Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WATU  watatu akiwemo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ngimu 
katika Halmashauri  ya Wilaya ya Singida, wamekufa na wengine 10 
kujeruhiwa baada ya gari aina ya  Noah waliyokuwa wakisafiria kuacha 
njia na kupinduka katika Kijiji cha Ijanuka,  Manispaa ya Singida.
  Mganga  Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dk. Deogratius 
Banuba, aliwataja  waliopoteza maisha kuwa ni Mkuu wa Shule ya Sekondari
 ya Kata ya Ngimu, Tatu  Bunku mwenye umri wa kati ya miaka 45 na 50 
aliyefia hospitali ya mkoa  alipokuwa akipatiwa matibabu, dereva wa gari
 hilo, Enock Mbaga (31) mkazi wa  Arusha na Hajira Ikhala (21) 
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngumbu, mkoani  Shinyanga aliyefariki 
dunia papo hapo.
  Aliwataja waliolazwa hospitali hapo kuwa ni  Ramadhani Hamisi (46) 
mkazi wa Kijiji cha Sepuka, Adamu Juma (28) mkazi wa  Kijiji cha Mgori 
na Mariamu Ramadhani (6) mkazi wa Kijiji cha Sepuka.
  Wengine ni Asha Saidi (26) Neema Mwiru (44) na  Teddy Kesi (24) wakazi
 wa Kijiji cha Ngimu, Therecie Pantaleo (14) mkazi wa  Kijiji cha 
Ilongero, Wilieliamana Elisante (24) mkazi wa Kijiji cha Mang’onyi  na  
Adamu Kiula (24).
  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida,  Mrakibu Mwandamizi wa 
Polisi (SSP), Claud Kanyorota, alisema ajali hiyo  ilitokea jana, saa 
moja asubuhi katika eneo la Kijiji cha Ijanuka.
  Alisema  uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
 kasi wa gari hilo T 227 BLN Toyota Noah  uliosababisha tairi la gari 
hiyo iliyokuwa na abiria 13 kupasuka na hivyo  kupinduka.
  Kaimu  kamanda huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waendesha 
vyombo vya moto kuwa  makini na kuepuka kujaza abiria zaidi ya uwezo wa 
vyombo husika pamoja na  kuepuka mwendo kasi.
Chanzo:Tanznia Daima  
0 comments:
Post a Comment