Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Muuguzi wa Wodi Namba Nne katika Hospitali ya Mkoa wa Singida,
Belta Lyamboko amesema alipoanza kazi katika hospitali hiyo mwanzoni mwa
mwaka 1981, alimkuta Mzee Abdi Lanjuu (75) na sasa anajiandaa kustaafu
akiamini atamwacha mzee huyo hospitalini.
Mzee Lanjuu amelazwa hospitalini hapo kwa miaka 43
sasa baada ya kupata ajali ya lori mwaka 1971, alipokuwa mtumishi wa
iliyokuwa Mamlaka ya Pamba Tanzania (TCA), Mkoa wa Mwanza.
Kuishi kwake hospitalini hapo kwa miaka mingi,
kumechangiwa na kutokuwa na ndugu wala rafiki wa kumhudumia. “Wakati
ninaanza kazi nikiwa kijana, Mzee Abdi alikuwa na nguvu na alikuwa
akitembelea kiti cha magurudumu, lakini katika miaka mitatu au zaidi
hali yake imekuwa mbaya na hawezi kutembea hata kwa kutumia kiti chake
cha magurudumu. Kila kitu pamoja na kula anafanya akiwa amelala
kitandani na anasaidiwa na wauguzi... tumeshamzoea na ametuzoea na sasa
tunaishi naye kama ndugu,” alisema.
Alisema kuwa tangu aanze kumwona mzee huyo
hospitalini hapo, hakuwahi kuwaona ndugu wala rafiki wanaokuja
kumtembelea au kumjulia hali.
“Kutokana na hali hiyo na kukaa naye kwa miaka 43
sasa, kila mmoja anamwona ni ndugu, sasa utamfanya nini na yuko
hapa...tunaishi naye, tunampatia misaada midogomidogo ya kumwezesha
kupata mlo, kinachopatikana tunampatia na tunaendelea kumsaidia,
hatutachoka,” alisema.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment