Huduma ya Tigo 4G LTE yazinduliwa Singida, sasa ipo miji 23 nchini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Tigo, Aidan Komba, akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mkoani Singida, kushoto ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Singida Raymond Royer.
Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma ya 4G LTE mkoani singida mapema leo.



Singida, Mei 22, 2017-Wateja wa Tigo mkoani Singida hivi sasa wanaweza kufurahia  kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika soko.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo unafuatia  mafanikio yaliyopatikana  baada ya kuizindua katika mji mingine mikubwa nchini.
Komba alisema  kwa kuifanya  huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo  kwa mara nyingine tena imeonesha  kujikita kwake katika kuboresha  mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa  na ubunifu katika soko hili.”
Alitangaza kuanza kwa enzi mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano  ndani ya Singida akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha  kunakuwepo uwezo mkubwa na muhimu  katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.
“Singida  ni kituo  muhimu kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia  huduma Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa rahisi zaidi.”
“Mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na hali kadhalika kukuza  uchumi na biashara”, alisema  Komba.
“Kama mnavyojua, Tigo imekuwa mstari wa mbele  katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri ukiwa ni uchimbaji wa visima 12  ambavyo tulivitoa kama msaada  kwa vijiji vya Singida mwaka jana,”  Komba alibainisha.
Aliongeza kwamba gharama ya vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua kuwa wateja wanachotakiwa  ni kuwa na kifaa  kinachowezesha 4G LTE  ama simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja wanaweza kubadilisha au kununua  kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika duka la Tigo la huduma kwa wateja  lililopo Singida Mjini.
Akizungumzia uwekezaji  katika mtandao,  Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya kisasa, ikilenga  kusaidia katika maendeleo endelevu ndani ya mkoa.
Alihitimisha kwa kusema, “Mipango  imo njiani katika kupanua huduma  kwa ajili ya mikoa iliyobakia ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”
Kwa upande wake, Meneja wa mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer  alibainisha umuhimu wa  huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha  huduma za uwanda mpana wa simu za mkononi.
Royer alisema, “Katika kipindi cha hivi karibuni  kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia 90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”
Aliongeza, “Kwa hiyo teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za  data zilizo na kasi kubwa  na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko  ambayo itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”
Mtandao wa 4G LTE  unamaanisha kasi  kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada  kutoka katika intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango kikubwa inaboresha  uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya mikutano. Hali kadhalika  inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na kutiririsha  video kutoka katika mitandao ya kijamii.


Mwisho

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL INAONGOZA KWA KUTOA HUDUMA ZA INTANET BORA NA ZA UHAKIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kwa sasa, juhudi za Rais Dkt. Magufuli kufufua huduma bora na za uhakika katika Mashirika na Makampuni ya Umma zinazidi kuleta *Matokeo chanyA+* Kampuni Simu ya TANZANIA -TTCL ndiyo kampuni pekee inaongoza kwa sasa kwa kutoa huduma za intanet bora na za uhakika. Rais wangu... *mzalendo na mchapakazi..* Nchi yangu... *Matokeo chanyA+*

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowasili wilayani Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Afisa Ustawi wa Jamii Yeremia Ngoo akiwapa maelezo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nyumbani kwa Bibi Agnes Kamota (75) walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea  Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi wakati yeye na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli walipofanya ziara  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki kucheza ngoma na vikundi vilivyojitokeza kuwalaki katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akihutubia wananchi wakati walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na  mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakioneshana kielele cha kilima cha Sukamahela ambapo inasemekana ndipo ilipo alama ya kuonesha katikati ya nchi ya Tanzania wakati wa ziara yao katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida Bw. Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. PICHA NA IKULU

NA MWANDISHI MAALUM
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.
Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.
Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.
Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.
Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.
Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.
Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.

SITAKI TENA KUSIKIA MSAMIATI "MRADI UKO CHINI YA KIWANGO", RC NCHIMBI AAGIZA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika ziara yake wilayani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.

Dkt. Nchimbi amesema msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.

Ameongeza kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.

Dkt. Nchimbi amesema viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.

“Mradi wakati unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango tutahakikisha fedha ya serikali inarudi”, amesema Dkt. Nchimbi.

Aidha katika kikao hicho na watumishi wote wa halmashauri hiyo amewaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuwaruhusu wanafunzi ambao hawana sare kuanza masomo huku utaratibu wa kuwafuatilia wazazi watimize majukumu yao ukiendelea.

“ Baada ya elimu kuanza kutolewa bure, changamoto nyingine iliyobakia kwa baadhi ya wazazi ni uwezo wa kuwashonea watoto wao sare za shule, sasa ninaagiza wakuu wa shule za sekondari na Msingi wote Wilayani hapa kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata kama hawajavaa sare za shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare tu”, ameagiza Dkt. Nchimbi.

Awali kabla ya kuzungumza na watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika mashamba ya wakulima ili kujionea na kushiriki na wananchi shughuli za kilimo hasa mashamba ya viazi katika kijiji cha Nkungi na mashamba ya mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani humo.

Dkt. Nchimbi akiwa katika shamba la mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha Nkungi alipanda viazi na kuhamasisha wananchi wengine walime mazao ambayo yanatumia maji kwa ufanisi kama vile viazi, mihogo, matama na uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini ili kujihakikishia uwepo wa chakula.

Amewataka watendaji hasa wa kada za kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea hasa kuandaa taarifa za makaratasi bali wawatembelee wakulima na wafugaji katika maeneo wanayofanya shughuli zao ili waweze kutoa ushauri kwa kupata picha halisi.“Sipendi kiongozi anayesema yupo karibu na wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo hivyo ni vyema kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”, amesema Dkt. Nchimbi.
 

NAIBU WAZIRI ELIMU MHANDISI MANYANYA AFANYA ZIARA MKOANI SINGIDA NA KUHAMASISHA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI YA WATU WAZIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Eliya Digha.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akimkaribisha Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya ili aweze kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya Singida.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule aliyoitembelea kukagua na kuhamasisha elimu ya watu wazima.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwa amekaa kwenye moja ya darasa lenye wanafunzi walio katika mpango ulio nje ya mfumo rasmi wa elimu ya watu wazima.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua daftari la mwanafunzi wa elimu ya watu wazima.

BILIONI 13.1 KUTUMIKA KUGHARIMIA MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na Nathaniel Limu Singida.
Halmashauri ya manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 13.1 bilioni, kwa ajili ya kugharamia miradi mitatu ya uimarishaji miji (ULGSP) inayogharamia na benki ya dunia.
  
Hayo yamesemwa juzi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyapembile, wakati akizungumzia kwenye hafla ya sherehe ya kusaini mkataba baina ya manispaa, washauri na mkandarasi atakayetekeleza miradi hiyo.
 
Amesema wamefikia hatua hiyo ya kusaini mkataba baada ya taratibu zote za kisheria za manunuzi kukamilika na kuongeza kuwa miradi hiyo ni ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 5.75 kwa kiwango cha lami.
 
 “Barabara hizo ni pamoja na ile inayoanzia kituo cha mafuta Namfua hadi ofisi ya Mamlaka ya mapato (TRA) ambayo itapanuliwa na kuwa mbili (double road). Nyingine ni ile inayoanzia ofisi za TRA hadi makazi ya askofu wa kanisa la katoliki (barabara ya Kinyeto)”, ameongeza.
 
Lyampembile amesema taratibu za manunuzi katika mkataba huu zilianza mwezi Mei mwaka jana na kukamilika Januari mwaka huu ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi ya shilingi 12.4 bilioni.
 
“Leo hii manispaa ya Singida itatiliana saini mkataba namba LGA/115/SMC/2016/2017 /W/NO.1 na kampuni ya China Henan International Co-operation Group Co.LTD (CHICO) ya jijini Dar-es-salaam. Ujenzi huo utakamilika baada ya miezi 12”, alifafanua zaidi.
 
Amesema CHICO atasimamiwa na  kampuni ya Luptan Consultants Ltd ya jijini Dar-es-salaam kwa gharama ya shilingi 648.3 milioni na itakamilika baada ya miezi 15. Mkataba wa mradi huo ni LGA/115/SWMC/2016/2017/C/No.02.
 
“Vile vile tutatekeleza mradi mwingine wa uandaaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa mansipaa yetu ya Singida.Mradi huu wenye mkataba LGA/115/SMC/2016/2017/C/No.03 una   thamani ya zaidi ya shilingi 55.9 milioni.Mradi huu utatekelezwa na mshauri mwelekezi chuo cha mipango Dodoma, Titus Mwageni”,alisema.
 
Sherehe hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo,zilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi.
 
Dk.Nchimbi Alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika ya TANESCO,TTCL na mamlaka ya maji (SUWASA) kutoa ushirikiano na mkandarasi,ili miundo mbinu yao isikwamishe utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utakapokamilika,utabadilisha madhari ya mji wa Singida.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WASHIRIKI IBADA YA KRISMASI KATIKA KANISA KATOLIKI (KANISA KUU LA MOYO MTAKATIFU WA YESU) MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU

RC NCHIMBI ALIPONGEZA SHIRIKA LA NYUMBA; AZUNGUMZA NA WATUMISHI MANYONI NA KUWAKUMBUSHA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA KIKUBWA CHA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mashudu ya alizeti yanayonunuliwa na kampuni ya Mount Meru tawi la Singida na kusangwa upya na kutoa mafuta ya kutosha.

RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
 

Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. 
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).  
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.

Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
  
Na Mathias Canal

Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.

Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.    
KAWAIDA...! RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida) Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016). Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake. Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba. Na Mathias Canal Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe. Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016). Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida. Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa