Home » » MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KUMWAGA NEEMA SINGIDA KWA KUJENGA NYUMBA 200 ZA KUKOPESHA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KUMWAGA NEEMA SINGIDA KWA KUJENGA NYUMBA 200 ZA KUKOPESHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC08020
Mkuu wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF)  mkoa wa Singida, Bw. Saidi Majimoto, akihamasisha wanafunzi wa ualimu kujinga na mfuko wa PSPF ili kujihakikishia kupata mafao ya kukidhi mahitaji.Kushoto ni afisa wa PSPF, Andrew Mtima.
DSC08012
Baadhi ya wanafunzi wa ualimu chuo cha Lake Hill mjini Singida,wakimsikiliza mkuu wa mfuko wa pensheni kwa watumisi wa umma (PSPF), Saidi Majimoto (hayupo kwenye picha)akiwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili kufaidika na mafao lukuki.
DSC08013
Bango la PSPF.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MFUKO wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) unakusudia kujenga nyumba 200 za gharama nafuu mkoani Singida kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake.
 Mkuu wa PSPF mkoani Singida, Said Majimoto alieleza hayo hivi karibuni wakati akitambulisha Mfuko huo kwa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Lake mjini hapa.
 Majimoto amesema kuwa mfuko huo umechukua hatua hiyo ili kuwawezesha wanachama wake kuishi mahali pazuri pasipo na usumbufu na kwa kwa bei nafuu kabisa.
Amesema kuwa kwa hivi sasa michoro ya viwanja hivyo, ambavyo vipo eneo la Mandewa iko tayari na kwamba ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kuanza wakati wowote.
 Majimoto alifafanua kuwa PSPF hutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama waliochangia miaka mitano na kuendelea ambapo hulipa kidogo kidogo kupitia mishahara yao kwa muda wa miaka hadi 25. “Mwanachama huanza kuishi katika nyumba yake mara tu anapoanza makato ya mkopo husika” amesema.
Aidha, alidokeza kuwa PSPF hutoa mikopo ya fedha  kwa kiwango cha hadi nusu ya mafao ya mwanachama aliyebakiza miaka mitano kustaafu, kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ununuzi wa nyumba mahali popote anapoamua mwanachama huyo.
 Mhasibu wa mfuko huo kutoka Makao Makuu, Andrew Msina amesema kuwa hadi sasa mfuko huo una wanachama 400,000, kati ya idadi hiyo asilimia 97 ya walimu walio kwenye ajira ni wanachama. Alisema kuwa wingi huo wa wanachama unatokana na ukweli kwamba PSPF ina aina ya kikokotoo bora zaidi kuliko mfuko mwingine wowote wa jamii nchini.
Msina pia amesema kuwa hadi Juni 2013 PSPF ilikuwa imelipa mafao ya sh. bilioni 543.7 kwa wastaafu mbalimbali nchini huku Mfuko huo ukiwa unajivunia thamani ya mafao ya sh. trilioni 1.25 kibindoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa