Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKA
la Mpango Endelevu wa Uboreshaji Mazingira (SEMA), limetumia zaidi ya
sh milioni 25 kununua vifaa vyenye ujumbe utakaowasaidia wakulima
kubadilika ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa shirika hilo lisilo la kiserikali, Ivo
Manyaku mkoani hapa mwishoni mwa wiki, alipotoa taarifa ya utekelezaji
wa programu hiyo.
Manyaku alitaja vifaa vilivyonunuliwa kwa lengo la kuwasaidia
wakulima kuwa ni vinyago 30, fremu 48 zenye ujumbe mbalimbali, shajara
33, mabango 48, vipeperushi 300 na magari sita ya abiria yamebandikwa
stika zenye ujumbe.
“Lengo kuu la hii programu ni kuona wadau mbalimbali wakiwemo
serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na raia mwenyewe
wakishirikiana, wakiwajibika na kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi ngazi zote,” alisema.
Alisema madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ni joto,
ukame, mafuriko, vimbunga vikubwa, magonjwa na kupungua kwa vina vya
maji katika vyanzo mbalimbali.
Alisema upo uwezekano wa kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya
tabia nchi kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kuendesha kilimo bora na
ufugaji wenye tija.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment