Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
Familia ya
marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura
pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na
Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa
upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika
kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo
(pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi,
kwa ajali ya gari.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amezindua huduma tembezi
za madaktari bingwa humo na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi
kupata huduma hizo za kibingwa.
Huduma
zilizozinduliwa Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi zitahusisha
huduma za za upasuaji, meno, macho, upasuaji wa mifupa, huduma za
kibingwa za magonjwa ya watoto, wanawake na huduma za mionzi.
Mhandisi
Mtigumwe amesema matarajio ya mkoa huo ni kuwa huduma tembezi za
kibingwa zitasaidia kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali kabla
hayajafikia hatua ya usugu na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa
kwenda nje ya mkoa.
“Huduma
tembezi za kibingwa zitawasaidia wananchi kutambua uwepo wa huduma za
kibingwa katika mkoa wa singida na kupata matibabu kwa gharama nafuu”
alisema Mhandisi Mtigumwe.
Naye
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya
Mkoa wa Singida amesema wazo la kuanzisha huduma tembezi za kibingwa
limetokana na idadi kubwa ya operesheni zilizofanyika kwa mwaka
2015/2016 na pia mkutano wa wadau wa afya mkoani hapa kuafiki wazo la
kuanzisha huduma hiyo.
"Kwa
kipindi cha mwaka 2015/2016 jumla ya operesheni kubwa na ndogo 4,836
zimefanyika katika hospitali mbalimbali mkoani hapa, aidha Idara ya
macho katika hospitali ya Mkoa imefanya jumla ya operesheni kubwa na
ndogo 2,020" ameongeza Dkt. Mwombeki.
Dkt.
Mwombeki amesema uwepo wa madaktari bingwa 11 mkoani Singida pia
umekuwa chachu ya utekelezaji wa huduma hiyo huku Mkoa ukifanya jitihada
za kuazima madaktari wengine katika mikoa jirani ya Dodoma na Manyara.
Baadhi
ya wagonjwa waliohudhuria katika siku ya kwanza ya zoezi hilo huku
huduma hiyo ikitarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tano wilayani hapo
wameeleza shauku na furaha yao ya kusogezewa huduma za kibingwa katika
halmashauri zao.
"Nilikuwa
naumwa jino ambalo limeota vibaya, niliambiwa nitaweza kufanyiwa
operesheni katika hospitali kubwa kama Muhimbili lakini hawa madaktari
wametusaidia , nimepata huduma haraka na kwa gharama nafuu, nawasihi
wenzangu waje kwa wingi" amesema Bi Neema Josseph Mkazi wa Kijiji cha
Kizaga Wilayani Iramba.
Naye
Mzazi wa mtoto Jonas Masaka amesema huduma za kibingwa zitamsaidia
mtoto wake mwenye matatizo ya macho na hiyo kumpunguzia gharama ya
kumpeleke katika hospitali kubwa kutibu tatizo la macho linalomsababisha
mtoto huyo kushindwa kusoma vizuri.
Huduma
ya tembezi za kibingwa Mkoani Singida zitafanyika katika Wilaya zote
tano za Mkoa nwa Singida na hvyo kupunguza wagonjwa wa rufaa
watakaopelekwa hospitali za Bugando, KCMC na Muhimbili.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na watumishi wa Hospitali ya
Malkia wa Ulimwengu iliyopo Kijiji na Kata ya Puma
Dc Mtaturu akizungumza na viongozi wa ngazi ya juu katika Hospitali Teule ya Wilaya ya ikungi Makiungu mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jengo jipya linalojengwa kwa ajili ya wodi na baadhi ya Ofisi za Hospitali ya Malkia wa ulimwengu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Malkia wa ulimwengu, Na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine
Wanachi Kijijini Mang’onyi wakisikiliza kwa makini
maelezo ya Mkuu wao wa Wilaya
Baadhi ya viongozi wakisikiliza maelezo ya awali katika
ufunguzi wa mkutano huo uliodumukwa zaidi ya masaa matatu
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wanasiasa kutoa matamko ya
kisiasa kwa maslahi yao binafsi huku wakiwa mbali na eneo la wawakilishi wao
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo
ya waendesha pikipiki.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na
kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa akiwashukuru
washiriki wote wa mafunzo hayo
Dc Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa APEC Respicius Timanywa zawadi
ya kuku iliyotolewa na wahitimu wa mafunzo hayo
Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kwa
kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi ya kijamii
imetajwa kuwa njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali
pamoja na maendeleo ya katika jamii husika.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya
demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile
kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho
katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya
ya Ikungi.
