Mratiibu
msaidizi wa polisi mkoa wa Singida,Irene Mbwatila,(anayeangalia
kamera),akizungumza na timu ya pamoja ya maafisa wa shirika la HAPA,YMC
na RFSU, inayofanya utafiti juu ya mradi wa ushiriki sawa wa wanaume
katika afya ya uzazi na ujinsia.
Baadhi
ya wanaume wakiwa na wake zao wakazi wa kijiji cha Ntuntu wilaya ya
Ikungi mkoa wa Singida, wakiwa kwenye foleni katika kliniki ya kijijini
hapo,wakisubiri kuingia kumwona muuguzi. Elimu iliyotolewa kwa pamoja na
mashirika ya HAPA na YMC,ya umuhimu wa ushiriki sawa wa wanaume katika
afya ya uzazi na unjisia, katika kipindi cha miaka mitatu, imechangia
wanaume pamoja na mambo mengine, kusindikiza wake zao kliniki kutoka
asilimia 0 hadi 80 ya sasa.
Muuguzi
wa zahanati ya kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary
Lema, akitoa dawa kwa mama mjamzito Lucia Hongoa, huku mume wake Edward
akiwa anashuhudia. Kijiji cha Ntuntu ni moja ya vijiji ambavyo elimu ya
ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia,inatolewa.
Muuguzi
wa zahanati ya kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary
Lema akitoa taarifa yake juu ya utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa
wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani). (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi
ELIMU
ya ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia inayotolewa
kwa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ya HAPA na YMC imezaa
matunda baada ya wanaume kubadilika, na kuanza kusindikiza wake zao
klinki na kusaidia kazi zote za nyumbani,imeelezwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, muuguzi wa kliniki ya zahanati ya
kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary Lema, amesema
kuwa miaka mitatu iliyopita,hakukuwa na mwanaume anayesindikiza mke wake
klinki.
Alisema
elimu hiyo imewahamasisha na kuwaelimisha wanaume ambao kwa sasa
wanashiriki kikamilifu, afya ya uzazi na ujinsia kutoka asilimia 0 hadi
80.
Lema amesema kuwa kwa sasa kama mwanaume hajamsindikiza mke wake mjamzito kliniki,atafanya hivyo kwa sababu za msingi.
“Kwa
kawaida wanaume wakazi wa wilaya hii na mkoa kwa ujumla,huwa ni mwiko
kusindikiza mke kliniki au kufanya kazi zingine za nyumbani kama kufua
nguo,kupika,kuchota maji na kusenya kuni.Lakini baada ya elimu hii ya
ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia
kutolewa,wanaume karibu wote,wamebadilika”,alifafanua.
Akifafanua
zaidi,alisema kuwa wanaume karibu wote wa kijiji cha Ntuntu kwa sasa
wanafanya/wanashiriki shughuli zote za nyumbani sawia na
wanawake,kitendo kinachoboresha sana mahusiano na mapenzi.
Kwa
upande wake Ana Charles, amesema kuwa baada ya elimu hiyo kutolewa
kijijini hapo, wanaume wamebadilika mno kwa kuwa wapole, kuwahi kurudi
nyumbani na mapenzi yameboreka zaidi.
“Kwa
sasa wanaume wetu wamejenga tabia ya kuambatana nasi kwenda kupata moja
baridi kitendo ambacho hakikuwepo miaka mitatu iliyopita.Pia wamekuwa
wapole hatupigwi ovyo kama ilivyokuwa zamani”,amesema Ana huku
akitambasamu.
0 comments:
Post a Comment