MKAZI 
wa Kitongoji cha Mrama Kijiji cha Musimi Kata ya Sepuka, Wilaya ya 
Ikungi mkoani Singida, Joseph Benjamin (61), amemuua mwanaye, Joramu 
Joseph (36) kwa kumpiga kisu shingoni, usiku akiwa nyumbani kwake wakati
 wakiwa wamelewa pombe. 
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Singida, 
Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Thobius Sedoyeka alisema, tukio hilo 
lilitokea mwishoni mwa wiki, saa 1:00 usiku katika Kijiji cha Musimi. 
Aidha,
 Kamanda Sedoyeka alisema baba mzazi Joseph Benjamin akiwa nyumbani 
kwake usiku alimchoma kisu shingoni na begani upande wa kushoto hadi 
kufa. 
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa, chanzo 
cha tukio hilo ni ulevi wa pombe na kutokana na ulevi huo marehemu 
alimtukana baba yake matusi makubwa ya nguoni kitendo ambacho 
kilimchukiza na kusababisha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kumchoma
 kisu shingoni kwa hasira. 
"Baada ya mauaji hayo kufanyika mtuhumiwa
 Joseph Benjamin alijisalimisha mwenyewe katika kituo kidogo cha Polisi 
cha Sepuka na baadaye akapelekwa kituo kikubwa cha polisi Ikungi," 
alisema. 
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawaasa wananchi 
kupunguza ulevi ambao umekuwa ni chanzo cha vitendo vya kikatili na 
upotevu wa amani katika maeneo yetu na nchi kwa ujumla.
Chanzo:Majira 
 
0 comments:
Post a Comment