21 WAJERUHIWA WAKITOKA HARUSINI

MTU mmoja amekufa na wengine 21 kujeruhiwa, baada ya basi dogo aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kutoka Shinyanga kwenye harusi, kurejea nyumbani kwao Morogoro kupinduka katika kijiji cha Ikugha wilayani Ikungi kwenye barabara kuu ya Singida - Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi akizungumza kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, walikolazwa majeruhi, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 8.00 mchana. Alisema kuwa ajali ilitokea baada ya Coaster hiyo, kuhamia upande wa kulia wa barabara, kukwepa uharibifu uliotokana na kungâ™oka mkanda wa chuma kwenye eneo hilo la daraja, hivyo kusababisha kugongwa kwa nyuma na basi la Zuberi lililokuwa likipita kwa kasi. Jina la dereva wa basi hilo la Zuberi, lenye namba za usajili T 983 ABU, lililosababisha Coaster...

MH. NYALANDU ATANGAZA RASMI NIA YA KUWANIA URAIS 2015

Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani. Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania. Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai. Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia...

CHADEMA YAKOMBA 350 KWA NYALANDU

   CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimefanya mkutano mkubwa na kujipatia wanachama wengi mahali panapodaiwa kuwa ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida Kaskazini, jimbo linaloongozwa na Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu. Katika mkutano huo uliofanyika juzi katika Kijiji cha Msange na kuhutubiwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu, ambapo zaidi ya wanachama 350 walikabidhiwa kadi pamoja na kuapishwa kiapo cha uzalendo kwa ajili ya kuwajengea ujasiri. Mwalimu aliwaambia wanachama hao kuwa kiapo hicho cha cha kuwajengea ujasiri, ni kwa ajili ya kujiunga na kundi la watanzania...

WANAFUNZI WASOMEA SEBULENI KWA MWALIMU

 WANAFUNZI 173 wanaosoma darasa la awali katika Shule ya Msingi Minga, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wanasomea kwenye sebule ya nyumba ya mwalimu kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa unaoikabili shule hiyo. Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Gregory Manimo, alibainisha hayo kwenye mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi 162 wa shule ya msingi Minga. Alisema kwa sasa shule hiyo ina vyumba 10 vya madarasa wakati mahitaji ya vyumba ni 38, huku kukiwa na vyumba viwili vya madarasa vilivyofikia hatua ya kupauliwa, nyumba mbili za walimu, ofisi moja ya mwalimu mkuu na ofisi mbili za walimu. “Shule ina madawati 188, meza 12, viti 27, nyumba mbili za walimu huku kukiwa na nyumba moja iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2006. Nyumba hii...

MBUNGE ASIHI WAKAZI WA SINGIDA KUIPIGIA KURA CCM

MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amewasihi wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini ili kukiwezesha kutekeleza Ilani yake kwa urahisi zaidi. Mbunge huyo alitoa mwito huo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la soko la zamani la Kibaoni mjini hapa. Alisema chaguzi za Serikali za Mitaa ni jiwe la msingi la nyumba inayojengwa na serikali yoyote ile, hivyo ili kuiwezesha nyumba hiyo kuwa imara wakazi wote wa Jimbo la Singida Mjini hasa wana- CCM, hawana budi kuipigia CCM kura nyingi ili kuiimarisha kisiasa. Alisema kuwa kwa vile tayari Mbunge wa jimbo hilo ni wa CCM, ingekuwa vizuri zaidi iwapo wananchi wataendelea kukiamini na...

WENYE MAAMBUKIZI YA VVU WAJIUNGA KWENYE VITUO

ZAIDI ya asilimia 69 ya watu waliobainika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani Singida wamejiunga kwenye vituo vya tiba na matunzo (CTC) na kuanza kupewa dawa za kupunguza makali ya VVU katika kipindi cha miaka tisa iliyopita. Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mkoa wa Singida, Edson Mdala alisema hayo juzi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Musimi kata ya Sepuka wilayani Ikungi. Mdala alisema kuwa tangu 2005 hadi kufikia Juni mwaka huu, jumla ya watu waliopimwa VVU na kujiandikisha CTC ni 17,720, kati yao 12,286 wanapata dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV). Kadhalika, alisema kuwa vituo vya kutolea huduma ya dawa vimeongezeka kutoka vitatu mwaka 2005 hadi kufikia 30, mwaka huu. Aidha,...

MO AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM SINGIDA‏

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Gulam Dewji akisalimiana na wapiga kura kura wake na wananchi wa jimbo la Singida mjini mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kibaoni tayari kuzindua kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Singida Mjini.(Picha na Geofrey Mwakibete wa MOblog). Mbunge wa Singida MO Dewji akipata mapokezi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika Kibaoni mjini Singida. Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Dewji akimnadi mgombe wa nafasi ya m/kiti wa mtaaa Kibaoni Timotheo Ruben John kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la...

SOMA HAPA-NANI ANACHEZESHA NGOMA YA ESCROW NA IPTL?

Kwa muda sasa kumekuwapo na tuhuma zinazohusu "wizi" wa fedha za akaunti ya escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2006. Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha zilizokuwa zikilipwa na Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL. Chimbuko la akaunti hiyo ni mgogoro wa tozo hiyo kwamba iligubikwa na utata baada ya kudaiwa kwamba Tanesco ilikuwa ikitozwa fedha nyingi kuliko inavyostahili.             Tuhuma za huo "wizi" hata hivyo hazikuishia tu kwa wahusika wakuu yaani makampuni ya umeme, bali zimetiririshwa hadi kwa watu binafsi ambao kimsingi hawana uhusiano wowote na mgogoro huo wa malipo na wala kuhusika kwa njia yoyote na hicho kinachodaiwa kwamba ni uporaji wa fedha za...

NYALANDU AMTEUA RC SINGIDA MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI ALICHOUUNDA JANA.

Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amemteua Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Paseko Kone kuwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi kitachofuatilia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki hapa nchini. Nyalandu alimteua Mkuu wa Mkoa huo kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wafugaji wa nyuki katika mkoa wake wa Singida bila kuchoka. Waziri Nyalandu alitoa uamuzi huo wakati akifuga kongamano la ufugaji nyuki la Afrika lililomalizika Jijini Arusha jana. Wajumbe Wengine walioteuliwa katika kikosi kazi hicho ni Juma Shaban Mgoo ambaye atakuwa katibu wa Kikosi kazi hicho na pia ni  Mtendaji Mkuu,wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na ambaye...

DC Igunga ajivunia mapato ya CHF, NHIF

Waziri wa afya na ustawi wa jamii,Dk.Seif Rashidi akifungua kongamano la tisa la baadhi ya waandishi wa habari lililoandaliwa na kufadhiliwa na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma hotel mjini Dodoma.Dk.Rashidi aliwataka wanahabari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko ya afya,ili waweze kuwa na uhakika wakati wote hata kama hawana fedha. Na Nathaniel Limu, Dodoma HALMASHAURI ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imekusanya zaidi ya shilingi 1.2 bilioni kutoka michango ya wanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) na vyanzo vingine vya huduma ya afya, kati ya mwaka 1996 na sasa. Fedha...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa