Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jererali, Ernest Mangu, 
kufuatia vifo vya askari watatu waliopoteza maisha katika ajali ya gari 
iliyotokea juzi katika kijiji cha Isuna, wilayani Ikungi mkoani Singida.
Askari waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Inspekta Miraji Mwegelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerald Mtondo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na 
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, Rais amesikitishwa
 na vifo vya askari hao, ambao wamekutwa na mauti wakiwa wanatekeleza 
majukumu yao ya kazi.
“Kupitia kwako Mkuu wa Jeshi la Polisi, natoa pole nyingi kwa 
familia za askari waliopoteza maisha, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na
 askari wote wa jeshi hilo ambao wameguswa kwa namna ya pekee na msiba 
huu,” ilieleza taarifa hiyo.
Rais Magufuli pia amewatumia salamu za pole askari walioumia katika
 ajali hiyo, akiwamo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarabi Mkoa wa 
Singida, Mratibu wa Polisi, Peter Magira na kuwaombea wapone haraka ili 
waendelee na majukumu yao ya kila siku.
     CHANZO: GAZETI LA NIPASHE
    
0 comments:
Post a Comment