Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipozi kwa picha na Mwenyekiti wa
Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba kushoto na Mama Sara Philipo
mwenye nyumba hiyo wakati alipozungumza na chifu huyo leo, Katika ziara
hiyo Kinana katika kijiji cha Kibampa na kukagua miradi mbalimbali ya
jamii hiyo ya Kihadzabe ikiwemo maji, mabweni ya watoto wa jamii hiyo
pamoja na zahanati iliyopo katika kijiji cha Munguli kata ya Mwangeza
wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone amewajengea mabweni na
kuwawekea mradi wa maji, Umeme na kuwafundisha kilimo cha mihogo na
mazao mengine ili kuweza kujikimu kwa chakula kwani jamii ya kabila hilo
inakula nyama, mizizi ya miti na asali.
Lakini
pia vijana hamsini wa Kabila hilo wamejiunga na jeshi la wananchi kwa
mpango mkuu wa mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone na serikali kwa
kuwaendeleza kielimu na kimaendeleo, kuna vijana wengine sitini
wataingizwa jeshini ikiwa ni mkakati wa kuielimisha jamii hiyo ili
kubadili maisha bila kuharibu mila yao.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-MKALAMA -SINGIDA)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa
Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba wakati alipotembelea na
kujadiliana naye mawili matatu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mama Sara Philipo mwenye nyumba
hiyo wakitoka nje mara baada ya Kinana kuzungumza na Chifu Edward
Mashimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi hao wa jamii
ya Wahadzabe huku Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward
Mashimba akitafsiri katika kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza.
Baadhi
ya wananchi wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Ndugu Abdulrahman
Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akiwahutubia.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kupanda
mbegu ya muhogo na vijana wa Kihadzabe katika shamba darasa ililopo
kijiji cha Kibampa kata ya Mwangezi ikiwa ni mafunzo ya kilimo kwa jamii
hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya jamii hiyo wakati alipokuwa akiwasili kijiji cha Kibampa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ya asili ya jamii ya Kihadzabe.
Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na
mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako
jamii hiyo inaishi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaklimiana na vijana wa
kisukuma aliowakuta wakipalilia shamba, vijana hao walimweleza Kinana
kuwa wanahitaji serikali iwatengenezee barabara yao jambo ambalo
litarahisha hata uuzaji wa mazao yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji katika
kijiji cha Munguli ambao umejengwa maalum kwa ajili ya jamii hiyo
anayetoa maelekezo ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher
Ngubiagai.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mabweni ya watoto wa
jamii ya Kihadzabe yaliyojengwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko
Kone katika kijiji cha Munguli mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 60 wa kiume 30 na wakiume 30 yamejengwa maalum kwa ajili ya
jamii kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
Baadhi ya wananfunzi wa shule hiyo
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo ya Munguli Athman Kinyere akisoma taarifa ya shule
hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Hii ni moja ya nyumba zinazotumiwa na jamii hiyo ya Kihadzabe.
Baadhi ya wananchi wa jamii hiyo wakiwa katika mkutano
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mtambo wa Sola
unaoendesha maji katika mradi wa maji wa kijiji cha Munguli ambao
umejengwa maalum kwa ajili ya jamii hiyo anayetoa
0 comments:
Post a Comment