Afisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Singida Bw.Patrick Mwaluli akitoa taarifa yake kwenye maadhimisho ya siku ya taaluma ya halmashauri hiyo.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Singida waliozawadiwa simu za vingajani kwa kufanya vizuri katika taaluma.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Afisa elimu mkoa wa Singida, Yusuph Kipengere, amewaagiza waratibu elimu kata, kuongeza kasi ya kuratibu na kusimamia kikamilifu utoaji taaluma, ili lengo la mkoa la kufaulisha mtihani wa kitaifa wa kumaliza elimu ya msingi kwa asilimia 85 lifanikiwe.
Kipengere ameto agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya taaluma wilaya ya Singida, yaliyofanyika Sepuka kilomita 27 magharibi ya Singida mjini.
Alisema jukumu la mratibu elimu wa kata, ni kuhakikisha kila mwalimu katika kata yake anatekeleza ipasavyo majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi.
Katika hatua nyingine, Kipengere alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa elimu wilaya ya SIngida, kwa uamuzi wake wa kupongeza shule na walimu waliofanya vizuri katika utoaji taaluma mwaka jana.
“Utaratibu huu ni mzuri mno, binadamu ukimpongeza na kumpa zawadi hata iwe ndogo namna gani, hujisikia kuheshimiwa sana,na hivyo ataongeza juhudi zaidi katika utendaji wake wa kazi. Naziomba wilaya zingine nazo ziige mfano huo”,alisema.
Halmashauri ya wilaya ya Singida, ina jumla ya shule za msingi 192 na shule za sekondari 61, kati ya hizo, shule 2 za msingi ni za binafsi na shule tano za sekondari ni za binafsi.
0 comments:
Post a Comment