Mzee
Abdi Nkhambi Lanjui (75) akiwa wodi namba nne katika hospitali ya mkoa
mjini Singida. Mzee Lanjui mzaliwa wa kijiji cha Mhintiri tarafa ya
Ihanja, aliyekuwa dereva wa kampuni ya mamlaka ya Pamba Mwanza, alipata
ajali katikati ya mwaka 1968 na kulazwa katika hospitali ya Sekoture
Mwanza na baadaye mwishoni mwa mwaka 1970,alihamishiwa hospitali ya mkoa
wa Singida, ambako anaishi hadi sasa. Ajali hiyo ilisababisha kukatika
mawasiliano kati ya kuanzia kiunoni na kushuka chini ambako kumepooza na
sasa kuna vidonda na sehemu ya mwili juu ya kiuno, bado inafanya
kazi.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MZEE
Abdi Nkhambi Lanjui (75) ambaye ameishi wodini kwa miaka 45 sasa
ameiomba serikali,Asasi na jamii kwa ujumla kumsaidia huduma ya chakula
kwa madai kwamba hana ndugu wa kumsaidia huduma hiyo.
Akizungumza
na MOblog hivi karibuni, Mzee Abdi ambaye kwa sasa hawezi kabisa
kunyanyuka kitandani amesema kuwa kwa miaka mingi uongozi wa hospitali
ya mkoa umemhudumia vizuri chakula cha kutosha.
Akifafanua
amesema baada ya hospitali hiyo kusitisha huduma ya chakula kwa
wagonjwa amekuwa omba omba na maisha yake yamebaki ya mlo moja kwa siku.
“Kwa
vile siwezi kunyanyuka kitandani na sina ndugu ye yote nimekuwa
nikiwaomba msaada manesi na watumishi wengine wa hospitani hapa na
nashukuru sana hawaniangushi wamekuwa wakinisaidia bila kuchoka na
wananiwezesha kupata angalau mlo wa siku moja”,amesema.
Mzee
Abdi pia ametumia fursa hiyo kuomba msaada wa fedha na msindikizaji kwa
ajili ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi mkoa wa Kilimanjaro ili
akapatiwe huduma ya matibabu.
“Sababu
ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni kutokana na ajali
iliyosababisha kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo za miguuni,kupooza Kwa
sababu hivi sasa sinyanyuki kitandani kumepelekea nipate vidoda kuanzia
makalioni hadi kwenye miguu kwa ujumla kwa sasa naishi maisha magumu
mno”amesema Mzee Abdi.
Mzee Abdi amelazwa wodi namba nne katika hospitali ya mkoa mjini hapa toka januari mosi mwaka 1971.
Awali
alilazwa katika hospitali ya Sekoture ya jijini Mwanza kuanzia mwaka
1969 baada ya kupata ajali ya lori alilokuwa akiliendesha kupasuka tairi
la mbele.
Amesema
akiwa hospitali ya Sekoture mwishoni mwa mwaka 1970 hali yake
ilibadilika na kuwa mbaya na ndipo alipomwomba mwajiri wake mamlaka ya
pamba imrudishe nyumbani katika kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja
wilaya ya Ikungi ili akasubiri kifo chake.
Hata
hivyo,amesema uongozi wa mamlaka ya pamba ulikataa kumpeleka kijijini
kwao na badala yake walimkabidhi katika hospitali ya mkoa wa Singida
mapema mwaka 1971.
Mzee
Abdi amesema aliondoka nyumbani kwao Mhintiri mwaka 1962 na kwenda
Mwanza mjini kusaka maisha bora alijifunza udereva na kisha kufanikiwa
kuajiriwa na mamalaka ya pamba mwaka 1968.Wakati akiondoka kwao
alimwacha baba,mama na kaka yake mkubwa.
Toka
alazwe hospitalini,wazazi wake na ndugu yake pekee walikuwa tayari
wamefariki dunia kwao walizaliwa watoto wawili tu wa kiume.
0 comments:
Post a Comment