Kutovaa helmeti kwagharimu maisha ya wapanda bodaboda Baadhi wapata
ulemavu wa kupoteza kumbukumbu Polisi watangaza kiama kwa wasiovaa
helmeti Na Shadrack Sagati BRUNO Sigala (24) amelazwa katika Taasisi ya
Mifupa ya Muhimbili (MOI) kwa miezi mitatu tangu alipoanguka na bodaboda
mkoani Singida.
Katika ajali hiyo alivunjika mikono yote, mguu moja na alitikisika
ubongo na sasa hana kumbukumbu. Ingawaje huu ni mwaka 2016. Lakini
Sigala kwa kukosa kumbukumbu, anasema ni mwaka 2018.
Hali kadhalika, wakati amelazwa wodini hapo kwa takribani miezi
mitatu hadi sasa, yeye anadai kwamba ana miaka mitano tangu afikishwe
katika wodi hiyo ya wagonjwa wa mivunjiko! Wauguzi wanaomhudumia
wanaeleza kuwa Sigala anasubiri kufanyiwa upasuaji wa mikono na mguu
baada ya kuhamishwa kutoka katika wodi inayoshughulika na majeraha ya
kichwa.
"Alipoanguka na bodaboda aliumia vibaya kichwani, migugu pamoja na
mikono. Alipofikishwa hapa madaktari waliangalia kipaumbele kwanza ni
ubongo, baada ya kupata ahueni katika majeraha yake ya kichwa ndipo
alipohamishiwa katika wodi hii ili aendelee na matibabu ya miguu na
mikono," anasema Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi.
Bruno Sigala ni kielelezo cha waendesha pikipiki maarufu kama
bodaboda ambao wanaanguka na kuumia vibaya kichwani kutokana na kutovaa
kofia ngumu ya kinga yaani helmeti kwa kimombo.
Kijana huyo alikuwa anafanya biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki
na aligongwa na gari katika ajali iliyomfikisha Muhimbili. Katika ajali
hiyo, Sigala aliumia kichwani, akajing’ata ulimi na kuvunjika mikono
yote na mguu mmoja. Akijieleza kwa kubabaisha anakiri kuwa hakuwa amevaa
kofia wakati anaendesha pikipiki.
"Sikuwa najua umuhimu wa kofia hiyo, kwani mafunzo yenyewe ya
kuendesha nilijifunzia tu mitaani, nikaanza biashara ya kubeba abiria."
Kofia ngumu zimetengenezwa kwa lengo la kumlinda mwendesha bodaboda
asiumie kichwa pale apatapo ajali. Baadhi ya kofia hizi zinatengenezwa
zikiwa na sehemu ya kupitishia hewa, kufunika uso usiathirike kwa kioo
maalumu ambacho hata kikivunjika hakileti madhara kwa mvaaji pamoja na
kulinda masikio.
Mwendesha pikipiki yuko hatarini kupoteza maisha pale apatapo ajali
kama hakuvaa kofia ngumu. Tafiti zinaonesha kuwa kofia ngumu hupunguza
hatari ya mwendesha pikipiki kuumia kichwa pale apatapo ajali kwa
asilimia 69 na inapunguza kifo kwa asilimia 42.
Takwimu zilizopo katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ya Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili ambazo zinahusisha miezi sita, Machi 15 hadi Septemba 15,
2011, zinaonesha kwamba wapanda bodaboda wengi wanaojeruhiwa vibaya pale
ajali za pikipiki zinapotokea, ni wale wasiovaa helmeti.
Wengi wao wanajeruhiwa vibaya kichwani. Daktari bingwa wa Magonjwa ya
Mifupa katika Taasisi ya MOI, Dk Bryson Mcharo, anasema katika utafiti
wake wa miezi 6 ukihusisha majeruhi wapatao 722, amebaini kuwa nusu ya
majeruhi hao walipanda pikipiki bila kuvaa helmeti.
"Katika utafiti huo nilibaini kuwa madereva pikipiki ambao wanaona
umuhimu wa helmeti ni wale ambao angalau wamepitia mafunzo ya udereva na
wana leseni, lakini wengi wa majeruhi ambao hawakuvaa kofia hawana
leseni na pia hawana mafunzo ya kuendesha pikipiki,” anaeleza Dk Mcharo.
"Karibia nusu ya majeruhi hao, asilimia 46, waliumia kichwani jambo
linaloonesha kwamba madereva wengi na abiria wao hawazingatii uvaaji wa
helmeti," anasema Dk Mcharo.
anasema kati ya majeruhi hao madereva wa pikipiki ndio wengi na zaidi ya nusu, asilimia 51.8, hawakuvaa helmeti.
Kwa mujibu wa Dk Mcharo, nusu ya majeruhi hao, walipata ajali baada
ya kugongana au kugongwa na magari na asilimia 7 waligongana kati ya
pikipiki na pikipiki huku asilimia 27 ni majeruhi waligongwa na
pikipiki.
Mkuu wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk
Juma Mfinanga, anasema mwaka 2015 walipokea majeruhi 8,400 waliotokana
na ajali za barabarani kiwango ambacho ni asilimia 61 ya majeruhi wote
wa ajali waliofikishwa katika kitengo hicho.
Dk Juma anafafanua kuwa kati ya majeruhi hao asilimia 71 walikuwa ni
madereva, asilimia 46 walikuwa ni abiria wakati asilimia 39 walikuwa ni
waenda kwa miguu. Anasema kwa mwaka huu kuanzia Januari hadi Julai
pekee, majeruhi wa pikipiki waliofikishwa kwenye kitengo hicho ni 4,900
kiwango ambacho ni sawa na asilimia 64 ya majeruhi wote wa ajali za
barabarani.
Anasema nusu ya ajali hizo (asilimia 51) ni majeruhi waliotokana na
ajali za pikipiki, huku idadi ya wanaume ni mara tatu ya wanawake ya
majeruhi wote waliofikishwa hospitalini hapo.
Dk Juma anasema majeruhi walioumia kichwani walikuwa ni asilimia 42
na kati ya hao asilimia 8 hadi 10 ni wagonjwa waliojeruhiwa vibaya na
kupona kwao ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu, huku asilimia 85 hadi 88 ni
wale ambao wameumia kwa kiwango cha kati na asilimia 61 ya majeruhi hao
walivunjika mifupa mirefu ambayo ni mikono na miguu.
Majeruhi waliohamishiwa katika taasisi ya mifupa ni asilimia 89.1 ya
majeruhi wa pikipiki waliopokelewa kituoni hapo mwaka 2015. Kuhusu
gharama, Dk Juma anasema gharama zinatofautiana kulingana na hali ya
mgonjwa, lakini akasema kwa wastani hospitali inatumia zaidi ya Sh
650,000 kwa mgonjwa mmoja anayefikishwa katika kitengo cha tiba ya
dharura kwa ajili ya kumtibia wakati wa dharura.
Uvaaji wa helmeti kwa dereva na abiria wa pikipiki ni moja ya
masharti yaliyowekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na
Majini (SUMATRA) wakati wa kutoa leseni kwa dereva wa pikipiki.
"Lazima awe na helmeti na abiria wake pia atatakiwa kuvaa kofia ya
kujikinga wakati wote na kwamba kofia hiyo inatakiwa kuwa na alama ya
eneo la utoaji huduma ya usafiri," inasema kanuni ya usafirishaji ya
pikipiki za magurudumu mawili na matatu ya mwaka 2010.
Kanuni hiyo inatoa masharti kwamba dereva wa pikipiki ya magurudumu
matatu kwamba haruhusiwi kubeba idadi ya abiria zaidi ya mmoja, dereva
wa pikipiki anatakiwa kuvaa kofia ngumu ya kujikinga wakati wote yeye na
abiria wake.
Lakini jambo hilo halifanyiki. Pikipiki nyingi zinazobeba abiria
zinatisha, unaweza kukuta dereva na abiria wake hawajavaa helmeti, au
dereva anayo lakini abiria hana. Wakati mwingine unaweza kukuta dereva
kavaa na abiria kaishikilia mkononi au kuipakata.
Hili limechangia dereva na abiria kupoteza maisha pindi inapotokea ajali.
Hili ndilo limemfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
kutahadharisha kwamba kupanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu ni dhamira
ya kujiua, kwa sababu dereva na abiria wakipata ajali ni rahisi
kupoteza maisha kwa kupigiza kichwa chini.
Makonda anawataka madereva wa bodaboda na abiria wao kuvaa helmeti.
“Nimeshawasiliana na kamati yangu ya usalama barabarani mkoa. Hili
nitalisimamia kikamilifu lazima wote wawe na helmeti,” anasema Makonda.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, Johansen
Kahatano, anasema sheria ya Sumatra ya pikipiki inamtaka dereva wake
avae helmeti wakati wote, kushindwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria kwa
makusudi. Kuhusu madai ya abiria kutopenda kuvaa hizo kofia, Kahatano
anasema kwamba amekuwa anawashauri waendesha pikipiki wasipakie abiria
ambao hawataki kuvaaa kofia ngumu.
"Usimamizi ni mgumu. Lakini tunaendelea kutoa elimu kwamba abiria
akipanda pikipiki aone umuhimu wa kuvaa helmeti na kuthamini maisha
yake. Hilo ni jambo la lazima. Sisi kama mamlaka tuna kazi ya kuendelea
kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuvaa kofia ," anasema Kahatano.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, hataki
kumung’unya. Uvaaji wa kofia ngumu helmeti kwa waendesha pikipiki na
abiria wao ni lazima. Yule ambaye atakaidi agizo hilo atakamatwa na
kuchukuliwa hatua za kisheria. Itaendelea kesho. Inserts "Karibia nusu
ya majeruhi hao, asilimia 46, waliumia kichwani jambo linaloonesha
kwamba madereva wengi na abiria wao hawazingatii uvaaji wa helmeti"
“Majeruhi walioumia kichwani walikuwa ni asilimia 42 na kati ya hao
asilimia 8 hadi 10 ni wagonjwa waliojeruhiwa vibaya na kupona kwao ni
kwa kudra za Mwenyezi Mungu.” “Kupanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu
ni dhamira ya kujiua, kwa sababu dereva na abiria wakipata ajali ni
rahisi kupoteza maisha kwa kupigiza kichwa chini.”
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ofisini mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa
kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii
yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya
wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu
Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel amesema kuwa
mfuko huo uangalie namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili
waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni
jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF
ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa
wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma
kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya
Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF
Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha
maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana
na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua wasanii hao kupitia
mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake
limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu
ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa
kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi
yetu vizuri sana kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni
ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa
wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia
katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kikazi wilaya ya Manyoni jana
Waziri Nchemba akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia)
Waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali kuingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni
Mbunge Lazaro Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida
Waziri Nchemba akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku manyoni
Wakulima wa Tumbaku wakisalimiana na waziri Nchemba
Baadhi ya madiwani wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea waziri Mwigulu Nchemba
Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wakiwa ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba
Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu akitambulisha viongozi mbali mbali kabla ya mkutano wa wakulima wa Tumbaku kuanza
Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizungumza na wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana
Diwani wa kata ya Mitundu wilaya ya Manyoni Bw Andrea Madole akimkabidhi nyalaka mbali mbali za uthibitisho wa michango kandamizi wanayobambikizwa wakulima wa Tumbaku na Kitengo cha AMIS waziri wa kilimo ,mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae alitangaza kufuta michango hiyo
Wakulima wa Tumbaku wakitoa kero zao kwa waziri Nchemba (hayupo pichani)
Wabunge wakisikiliza kero za wakulima wa Tumbaku
waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu wakati akieleza kilio cha wakulima wa Tumbaku wilaya ya Manyoni wakati wa mkutano wa waziri Nchemba na wakulima wa Tumbaku uliofanyika ukumbi wa CCM Manyoni jana
WAZIRI wakilimo
,mifugo nauvuviBw MwiguluNchemba amefuta michango hewa
iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku kwaUNION kwakupitiakitengocha AMIS huku akiagiza serikaliyawilaya ya Manyonikuwachukulia hatuakali aofisaushirika mkoaAndru Msafiri na
afisaushirika Wilayahiyo Bw Alfred Sekiete iwapo
watabainikakuhusikadeni la bilioni 7ambalo wanadaiwa benki wakulimawa
tumbaku.
Waziri Nchembaalilazimika kutoa maagizohayobaadayawakulimawa zao hilo la
Tumbakukulalamikia utaratibu mbaya wa
baadhi yaviongozi wa UNION na APEX
pamoja na baadhi ya maofisaushirikakujinufaishakupitia mgongowawakulima hao.
Akitoa agizohilojana mjini Manyoni wakati wamkutanowapamoja kati yake nawakulima waTumbaku na viongozimbali
mbaliwa Serikaliyawilaya ya Manyoni na wabungewanaotokawilaya ya Maeneo yanayolimwa Tumbaku mkoani
Singida.
Waziri Nchembaalisemakuwabaadhiya mamboambayo serikaliya Rais Dr John Magufulihaipendikuona nipamoja nawakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo
kimsingi haiwasaidii kupiga hatua kimaendeleozaidi yakuwatesa .
“ Mamboya ajabusanahiki kitukinaitwa AMIS ni
kuwatozawakulima michango ya ajabu
ajabuetiwakulimakutozwadola 1200 kwaajiliya kusafirisha Tumbaku tokaDar
es Salaam kwenda UNIONpiawanachangia dola 10 kwakutunzakumbukumbu zao,dola 3 kupakia nakushusha mara mchango kwa ajili ya ADMINmambo ya ajabu kabisa wakulima
wanahusikavipi na malipo maadmin yani
wanatumia lughazakijanja kijanja kuwaibiawakulima ADMIN wa makundi kama yale ya Whatsap kwa wakulimatena…sasa kuanzia leo natangazakufuta michangohii isiyo na maelezo ya kutosha na
kuagizakujipanga upya kwakuwashirikishawakulima na taarifahiyo ndani ya siku 7 niipate “
Waziri chembaalisemakuwa kabla yakuanzakuwatozawakulima hao michango
nivizurimakubaliano yamichangohiyo yafanyikeupya kwa
kuwashirikishawakulima na sio
kuendeleakutumia taratibuzazamani ambazo ni mzigo kwamkulima.
Kuhusu maafisaushirikikudaiwakukopabenkikupitia mgongo wawakulimawatumbaku nakupelekeawakulima haokudaiwadenibenki
la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wawilaya ya Manyoni kuagiza wakaguzina wataalam wakekufanyauchunguzina iwapo itabainikakuwa maofisahaowalihusika na denihilohatuastahikikuchukuliwa dhidi
Alisemanikosakwa maofisaushirikakukopakwaudhaminiwawakulimawakatiwao siwazalishaji wa mazao hayo yakilimo na kuwa maeneomengi
wakulimawalikuwa wakiwalipia madeni
benki maofisahao ambao huombamikopo kupitia vyamavya msingi vyawakulima na wakati mwingine hushirikiana na
benki kutoa mkopo mkubwa ilinao waweze
kugawana .
Pia aliagizaUNIONkufanya kazi yakuwasaidiawakulima na siokuwakandamizawakulima nakuwa maeneomengi nchini ambayoUNION wapo
kumekuwa na migogoro na kero nyingi kwawakulima na kuwa mazao ambayo wakulima hawana UNION kama Mahindi ,
mpunga na alizeti wakulima wanafanyashughulizao pasipo migogorohivyo kuzitaka UNION zinazojihusisha nawakulima wa Tumbaku , Korosho ,pamba na mazao
menginekujitathiminivinginevyo hazina maana kuwepo.
Aidhawaziri Nchembaaliagiza benki ya CRDB kuwalipa pesazaozote wakulimawa Tumbaku ambao
wamemaliza madeni yao yapembejeona kuendeleakuwadai wanaodaiwa na si vinginevyo .
Mbungewa Singida Kaskazini Lazaro
Nyalandualisema kuwakiliokikubwachawakulima wa Tumbaku Manyoni ni uwepowa mtu kati katika kilimohicho
hivyokuwatesawakulima hao nakuwaUNIONna APEXbado si ukombozi kwawakulima wazao la Tumbaku kwanialisemawakulima wamekuwa wakilipwa asilimia 50 ya
mauzo ya mazao yao na benki ya CRDBna
asilimia 50 nyinginekushikiliwa na
benki kwa mkopo wa vyamavyaovya msingi hata kama mkulimahusika hadaiwi.