DAS wilaya Iramba Singida, Yahaya Anania, akikabidhi sehemu ya msaada wa thamani ya zaidi ya Milioni moja
Wahadzabe wakisubiri msaada kutoka kwa klabu ya wanahabari mkoa Singida(SINGPRES0, walipotembelea ili kutoa msaada
Seif Takaza (kushoto), Mwenyekiti wa klabu ya wanahabari mkoa Singida akikabidhi sehemu ya msaada wa kibinadamu kwa katibu tawa
Singida, 
Mei 04, 2012. 
WANAHABARI mkoa Singida, kupitia klabu yao SINGPRESS,  wameungana  na wanahabari wenzao duniani kwa kuadhimisha siku yao kwa kutoa msaada  wa kibinadamu kwa jamii ya Wahadzabe wanaoishi kitongoji cha Kipamba,  kata Mwangeza, wilayani Iramba. 
Katika kuadhimisha siku hiyo, SINGPRESS imetoa msaada wa chakula na vifaa vya shule vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni moja. 
Msaada  huo ulikabidhiwa kwa mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya Iramba,  Yahaya Anania, kabla naye kumkabidi mwenyekiti wa kitongoji hicho,  Edward Mashimba, ili kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji,  viwafikie walengwa waliokuwepo katika hafla hiyo. 
Akipokea  msaada huo, Anania aliwashukuru wanahabari, kutokana na kuithamini  jamii hiyo, inayoishi maisha ya shida, kwa kuhamahama porini, huku  chakula chao kikuu kikiwa ni mizizi, matunda na nyama pori, ambavyo hata  hivyo hivi sasa imekuwa shida, kutokana na kuingiliwa na jamii ya  wafugaji katika eneo lao. 
Hata  hivyo, katibu tawala huyo amesema serikali kwa kushirikianana wadau  mbalimbali, imekuwa ikitoa misaada ili kuinusuru jamii na maisha ya  shida. 
Alisema  tayari serikali imetenga eneo lo na kulifanya kuwa hifadhi maalumu,  lakini pamoja na jitihada hizo, bado jamii ya wafugaji imeingilia makazi  yao na kuanza kufyeka msitu ovyo katika makazi yao. 
Kutokana  na hali hiyo, katibu tawala huyo ameitaka jamii hiyo kuwafichua wote  wanaoharibu mazingira, katika kipindi hiki ambacho taratibu zinaendelea  kuwatoa wote waliovamia eneo lao. 
Mapema  mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza, alimweleza mgeni rasmi kuwa,  wanahabari wa Singida badala ya kuadhimisha siku yao mjini, walionelea  vyema kwenda katika jamii hiyo ili watoe sauti yao ambayo itasikika  katika jumuiya mbalimbali ndani na nje, waweze kusaidiwa. 
“Sisi  tumeona badala ya kuadhimisha siku hii mjini Singida, tumeona tuje  kwenu tuwaletee hiki kidogo na jamii ingine ielewe matatizo  yenu…..kuliko hivi mnavoishi miaka yote, lakini hakuna mabadiliko  yoyote, naamini tutaungwa mkono na wengi,”alisema. 
Msaada  huo uliungwa mkono kwa kupigwa jeki na mfanyabiashara maarufu wa mjini  Singida, Bw. Nagji, ambaye alijitolea katoni kadhaa za sabuni ya  kufulia, Biskuti, madaftari na pipi, ili kuisaidia jamii hiyo.
Na Elisante John  



0 comments:
Post a Comment