziki na mgeni rasmi.
Mamiss wenzake wakifurahia pamoja na mshindi Doris Molel.
Mameneja wa Coca Cola ambao nao walidhamini shindano hilo.
Mwandishi wa MO Blog Mkoa wa Singida Hillary Shoo, akiwa amepozi na mkewe Mama Hope.
Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy mama Assa akizungumza kwenye shindano la kumtafuta Miss Singida 2014.
Mama wa Mipasho Khadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani kabla ya kuanza shindano hilo.
Mwakilishi wa METL Singida Hasan Mazala akitoa nasaha zake mbele ya mgeni Rasmi.
METL mojwawapo ya wadhamini wa shindano hilo kwa miaka 13 sasa.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO WA MO BLOG).
       
0 comments:
Post a Comment