Mkuu wa mkoa wa Singida aagiza waalimu wakuu wakajifunze matumizi ya fedha kwa mwalimu mkuu mwenzao





Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Mwanzi Manyoni mjini.Dk.Kone hakufurahishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakati shule ikiwa na akiba ya zaidi ya shilingi milioni sita.(Picha na Nathaniel Limu).
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Olivary Kamili akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake. Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone ameagiza walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa sekondari wafike shule ya msingi mchanganyiko Ikungi, ili wakajifunze juu ya matumizi bora ya fedha za Umma.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mkuu wa  mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amemwagiza mkurugenzi mtenadaji wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni, achague walimu wakuu wanne wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari wanne, awapeleke shule ya msingi mchanganyiko Ikungi, ili wakajifunze juu ya matumizi bora ya fedha za umma.
Akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Mwanzi iliyopo mjini Manyoni pamoja na viongozi wa wilaya ya Manyoni Dkt. Kone amesema shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi,ni shule ya mfano mkoani Singida kwa matumizi mazuri ya fedha za uuma.
Amesema Ofisi ya mkuu wa shule hiyo ni nzuri mno, pengine si rahisi kuifananisha na ofisi nyingi za wakuu wa wilaya. Ina samani za kisasa, tv, kompyuta, internet, jokofu na makochi ya hali ya juu na kuwa Ofisi kama ile inavutia na inachangia mhusika kubaki ofisini kipindi chote cha kazi.
Akifafanua zaidi, amesema majengo ya shule ya msingi mchanganyiko Ikungi pamoja na ujenzi wa uzio wa ukuta, yamekarabatiwa/kujengwa yana ubora unaofanana na thamani ya fedha zilizotumika.
Dkt. Kone amesema walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari, hawana budi kufika kwenye shule hiyo ili kujifunza mwenzao Olivary Kamilly (mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi) anavyutumia fedha za umma vizuri.
Mkuu huyo wa mkoa, ametoa agizo hilo, baada ya kutokuridhishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari Mwanzi mjini Manyoni, wakati shule hiyo benki ina zaidi ya shilingi milioni sita ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kutumiwa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kone amewaagiza watendaji wa halmashauri za wilaya na Manispaa, kujenga utamaduni wa kutembelea miradi mara kwa mara, ili miradi yote ya maendeleo iweze kutekelezwa kwa ubora unaofanana na fedha zilizotumika.
Amesema katika ziara yake wilayani Manyoni, amebaini baadhi ya miradi imetekelezwa chini ya kiwango na kitendo hicho kimechangiwa na viongozi kutokwenda vijijini  kutembelea miradi.
“Acheni tabia ya kukaa maofisini, jengeni utamaduni wa kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo, ili iwe na ubora unakusudiwa uweze kufikiwa”alisema Dk.Kone.
Aidha, amewataka kutunza vizuri miradi iliyomalizika na ile inayohitaji ukarabati, ifanyiwe ukarabati unaofanana na thamani ya fedha zitakazotumika.
Chanzo Mo Blog

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji atoa msaada wa baiskeli kwa walemavu



Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na mmoja kati ya walemavu watano aliowakabidhi baiskeli za magurudumu matatu kwa ajili ya kuwasaidia kumudu maisha yao hivi karibuni.Pamoja na msaada wa baiskeli hizo, Dewji pia alitoa msaada wa Wheel Chair 24 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.Thamani ya msaada huo ni zaidi ya shilingi milioni 14.
Na Nathaniel Limu
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa viti 24 maalum vya wagonjwa (wheel chairs) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 24 milioni, kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.
Pamoja na viti hivyo mbunge huyo ametoa msaada wa baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu watano wa jimboni kwake.
Akizungumza kwenye makabidhiano ya msaada huo, Dewji amesema msaada huo ni mwendelezo wa misaada mbalimbali anayoitoa jimboni kwake, kwa ajili ya kusaidiana na serikali kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo za sekta ya afya.
Alisema ana aimani kwamba viti hivyo vitasaidia wagonjwa katika hospitali hiyo hasa wale watakaokuwa hawawezi kutembea.
“Tunaochoomba tu ni kwamba viti hivi vitunzwe vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu”,alisema mbunge huyo.
Awali mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa, Dk.Suleiman Muttani amepongeza mbunge Dewji kwa msaada huo ambao amedai umekuja kwa wakati muafaka.
Dk.Muttani amesema hospitali hiyo inayoendelea kujengwa ina mahitaji mengi na makubwa yakiwemo ya vitendea kazi ambavyo serikali ikiachiwa ifanye peke yake, itachukua muda mrefu kukidhi mahitaji ya hospitali hiyo ambayo itategemewa pia na mikoa jirani.
“Kwa kweli nakushukuru sana mbunge wetu kwa msaada huu wa viti.Tunakuomba usichoke kuisaidia vifaa hii hospitali ya rufaa.Tusaidie pia kuwahamasisha marafiki zako au taasisi mbalimbali ziweze/waweze kutusaidia vitendea kazi kwa kadri ya uwezo wao”,amesema Dk.Muttani.
Kwa mujibu wa Dk.Muttani, hospitali hiyo ya rufaa itakapokamilika itakuwa na majengo 47 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 150 bilioni.
Serikali kila mwaka imekuwa ikitenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi.Kwa utaratibu huo wa kutenga kiasi hicho cha fedha hospitali hiyo itachukua zaidi ya miaka 45 kukamilika kujengwa.
(Picha na Nathaniel Limu).

Mkoa wa Singida wazindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya kudhibiti uhalifu


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na baadhi ya  viongozi wa jeshi polisi mkoa wa Singida muda mfupi kabla ya kuzindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya wakaguzi wa tarafa mkoani Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa pikipki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kushoto ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Mgana Msindai.
 Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Singida wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa pikipiki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akijaribu kuendesha pikipiki za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singid Mgana Msindai akishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya pikipiki 22 za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Pikipiki hizo zimetolewa rasmi kwa ajili ya kukabidhiwa maafisa polisi wa tarafa za mkoa wa Singida.

Basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji


WATU 12 raia wa Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Singida, kulipa faini ya Sh100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya  Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.
Pia mahakama hiyo, imeamuru basi la Kampuni ya Mtei ya mjini Arusha lililokuwa limebeba Waethiopia hao kukamatwa na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.
Waethiopia hao ambao wote bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud, Tazana  Walao, Mohammed Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abdalah na Alamu Gabresekesie.
Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu  Kidisu, Yassin Mohammed Hassan, Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.
Baada ya mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Ahmed Seif kuwasomea makosa hayo mawili ya kuingia na kuishi  nchini bila ya kuwa na kibali, washtakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa hayo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mwanasheria wa Serikali, Seif, aliiomba mahakama hiyo  iwape adhabu kali washtakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali chochote halali.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Kiongozi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na upande wa mashtaka na utetezi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa faini ya Sh100,000 kila mshtakiwa.
Washtakiwa wote 12 walilipa faini hiyo.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali Seif, washtakiwa hao walikamatwa Januari 17, mwaka huu alasiri katika eneo la Kijiji cha Kititimo nje kidogo ya Mji wa Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakidai kwenda Afrika Kusini.
Mwananchi


ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA


Mwenyekiti
wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.

Foleni
ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa
kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi
ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini,wakimsikiliza kwa
makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo
kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi
vifaa vya michezo.
Baadhi
ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo
wa soka jimboni kwake. Picha zote na Nathaniel Limu

Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9
vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi januari 20 mwaka huu.

Vifaa
hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za
magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi
ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi
hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la
Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa
misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza
wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

“Dewji
toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi
na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza
kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda
watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

Awali
msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza
kimaisha.

Kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog

WEMA SEPETU NA WENZAKE WANOGESHA UZINDUZI WA KAMPENI YA KILIMO KWANZA KWADELO, KONDOA

 Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
 Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
 Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
 Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
 Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
 Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
 Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzindzi huo
KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
 Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
 KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani
 J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
 Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
 BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
 Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
 Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampeni ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir Nkoromo

Mkuu wa wilaya ya Singida ahimiza watoto kupelekwa kupata chanjo za Rotarix na PCV 13.

Pichani Juu na Chini ni Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi (katikati) akitoa chanjo ya Rotarix kwa mtoto muda mfupi baada ya kuzindua utoaji wa chanjo hizo.(Picha na Nathaniel Limu).
Baadhi ya watoto wakiwa wanasubiri kupata chanjo mpya za Rotarix inayokinga ugonjwa wa kuharisha na PCV inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Uzinduzi wa chanjo hizo ulifanyika katika kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida kwa ngazi ya wilaya ya Singida.
Na Nathaniel Limu
Serikali wilayani Singida imewahimiza viongozi  na watendaji wote serikalini, vyama vya siasa, dini, taasisi na wadau wote, kushiriki kikamilifu kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu chanjo mbili mpya za Rotarix na PCV 13.
Chanjo ya Rotarix, inakinga ugonjwa wa kuharisha na PCV 13 inakinga ugonjwa wa nimonia kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Queen Mlozi wakati akizindua chanjo hizo mpya kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida.
Amesema utafiti uliofanywa juu ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, imebainika magonjwa ya kuharisha na nimonia yana mchango mkubwa katika vifo hivyo.
Mlozi amesema kutokana na utafiti huo, serikali imeamua kuanzisha chanjo hizo mpya ili kudhibiti vifo hivyo vinavyotokana na kuharisha na nimonia.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘mtoto asiyechanjwa ni hatari kwake mwenyewe na wengine, mpeleke akapate chanjo’.

Mamia wakwama, wawili wafariki Singida Kutokana na Mvua Kubwa Zinazoedelea Kunyesha







Wananchi wakivuka kwa miguu katika Daraja la Manung’una, lililopo katika
Kijiji cha Msisi, Singida ambalo limekatika kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha. Picha Gasper Andrew  
-- 
MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Singida, zimesababisha maafa
makubwa baada ya watu wawili, mmoja akiwa raia ya China, kufariki dunia
kwa kusombwa na maji,huku mamia ya abiria wakikwama njiani baada ya
daraja linalounganisha mkoa huo na mingine kukatika.Kukatika kwa Daraja la Munung’una kwa siku mbili
sasa,kumesababisha msongamano mkubwa wa magari yanayokadiriwa kuwa
zaidi ya 300.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa
waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni Xue Hui (36),maarufu kwa
jina la Kevin na Mariamu Samweli(18), mkazi wa Kijiji cha Maluga ambao
walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa na maji.




Vifo vyao vimeongeza idadi ya watu waliofariki
dunia kutokana na mvua mkoani Singida kufikia sita katika siku tatu
zilizopita. Mvua za juzi, zilisababisha watu wanne wa familia moja
katika Wilaya ya Mkalama kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba
ya tembe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alisema raia
huyo wa China, alifariki dunia juzi jioni katika Kijiji cha Gumanga
Wilaya ya Mkalama baada ya gari alilokuwa anasafiria kusombwa na maji...
“Mchina huo alikuwa na mtoto wake ambaye alinusurika kifo.”

Alisema
Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula
uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa
kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”




Abiria wakwama
Mvua hizo kubwa
zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha
daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani
Singida kuvunjika.

Kutokana na athari hiyo, kumekuwa na msongamano
mkubwa wa magari baada ya mawasiliano kati ya Singida na mikoa ya kanda
ya ziwa na nchi jirani kukatika.
Baadhi ya wananchi walilalamikia uharibifu huo
wakisema umetokana na ujenzi wa daraja hilo kuwa wa kiwango cha chini.
Dereva, George Medadi akitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam, alisema
daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya kiwango.

Wazazi manispaa ya Singida watakiwa kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao juu ya Ukimwi na namna ya kujikinga.



 Mkufunzi wa mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI, Dk. Elia Petro akiwajibika darasani.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida,wanaohudhuria mafunzo juu ya madhara yatokanayo na UKIMWI.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kituo cha vijana cha mjini Singida,kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT).

Kituo cha vijana mjini Singida kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
 Jumla ya wanafunzi zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida, wanahudhuria mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa, hauna kinga wala chanjo.
Wanafunzi hao kwa sasa wapo mapumziko hadi Januari shule zitakapofunguliwa.
Mafunzo hayo yanatolewa na kituo cha vijana Singida kinachomilkiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) la mjini Singida.
Mratibu wa mafunzo hayo Peter Samweli, amesema wanafunzi hao ni wale wenye umri wa miaka 12 hadi 15, na awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, yalihudhuriwa na wanafunzi  60.
Amesema awamu ya pili inayoendelea hivi sasa, ina wanafunzi 40 ambao pamoja na kujifunza juu ya UKIMWI wenyewe, pia wanafundishwa namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.
Peter amesema vile vile wanafundishwa juu ya athari za madawa ya kulevya, ulevi na namna nzuri ya kujikinga na mimba za utotoni.
Katika hatua nyingine, Peter ametoa wito kwa wazazi na walezi, kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao, mara kwa mara juu ya ugonjwa wa UKIMWI na namna nzuri ya kujikinga.
Amewataka wahakikishe watoto wao wanakuwa na ufahamu mkubwa wa athari za UKIMWI, madawa ya kulevya, mimba za utotoni na ulevi, ili waweze kujikinga na mambo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Wazazi manispaa ya Singida watakiwa kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao juu ya Ukimwi na namna ya kujikinga.



 Mkufunzi wa mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI, Dk. Elia Petro akiwajibika darasani.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida,wanaohudhuria mafunzo juu ya madhara yatokanayo na UKIMWI.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kituo cha vijana cha mjini Singida,kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT).

Kituo cha vijana mjini Singida kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
 Jumla ya wanafunzi zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida, wanahudhuria mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa, hauna kinga wala chanjo.
Wanafunzi hao kwa sasa wapo mapumziko hadi Januari shule zitakapofunguliwa.
Mafunzo hayo yanatolewa na kituo cha vijana Singida kinachomilkiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) la mjini Singida.
Mratibu wa mafunzo hayo Peter Samweli, amesema wanafunzi hao ni wale wenye umri wa miaka 12 hadi 15, na awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, yalihudhuriwa na wanafunzi  60.
Amesema awamu ya pili inayoendelea hivi sasa, ina wanafunzi 40 ambao pamoja na kujifunza juu ya UKIMWI wenyewe, pia wanafundishwa namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.
Peter amesema vile vile wanafundishwa juu ya athari za madawa ya kulevya, ulevi na namna nzuri ya kujikinga na mimba za utotoni.
Katika hatua nyingine, Peter ametoa wito kwa wazazi na walezi, kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao, mara kwa mara juu ya ugonjwa wa UKIMWI na namna nzuri ya kujikinga.
Amewataka wahakikishe watoto wao wanakuwa na ufahamu mkubwa wa athari za UKIMWI, madawa ya kulevya, mimba za utotoni na ulevi, ili waweze kujikinga na mambo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Mgana Msindai apania kufufua michezo mkoani Singida na kuwataka wadau kutoa ushirikiano.



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai akizungumzia kufufua michezo wakati akihutubia wakazi (hawapo kwenye picha) wa kata ya Aghondi jimbo la Manyoni magharibi. Mkutano huo wa hadhara ulifanyika katika kijiji cha Kamenyange.Wa kwanza kulia ni mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji na anayefuata ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni.(Picha na Nathaniel Limu).
Mwenyekiti wa CCM Mkowa wa Singida Mgana Izumbe Msindai, amedai kwamba CCM, serikali ya Mkoa na wadau mbalimbali,  kwa pamoja watashirikiana ili kufufua michezo kwa lengo la kurejesha heshima ya mkoa katika sekta ya michezo.
Msindai maarufu kwa jina la CRDB benki inayomjali mteja, ameyasema hayo wakati akizungumza na wana-CCM na wananchi kwa ujumla wa kata ya Aghodi, Kata ya Sajaranda jimbo la Manyoni Magharibi.
Amesema mkoa wa Singida katika miaka ya nyuma, ulikuwa ukifanya vizuri sana kwenye mashindano ya michezo mbalimbali, ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu, netiboli na riadha.
Msindai amesema lakini katika miaka ya hivi karibuni, michezo mkoani Singida imeporomoka kwa kasi ya  kutisha.
Amesema tatizo la kuporomoka kwa michezo ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu, kwa vile michezo ina faida nyingi.
Kwa hali hiyo, amesema mlango wa ofisi yake utakuwa wazi wakati wote kwa mtu/watu wenye maoni, ushauri na mapendekezo ya namna nzuri, itakayosaidia.

Serikali Wilayani Singida yazindua awamu ya pili ya kampeni ya Vita dhidi ya Jangwa.



Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizindua upandaji miti katika kijiji cha Kitope manispaa ya Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akishiriki kampeni ya kupanda miti ili kuokoa wilaya hiyo isikumbwe na balaa la Jangwa.


Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.

Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Serikali wilayani Singida imepiga marufuku mara moja uvunaji ovyo wa misitu, kwa madai kwamba uvunaji wa aina hiyo, unatishia wilaya hiyo kugeuka jangwa.
Mkuu wa wilaya hiyo mwalimu Queen Mlozi, ametoa agizo hilo la kupiga marufuku, wakati akizindua awamu ya pili ya kampeni ya vita dhidi ya jangwa katika wilaya hiyo.
Amesema kumekuwa na uvunaji wa ovyo wa msitu usiokuwa na uwiano na upandaji wa misitu, unachochewa kwa kiasi kikubwa na biashara ya mkaa.
Mlozi amesema hivi sasa kuna malori mengi kutoka wilaya ya Arusha na Manyara, ambayo yanasafirisha mamia kwa mamia ya magunia ya mkaa kutoka Wilaya ya Singida, biashara ambayo inataka kuacha wilaya yetu kuwa jangwa, haikubaliki na hatutaki iendelee ni lazima tuikomeshe.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuanzia sasa, vizuizi viwekwe kwenye sehemu husika  ili kuyakamata malori hayo ya mkaa na wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ant desert environment scheme Kitanto Said, alisema katika awamu hii ya pili ya kampeni dhidi ya jangwa, wanatarajia kupanda miti zaidi ya elfu moja.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa