Home » » MKUU WA MKOA WA SINGIDA AMUAHIDI JK UTENDAJI BORA KUFUATIA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA.

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AMUAHIDI JK UTENDAJI BORA KUFUATIA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA.


Mkuu wa mpya wa wilaya ya Singida mwalimu Queene Mlonzi akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.
Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi Manju Salum Msambya akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vichent Kone (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya ya Singida muda mfupi baada ya kuwaapisha.
Baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Singida waliohudhuria kuapishwa kwa wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Singida.
Mwenyekiti wa CHADEMA manispaa ya Singida John Kumalija akimpongeza mkuu mpya wa wilaya ya Manyoni Fatuma Taufiq muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama Mussa Chang’a akiwa kwenye picha na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iramba Grace Mesaki. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone amempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuupa mkoa huo timu kabambe ya wakuu wa wilaya ambayo, amedai itasaidia pamoja na mambo mengine mkoa kujitosheleza kwa chakula.
Dk. Kone ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Manyoni Fatuma Hassan Taufiq, Mussa Chang’a wa wilaya mpya ya Mkalama, Mwalimu Queene Mlonzi wa Singida, Manju Salum Msambya wa wilaya mpya ya Ikungi, Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda ambaye hata hivyo hakuwepo kwenye hafla hiyo ya kuapishwa.
Amesema wakuu hao wa wilaya anawafahamu vizuri sana uwezo wao wa kuchapa kazi ambao kwa ushirikianao na wananchi na wadau wengine wa maendeleo mkoa utapaa kimaendeleo.
Kwa upande wa wakuu wa wilaya hao, mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama Chang’a, amesema amefarijika mno na kitendo cha kuteuliwa na anakiona kuwa ni deni kubwa ambalo malipo yake ni kuwatumikia kikamilifu wakulima na wakazi wa Mkalama.
Amesema atahakikisha kilimo katika wilaya hiyo kinakuwa cha tija zaidi na masoko ya uhakika kwa mazao yao yanapatikana. 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa