Na Nathaniel Limu, Singida
WAANDISHI wa Habari mkoani Singida,
wamehimizwa kuondokana na uandishi habari wa mazoea na badala yake
wabadilike na kuwa wabunifu ili kazi yao iweze kukidhi viwango vya
wakati uliopo.
Changamoto hiyo imetolewa hivi
karibuni na mwandishi wa habari mkongwe, Eda Sanga wakati akizungmza
kwenye semina ya Uhabarisho wa Mfuko wa Habari Tanzania (Tanzania Media
Fund TMF) kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida.
Amesema waandishi wa habari ule wa business as usual, haufai umepitwa na wakati unadumaza maendeleo ya mhusika.
amesema uandishi wa habari kwa sasa
umetakiwa mwandishi wa habari ujitume, uwe mbunifu, ufanye uchunguzi wa
kina ili ukiandika habari watu wakupongeze au wakusifu.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa
Singida,wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na maafisa kutoka
Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) juu ya kuchangamkia ruzuku zinazotolewa
na mfuko huo.Picha na Nathaniel Limu.
Kwa hali hiyo, aliwataka
kujitathimini juu ya utendaji wao wa kila siku na wahakikishe habari zao
zisiwe na upande moja mbali ziwe ‘balanced’.
Awali Afisa Habari wa TMF makao
makuu,Japhet Sanga amewahimiza waandishi wa habari nchini kujenga
utamaduni wa kuomba uwezeshaji wa fedha kutoka TMF ili pamoja na mambo
mengine kuongeza uzoefu zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
Akifafanua, amesema TMF inatoa ruzuku
ya fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi
ambazo zinaibua mambo mengi mapya na hasa kero zinazowakabili wananchi
wakiwemo wa vijijini.
“TMF tunaamini kwamba kwa vyo vyote
habari za uchuguzi zitamwezesha mwandishi husika kujifunza mambo mapya
kwa hiyo atakuwa amepanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi”.,amesema.
0 comments:
Post a Comment