Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Juma 
Juma (52), amefariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye nyumba ya 
kulala wageni akiwa na mwanamke ambaye imedaiwa ni mhudumu wa baa.
                
              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela
 alisema tukio hilo lilitokea  Mei 3, saa 4:00 usiku chumba kwenye Na. 
S.2 cha nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New 
mjini Kiomboi.
Alisema saa 6:00 usiku siku ya tukio hilo, dereva 
huyo alimuaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hangechelewa 
kurudi nyumbani kwa hiyo asifunge mlango wa mbele ya nyumba.
Alisema kuwa saa mbili baadaye, dereva huyo 
alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni ambayo 
iko mita 50 kutoka nyumbani kwake.
“Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa 
wahudumu wa baa hiyo aitwaye Agness Mayo (32) anayesadikiwa kuwa na 
uhusiano naye wa kimapenzi,” alisema.
Kamwela alisema mhudumu huyo wa baa alitoweka Mei 
4, mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea 
kusikojulika.
Hata hivyo, ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wenzake.
Kamanda huyo alisema kuwa tangu siku Mei 3, chumba
 alicholala Juma hakikufunguliwa hadi Mei 5 mwaka huu wakati mwili wa 
dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika.
“Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni
 pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa 
mahakamani endapo atabainika kuhusika na tukio,” alisema kamanda 
Kamwela.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment