LOWASSA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA WANYATURU, MKOANI SINGIDA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mmoja wa wazee wa Kimila wa Kabila la Wanyaturu, Mzee Semani Nyambia akimvisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, vazi la kimila (mgololi) ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa mlezi wa Wanyaturu, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, SINGIDA.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015. katika hotuba yake, Mh. Lowassa amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Rais wa Tanzania, ataanzisha viwanda vya kusindika zao la alizeti, ili wakulima wa zao hilo waweze kufaidika na pia atakabiliana na kero zote za Mkoa wa Singida kwa ujumla. Mh. Lowassa, kesho Septemba 14, 2015 ataendelea na ziara yake ya Kampeni katika Mkoa Shinyanga, baada ya leo kumaliza katika Mkoa wa Singinda, kwenye Majimbo ya Manyoni Magharibi, Singida Kaskazini, Iramba Mashariki na Iramba Magharibi.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA katika Jimbo la Singida Kaskazini, David Djumbe,  wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, baadhi ya wagombea wa Udiwani wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.

Hawa wote wameahidi kuwapakura.
Vijana wa Ilongero wakifatilia kwa makini Mkutano huo.
Wananchi wa Ilongero, Singida Kaskazini wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Wakiperuzi picha za Mgombea wao.

Kina Bibi Mkutanoni.
Furaha toka moyoni.
Mzee Msindai akizungumza.
Chopa ikitua.































Mwigulu Nchemba awashukia wapinzani wanaotumia hotuba za Baba wa Taifa kwa mtaji wa kisiasa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC01685Naibu waziri wa fedha na mgombea ubunge jimbo la Iramba,Mwigulu Nchemba,akihutubia mamia ya wakazi wa wilaya ya Mkalama waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge na udiwani CCM uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa kijiji cha Iguguno jana..
DSC01700Naibu waziri wa fedha na mgombea ubunge jimbo la Iramba mkoa wa Singida,Mwigulu Nchemba,akimkaribisha mgombe ubunge jimbo la Mkalama,Alan Joseph Kiula jana,kuomba kura kwa wakazi wa wilaya ya Mkalama kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa michezo wa kijiji cha Iguguno.
DSC01735Naibu waziri wa fedha na mgombea ubunge wa jimbo la Iramba mkoa wa Singida,Mwigulu Nchemba (kushoto) akiwatambulisha wagombe ubunge viti maalum,Martha Malata (katikati) na Shyrose Matembe (kulia) mbele ya mkutano wa kampeni za nafasi za ubunge na udiwani jimbo la Mkalama jana.
DSC01729Mgombea ubunge jimbo la Mkalama mkoa wa Singida,Alan Joseph Kiula,akiomba kura kwenye mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa jimbo hilo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa kijiji cha Iguguno jana.
DSC01732Mgombea udiwani CCM kata ya Iguguno tarafa ya Kinyangiri,Lyochi,akiomba kura kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa kijiji cha Iguguno jana na mgeni rasmi alikuwa naibu waziri wa fedha,Mwigulu Nchemba.Picha zote na Nathaniel Limu.
DSC01632
Naibu waziri wa fedha na mgombe ubunge jimbo la Mkalama mkoa wa Singida, Mwigulu Nchemba (mwenye skafu), akiingia kwenye uwanja wa michezo wa kijiji cha Iguguno,kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani CCM zilizofanyika jana.Wa pili kushoto mrefu aliyenyanyua mkoano juu,ni mgombea ubunge jimbo la Mkalama, Alan Joseph Kiula. 


Mwigulu pamoja na mambo mengine,amewataka wakazi wa mkoa wa Singida,kuichagua CCM kwa madai ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuwatumikia wananchi.
Naibu Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewataka Viongozi/ watu wanaojifanya mabingwa wa kutumia baadhi ya hotuba za hayati Mwalimu Julius Nyerere kujinufaisha kisiasa, watumie pia hotuba za hayati Nyerere zenye mwelekeo wa kuwakosoa,ili waweze kuthibitisha ubingwa wao.
Amedai mabingwa hao wakiweza kutoa ufafanuzi hata kwa hotuba zinazowakwaza,kwa njia hiyo, watakuwa wanawajengea wananchi mazingira mazuri ya kutoa maamuzi stahiki Oktoba 25 mwaka huu wakati wa kuchagua viongozi wanaowataka.
 
Mwigulu ambaye anatetea nafasi yake ya ubunge jimbo la Iramba kwa awamu ya pili mfululizo, ametoa wito huo juzi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani, jimbo la Mkalama mkoani Singida.
 
Akifafanua,alisema hivi karibuni baadhi ya wagombea mbalimbali wakiwemo wa nafasi ya urais, wamekuwa wakitumia baadhi ya hotuba za hayati baba wa Taifa, wakilenga kuwaaminisha wananchi kuwa wawachague kwa madai watafuata nyayo za hayati baba wa faifa, na kwamba wanauchungu na wananchi.
 
“Wengi wa viongozi hawa wanajaribu kuwahadaa wananchi kwa kitendo chao cha kuhama CCM kimezingatia maneno yaliyowahi kutolewa na hayati baba wa taifa kuwa, mabadiliko usipoyapata ndani ya CCM, unaweza kuyapata nje ya CCM”,alisema.
 
Akifafanua alisema mabadiliko ya kweli yaliyokuwa akiyazungumzia hayati Nyerere, sio ya kuhama vyama, ni mabadiliko ya kiutendaji ambayo yatafanyika  ndani ya CCM na si kwa kukimbilia upinzani.
 
Mwigulu alisema kuwa itapendeza zaidi endapo mabingwa hawa watazungumzia pia maneno yaliyotolewa na hayati rais wa kwanza,Nyerere,kwamba ‘anayekimbilia kwenda ikulu kwa kutumia fedha,fedha hizo atazirejeshaje’.
 
“Kama wao ni mabingwa,basi wazungumzie maneno ya hayati Julius Nyerere ya ‘ikulu kuna nini pale hadi mtu apakimbilie,mtu aote rushwa hadi kwenye vyuo mbalimbali,hizo pesa amezitoa wapi na kama amekopa,atazirejeshaje.Wakizungumzia maneno hayo ambayo yapo kwenye hotuba ya hayati baba wa taifa na kutupa majibu ya kuridhisha,pengine kidogo tunaweza tukawaelewa”,alifafanua zaidi.
 
Katika hatua nyingine,Mwigulu alisema wana CCM waliokihama Chama cha Mapinduzi baada ya kushindwa kwenye kura za maoni, huko walikokimbilia kutimiza azma yao au tamaa zao  za kutaka uongozi, wasipopata wanachokihitaji, baada ya Oktoba 25 mwaka huu, watarejea CCM.
 
“Wewe fikiria mtu kama Lowassa amelelewa na CCM takribani  miaka 40 sasa, kichwa chake chote hakina kitu kingine kimejaa CCM. Mambo ambayo atataka kuyaanzisha kwenye Ukawa yatakuwa na harufu kubwa ya CCM tu. Kwa hiyo, huko walikokimbilia kusaka uongozi njia yo yote ikiwemo ya matumizi ya makubwa ya rushwa, wamekwenda kuanzisha CCM (B) hakuna cha ziada”,alisema.
 
Akisisitiza, alisema upinzani kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu haupo kabisa, ni kilichopo ni CCM (A)na CCM (B ndizo zitakazochuana  kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Aidha, Mwigulu ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatishwakatishwa kwa kushangiliwa, amewataka wakazi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla, wasikubali hadaa inayotolewa na mgombea urais kupitia Ukawa, eti akichaguliwa serikali yake ataiendesha kwa kasi ya aina yake ambayo haijawahi kutokea nchini.
 
Mwigulu amesema mgombea huyo, yeye mwenyewe hana kasi aina hiyo anayoisema.
 
“Ongea ya mgombea huyo, ninyi ni mashahidi, anaongea kwa kasi inayofanana na mwendo wa kinyonga, hotuba zake hazizidi dakika tano, kunyanyuka kwake kutoka kwenye kiti, ni kwa kasi ya kinyonga vile vile,hapo alipo hana kabisa  kumbukumbu ya kitu cho chote kichwani mwake,na mbaya zaidi hawezi kusafiri kwenye barabara za vumbi kiuno kitamletea matatizo makubwa”,alisema.
 
Alisema chaguo la Watanzania kwa nafasi ya urais wa awamu ya tano, ni DK. John Pombe Magufuli, ambaye ni mtu asiyekuwa na makandokando, mwadilifu na mchapakazi wa kupigiwa mfano.
 
Mwigulu,alisema anayoimani kubwa kwamba Watanzania wote watampa DK. Magufuli kura ya ndio na watachagua wabunge na madiwani wote kutoka CCM A na si vinginevyo

Hospitali ya Mkoa Singida yapigwa tafu ya mashuka na benki ya Posta nchini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC01622
Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida, Redenoter Rweyemamu, akizungumza kwenye hafla ya benki hiyo kutoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili, kwa hospitali ya mkoa mjini hapa, inayokabiliwa na uhaba wa shuka na kusababisha wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
DSC01626
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk. Daniel Tarimo, akitoa shukrani zake kwa benki ya posta tawi la Singida mjini kwa msaada wake wa mashuka kwa hospitali hiyo.Dk.Tarimo amedai kuwa bado hospitali hiyo inaupungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.
DSC01611
Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida mjini (katikati),akimkabidhi Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk.Daniel Tarimo mashuka 104. Mashuka hayo yamepunguza makali ya uhaba mkubwa wa shuka na sasa, kuna upungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.
DSC01629
Bango la benki ya posta.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
BENKI  ya Posta Tawi la Singida Mjni, imetoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa hospitali ya mkoa ya mjini hapa, ili kupunguza uhaba mkubwa unaoikabili hospitali hiyo.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Redempter Rywemamu, alisema hatua hiyo imechukuliwa  na benki ya posta,ikiwa ni  ni kuitikia  wito uliotolewa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, kusaidia hospitali hiyo shuka, kwa lengo la kumaliza tatizo linaloelekea kuwa sugu la uhaba wa shuka.
“Sisi kama benki ya posta, tunalo jukumu la kuhakikisha tunashiriki kikamilifu kutatua kero zinazoikabili jamii ambayo ndani yake, hapo wateja wetu. Hospitali yetu hii ya mkoa, tunafahamu inapokea wagonjwa na majeruhi wengi, kwa hiyo pamoja na msaada wa leo, niahidi tu kwamba tunaendelea kusaidia kadri uwezo utakavyoturuhu” alisema.
Naye Afisa muuguzi wa hospitali hiyo, Amina Mlangida, alitumia fursa hiyo kuishukuru benki ya Posta Singida, kwa msaada wa mashukua hay, kwa kudai msaada huo umetolewa kwa wakati muafaka.
Alisema hospitali hiyo kongwe mkoani hapa, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa shuka unaochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi, kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
“Afisa Mlangida alitumia nafasi  hiyo kuwaomba  wadau wengine wa sekta ya afya, kuiga mfano wa benki ya Posta, katika kusaidia kupunguza uhaba mkubwa  wa shuka kwenye hospitali hii ya Mkoa”,alisema.
Kwa upande wake, Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk. Daniel Doniel Tarimo, alisema baada ya kupokea msaada wa mashuka kutoka benki ya Posta, bado hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2000, magodoro 236.
Dk. Tarimo alitumia fursa hiyo kuialika benki ya posta kwa ajili ya kukutana  na wafanyakazi wa hospitali hiyo,  ili kuwafahamisha/kuwaelemisha juu ya  huduma zinatolewa na benki hiyo, pamoja na mikopo itakayosaidia kupunguza makali ya maisha ya wafanyakazi hao.
Mo Blog

MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MATUNDU NANE YA CHOO BORA KWENYE SHULE YA MSINGI KIBAONI SINGIDA DSC01579

DSC01579
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
DSC01583
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
DSC01592
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
DSC01596
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
DSC01600
Mwakilishi wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
DSC01603
Jengo la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua, alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MAMA SAMIA AHUTUBIA SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

unnamed
Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati, akimuombea kura Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni mkoani Singida, leo.(Picha na Bashir Nkoromo).

ABBAS MAZIKU: MFANYABIASHARA ANAYETAMANI KUFUATA NYAYO ZA BILIONEA MO DEWJI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

04.jpgk
Mfanyabiashara wa Kimataifa Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO' amabaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.
Na Mwandishi Wetu
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.
Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.
Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini Vietnam aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.

Alipoanzia

Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba yaliyokuwa na mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Choroko, Mtama, Alizeti, Mashudu yapamba na pamoja na Pilipili Manga.

Anayapata wapi mazao?

Anasema mazao huyakusanya kutoka kwa wafanyabaishara wadogo wadogo ambao hukusanya mazao kwa wakulima pamoja na minada inayofanywa na vyama vya ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa kila wiki.

Anayasafirisha kwa njia gani?

Akizungumzia jinsi anavyosafirisha mazao hayo, Maziku anasema hutumia usafiri wa barabara kuyatoa mikoani hadi kuyafikisha kwenye maghala ambayo hutumia kuyahifadhi kabla ya kufungasha.
"Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa nayafungasha kwa kutumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina la kampuni yangu na baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS na ndipo hufuatiwa na hatua ya mwisho ya usafirishaji ambayo huwa natumia Meli za mashirika mbalimbali ikiwemo IPTL, MAERSK na nyinginezo kwa ajili ya kwenda nchini Vietnam", anasema Maziku.
Anabainisha baada ya hatua zote hizo hufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo watu wa Mamlaka ya mapato T.R.A, wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Ufugaji, Wanasheria pamoja na maofisa wa usalama wa Taifa ambao uhakikisha hatua zote halali zimefutwa.
Maziku anaweka bayana kwamba kwa biashara za kimataifa taasisi kama Shirika la viwango TBS na mamlaka ya Chakula na Dawa huwa hawahusiki bali wahusika wakuu ni SGS.

Anajiendeshaje Kibiashara?

Maziku anajinasibu kuwa biashara ya mazao kupeleka nje ya nchi ni biashara yenye ushindani mkubwa hivyo anakumbuka alianza na mtaji wa sh 2,000,000 na sasa anazungumzia mtaji wa sh mil 200.
“Si rahisi kufika nilipofikia kwa sababu biashara hii ina ushindani mkubwa, ninashindana na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na zaidi”, anasisitiza kwa hisia kali.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara ya mamilioni ya pesa baada ya ubora wa mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa hivyo ilimpa wakati mgumu ambao aliyumba kibiashara kutokana na mtaji wake kukata hivyo ili mlazimu kuingia benki na kukopa pesa ambazo hadi sasa bado analipa deni hilo.
“Nilipata hasara kubwa sana ambayo hadi leo hii bado ninalipa hilo deni nililokopa benki ingawa pia fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ya biashara zingine ninazozifanya zinaendelea kuifanya biashara hii ya mazao kwenda nje ya nchi iendelee kuwepo” anasema Mfanyabiashara huyo wa kimataifa.

Kaimu Msimamizi wa uchaguzi Singida mjini atupilia mbali pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC01221
Kaimu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini, Gerald Muhabuki Zephyrin,akizungumza na Modewjiblog juu ya uchaguzi ubunge jimbo la Singida mjini.(Picha na Gasper Andrew).
Na Nathaniel Limu, Singida
PINGAMIZI lililowekwa na Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA),jimbo la Singida mjini, dhidi ya mgombea wa CCM Mussa Ramadhan Sima kuwa fomu zake haziko sawa kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za uchaguzi,limetupiliwa mbali kwa madai kwamba halina mashiko.
Akizungumza na mwakilishi wa Modewjiblog ofisini kwake, kaimu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini,Gerald Muhabuki Zephyrin, alisema kuwa CHADEMA iliwasilisha pingamizi kwamba barua ya kumthibitisha Sima kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM, imesainiwa na mtu ambaye hakubaliki kisheria.
Akifafanua, alisema mgombea wa jimbo la Singida mjini kupitia CHADEMA, Msindai Mgana Izumbe, amelalamikia barua hiyo kuwa imesainiwa na  Mary Maziku, kwa madai sio katibu halisi wa mkoa wa Singida.
Gerald alisema katika  kujiridhisha kama kweli Maziku sio mtu stahiki wa kumuthibitisha mgombea wa CCM kwenye nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini,aliwasiliana na makao makuu CCM Lumumba jijini Dar-es-salaam,na kujibiwa kwa barua kwamba Maziku ndiye katibu wa CCM mkoa wa Singida.
“Mgombea Msindai ambaye alikuwa mwenyekiti CCM mkoa hadi kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni,katibu wake wa mkoa kwa wakati huo, alikuwa Mary Chatanda ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mary Maziku kipindi cha mchakato wa kura za maoni unaendelea.Maziku ndiye aliyesaini barua ya kumthibitisha Sima”,alifafanua zaidi.
Katika hatua nyingine,Gerald ambaye ni mkuu wa idara ya utumishi na utawala manispaa ya Singida,amesema kuwa aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Singida mjini,Victoria John Msusu kupitia UPDP,ameeguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kushindwa kuwasilisha fomu kwa wamadai na kushindwa kulipa ada ya fomu shilingi 50,000.
Msimamizi amewataja wagombea wa ubunge wa jimbo la Singida mjini waliopitishwa na chama kwenye mabano kuwa ni ni pamoja na Sima (CCM),Jeremia Paulo Wandili (ACT Wazalendo),Msindai Mgana Izumbe (CHADEMA) na Mwanamvua John Haji (CUF).
Alisema kampeni zimeishaanza vizuri kwa amani na utulivu mkubwa na amewaoomba wagombea kufanya kampeni kwa ustarabu na kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za uchaguzi.
“Matarajio ya wananchi wa jimbo la Singida mjini,ni kwamba oktoba 25 mwaka huu,wapige kura kuwachagua viongozi wanaoamini watawaletea maendeleo ya kweli na si vinginevyo”, alisema Gerald.

Mgana Msindai achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo ya Singida mjini kwa tiketi ya CHADEMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
IMG-20150821-WA0001
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa wenyeviti CCM mikoa ya Tanzania, Mgana Izumbe Msindai, akikabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya manispaa ya Singida, Joseph Mchina ya kugombea ubunge jimbo la Singida mjini kupitia tiketi ya CHADEMA.
(Picha na Nathaniel Limu).
 

Nyalandu achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

FOMU
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu akichukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kwa  MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI, Mkurugenzi Mtendaji HAJJAT MWASUMILWE.
hotubA
Nyalandu akihutubia wananchi Kinyagigi.
kinyagigi
Lazaro Nyalandu akiwa Kinyagigi.
MAPOKEZI
Wananchi wa kijiji cha Kinyagigi wakimpokea Nyalandu.
 
 

Kijana tajiri Afrika ni Mtanzania

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mfanyabiashara tajiri kijana Mohamed Dewji
Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.
Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .
“Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo.
Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.
Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.
Kwa mujibu wa tovuti yake, Metl inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.
Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Dewji anashika nafasi mbili juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho.
Rostam amefungana nafasi ya 26 na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na Femi Otedola wenye utajiri wa Sh1.8 trilioni kila mmoja.
Orodha hiyo ya 29 bora inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa na utajiri wa Dola 15.7 bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango ambacho ni mara moja na nusu ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka 2014/15.
Forbes linamtaja Rostam kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.8 trilioni), kiwango ambacho kimebaki pasi na mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana. Rostam anamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom.
BBC

CHAGUA AMANI RAI KATIKA KURA ZA MAONI SINGIDA MJINI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chagua Amani Rai Jimbo la Singida Mjini.

Maziku amaliza mgogoro wa Nyalandu na wenzake, waendelea na mchakato kuomba kura kwa wananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KATIBU
Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mgogoro wa wagombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini.
maziku
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku akiwa ofisini kwake.
MONKO
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, Jastine Monko akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la CCM Mkoa wa Singida baada ya kumaliza tofauti zao.
nyalandu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya CCM Mkoa wa Singida, mara baada ya kikao cha maridhiano baina yake na wagombea wenzake saba kumalizika na kuondoa tofauti zao.
GARI
Wagombea wa Ubunge Singida Kaskazini wakipanda gari kuendelea na mchakato kwa kuomba kura kwa wananchi baada ya kumaliza kikao na Katibu wa CCM Mkoa Mary Maziku.(PICHA ZOTE NA HILLARAYSHOO,  SINGIDA).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
Hatimae mgogoro uliokuwa ukifukuta kwa wagombea saba wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kutaka kugomea kuendelea na mchakato wa kura za maoni umemalizika na sasa wagombea hao wanaendelea na zoezi.
Hatua hiyo ya wagombea saba kutaka kugomea ilidaiwa ni kutokana na mgombea mwenzao Lazaro Nyalandu kukiuka taratibu za mchakato huo, na hivyo kuonekana kana kwamba anabebwa na viongozi wa Wilaya ya Singida vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana , Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku alisema baada ya kikao cha kuwakutanisha pande zote mbili , kila moja alikuwa na malalamiko yake, lakini baada ya kikao cha pamoja cha zaidi ya saa moja, walimaliza suala hilo.
Maziku alisema kuwa kilichotokea ni siasa za kupakana matope, kuchafuana , kudharauliana na kejeli za hapa na pale miongoni mwa wagombea hao.
Aidha alisema baada ya kusikiliza malalamiko ya wagombea saba Justine Monko, Yohana Sintoo, Amos Makiya, Alon Mbogo, Sabasaba Manase, Michael Mpombo na Mungwe Athuman,dhidi ya Nyalandu  ambaye nae alikuwa na malalamiko yake, walikubaliana kimsingi kuondoa tofauti zao kwa kuwa wote ni wana CCM.
“Hawa saba walikuwa wakimlalamikia Nyalandu lakini na yeye alikuwa akiwalalamikia hawa, sasa baada ya ya kukaa pamoja tumeona hakuna haja ya kuendelea na malumbano kwa kuwa wote wameonekana kuwa na makosa madodo madogo ambayo hayana mashiko bali ni siasa za kawaida kwenye chaguzi mbalimbali.” Alisistiza Maziku.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema hana tatizo na mgombea yeyote na kwamba madai ya wagombea wenzake kumlalamikia ni dalili za kuanza kushindwa.
“Mimi niwaambie waandishi wa habari nimefanya mambo mengi katika Jimbo hili la Singida Kaskazini na wananchi watanipima kwa kazi sio maneno, na nina uhakika wa kupata zaidi ya aslimia 90 ya kura za maoni.”Alijigamba Nyalandu huku akionesha kujiamini sana.

NDOTO YA WEMA SEPETU KUWA MBUNGE YAYEYUKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Haikuwa bahati yake. Safari ya Wema Sepetu kuelekea bungeni imefikia tamati.

Hiyo ni baada ya kushindwa kuwashawishi wanachama wa CCM mkoani mkoani Singida kumpa dhamana ya kuwawakilisha kwenye viti maalum vya ubunge.
Wema ameshindwa kupita kwenye kura za maoni za ubunge huo kwa kupata kura 90 tu. Aliyeongoza kwenye kinyang’anyiro hicho ni Aysharose Mattembe (311), Martha Mlata (235) na Diana Chilolo (182).
Wema amekubali kushindwa na kudai kuwa ushiriki wake umempa ujasiri zaidi.
“Nilivyoamua kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka,” ameandika kwenye kwenye Instagram.
“Nawapongeza walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo. Nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya,” ameongeza.
“2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things loading.. Most of all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi na nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo kwanza inaanza.”

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa