Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewatuhumu Rais Jakaya Kikwete
na Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa kugeuza Ikulu kuwa kituo cha
kuanzisha taasisi binafsi.
Shutuma hizo zilitolewa juzi na Mkurungenzi wa Sera na Utafiti wa
CHADEMA, Mwita Waitara, wakati akihutubia mikutano ya hadhara kwa
nyakati tofauti katika kata za Saranda na Makuru wilayani Manyoni,
Singida.
Waitara alisema katika uongozi wao, marais hao waliwaruhusu wake zao kuanzisha taasisi binafsi kwa kutumia rasilimali za umma.
“Rais Mkapa alimruhusu mke wake Anna, akaanzisha Mfuko wa Fursa Sawa
kwa Wote (EOTF) jambo ambalo limejirudua tena kwa mke wa Rais Kikwete,
Salma aliyeasisi Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).
“Ndugu zangu, katiba iliyopo haisemi chochote kuhusu mke wa rais
kutumia Ikulu kuanzisha taasisi yake,” alisema Waitara, huku akiwataka
wananchi kudai katiba mpya wanayoitaka.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na
Jaji mstaafu Joseph Warioba inataka zawadi zote anazopewa mke wa rais
nje ya nchi, lazima iwe mali ya umma sio yake binafsi kama inavyofanyika
sasa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Singida, Shabani Limu, aliwaomba wananchi wa
mkoa huo kujiandikisha kwa wingi kwenye maboresho ya daftari la
wapigakura yaliyopangwa kufanyika Septemba.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment