SINGIDA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA USAFI WA MAZINGIRA KIKAMILIFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Evelyn Mkokoi – Singida
Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.
Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.
Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.
“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.
Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI MKOANI SINGIDA WAMETOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 20 KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 





Na Evelyn Mkokoi-Singida
Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.
Baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.
Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.
Aidha Baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Injinia Joakim Masakala  akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi katika mwili wa binadamu.
Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo Hatarini kutoweka kabisa.
 

WAFANYABIASHARA MKOANI SINGIDA WAJIPATIA BILIONI 1.8 KWA MAUZO YA KUKU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Nathaniel Limu-Singida
Wafanyabiashara wa kuku wa asili/kienyeji mkoani Singida wamejipatia mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, baada ya kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha mwaka jana hadi sasa.
 
Hayo yamesemwa juzi na kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji wakati akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili, kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.
 
Chowaji amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kuku hao 151,242 kusafirishwa  na kuuzwa nje ya mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.
 
“Kuku wa asili wakifungwa vizuri kwa kudhibiti ugonjwa wa mdondo na kuzingatia kanuni za ufugaji bora wanaweza kuleta mabadiliko makubwa na ya haraka ya kipato. Kuku wa asili pia ni lishe bora hususani kwa watoto na akina mama”, ameongeza Choaji.
 
Ili kuimarisha ufugaji kuku wa asili amesema imependekezwa halmashauri zote zitekeleze mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka kwa kutumia watoa chanjo wasiokuwa wataalam wa mifugo.
 
Akisisitiza amesema “Mkakati huu unatarajiwa kuanza mara halmashauri zitakazokamilisha utoaji wa mafunzo kwa watoa chanjo hao. Halmashauri zimesisitizwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mkakati huo ili kuinua kipato cha wananchi kwa haraka zaidi”.
 
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kikao hicho, Mhandisi Mathew John Mtigumwe, akifungua kikao hicho ameagiza kuwa wananchi wahamasishwe, ili wasiendelee kuuza chakula walichovuna msimu uliopita kiweze kuwafikisha msimu ujao wa mavuno.
 
Mhandisi Mitugumwe amesema kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) mvua za msimu huu zinatarajiwa kunyesha kwa kiwango cha chini ya wastani.
 
“Hivyo ni jukumu letu sote kuhimiza na kushauri wananchi kufuata kanuni bora za kilimo na kupanda mazo ya kipaumbele yanayostahimili ukame, na yanayokomaa mwa muda mfupi.
 
Wakati huo huo Mkuu huyo wa mkoa, ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa wananchi wadau wa elimu, wafanyabiashara, kampuni za simu za viganjani na mashirika ya umma na binafsi, kwa kushiriki kutekeleza agizo la rais Magufuli la kumaliza uhaba wa madawati mashuleni.

WAZIRI MWIGULLU AWAONYA MADEREVA WANAOACHA MITI NA MAWE BARABARANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Nathaniel Limu- Singida
Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba (mb), ameliagiza jeshi la polisi nchini,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria  madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.

Nchemba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida, ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha 38 cha bodi ya barabara mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.
 
Amesema baadhi ya madereva wa magari na hasa yale makubwa,hutumia mawe kuzuia magari yao kutembea wakati wakiyafanyia matengenezo ya dharura.
 
“Wakiisha maliza kuyafanyia matengenezo magari yao, madereva hao huyaacha barabarani mawe na matawi ya miti ambayo hutumika kutoa tahadhari kwa vyombo vingine vya moto. Kitendo hicho kinahatarisha maisha na mali za watumiaji wengine wa barabara kwa vile yanaweza kusababisha ajali”, amesema Mwigullu.
 
Kwa hali hiyo amesema jeshi la polisi linapaswa kuimarisha mawasiliano ili waweze kuwathibiti na kuwakamata madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.
 
Katika hatua nyingine, waziri huyo amesema upo umuhimu mkubwa wa wananchi na hasa wale wanaoishi kando kando ya barabara kuelimishwa juu ya matumizi bora ya barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi ili waweze kuacha kupitisha mifugo yao na mikokoteni barabarani.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya barabara na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameagiza kuwa fedha zinazotolewa na serikali na wafadhili mbalimbali wa miradi ya barabara matumizi yake yasimamiwe kikamilifu, ili zitumike kwa miradi iliyokusudiwa.
 
“Ujenzi wa miradi hiyo ya barabara ufanane na thamani halisi ya fedha zilizotumika. Pia kazi za ujenzi wa barabara za ngazi zote wapewe wakandarasi bora na wenye uwezo wa kutekeleza miradi ikakamilika kwa wakati. Nasisitiza kuimarishwa kwa usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara wa miradi ya barabara ili ziwe za kiwango kinachokusudiwa”,amesema.
 
Wakati huo huo, mhandisi Mtigumwe ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa alikuwa meneja TANROADS mkoa, ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa TANROADS mkoa wa Singida chini ya meneja wake Mhandisi Leonard Kapongo kwa kazi nzuri ya usimamizi na ukaguzi uliopelekea miradi ya barabara kujengwa kwa ubora unaofafana na fedha zilizotumika.

ANNE MAKINDA AZITAKA HOSPITALI ZA SERIKALI ZIBORESHE HUDUMA ILI ZIPATE WATEJA WENGI WA BIMA YA AFYA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda amezishauri hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali kuboresha huduma za afya ili wananchi waliojiunga katika mifuko ya afya ya jamii (CHF) na mfuko wa bima ya afya washawishike kutumia huduma katika hospitali zao.

Makinda ametoa rai hiyo alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa na changamoto zilizopo ili kwa ushirikiano wa mfuko wa bima ya afya na wadau wake waweze kuzitatua.

Amesema hospitali na vituo binafsi au vya mashirika mbalimbali wamekuwa wanufaikaji wakubwa wa kupata wateja wengi wa bima ya afya na mifuko ya afya ya jamii kutokana na kusifiwa kuwa wanatoa huduma bora tofauti na hospitali za serikali ambazo hupata wateja wachache na hivyo kupata faida kidogo.

Makinda amesema hamasa anayoitoa ya kuboresha huduma kwa vituo vya serikali haimaanishi mfuko wa taifa wa bima ya afya hauthamini vituo na hospitali binafsi bali inataka hospitali za serikali kuboresha huduma na kuingia katika ushindani.

Ameongeza kuwa changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba inawakatisha tamaa watumiaji wa bima ya afya pamoja na watu wengine kujiunga hata hivyo mfuko wa bima ya afya na hospitali za serikali zimejipanga kuziondoa changamoto hizo.

Aidha Makinda ameupongeza Mkoa wa Singida kwa kufanya vizuri katika mfuko wa afya jamii na bima ya afya huku akisisitiza kuendelea kuboresha ili Mkoa wa Singida uwe mfano kwa mikoa mingine ya Tanzania.

Akitembelea majengo mapya ya hospitali rufaa iliyopo eneo la Mandewa Makinda amevutiwa sana na majengo hayo huku akiutaka uongozi wa Mkoa kwa kushirikia na wadau wengine hasa mfuko wa bima ya afya kutafuta pesa za ukamilishaji wa majengo muhimu ili huduma zianze kutolewa katika hospitali hiyo kwakuwa itakuwa msaada hata kwa kanda nzima ya kati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew J Mtigumwe amemshukuru Anne Makinda kwa kuutembelea mkoa wa Singida ili kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amemuahidi Makinda kuwa Mkoa utaendeleza ushirikiano mzuri na Mfuko huo na kuomba waendelee kutoa ushirikiano wa vifaa tiba na ukarabati wa miundombinu ya hospitali na vituo vya afya vya serikali ili kuboresha huduma za afya Mkoani Singida.

Ameongeza kuwa Mkoa utaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii na bima ya afya ili wapate huduma bora hata wakati wakiwa na upungufu wa fedha kwani bima huokoa maisha.

WAGONJWA WA KISUKARI SINGIDA WAADHIMISHA SIKU YA KISUKARI DUNIANI KWA KUPIMWA MACHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Daktari bingwa wa macho Mkoani Singida Ngh'ungu Kuzenza akimfanyia uchnguzi wa macho mgonjwa wa kisukari katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.
 Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wa kliniki ya Hospitali ya Mkoa wa Singida wakisubiria kufanyiwa uchunguzi wa  macho katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.


Na Grace Singida

Wagonjwa wa kisukari Mkoani Singida leo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya macho na daktari bingwa wa macho katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari duniani ikiwa na kauli mbiu ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya macho.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida Dokta Ramadhani Kabala amewaambia wagonjwa wa kisukari waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi wa macho kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yamelenga kuzuia wagonjwa wasiathirike zaidi na magonjwa yatokanayo kisukari.

Dokta Kabala amesema ugonjwa wa kisukari hushambulia zaidi macho, figo na moyo hivyo serikali imeweka mkazo wa kuwafanyia uchunguzi ili kubaini tatizo ili wapatiwe matibabu mapema au kuzuia yasitokee kabisa kwa kufuata kanuni na taratibu za ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa ugonjwa wa kisukari unawakumbusha watu kuishi kwa kufuata kanuni bora za afya kama kula mlo kamili, kula matunda badala ya juisi zilizotengenezwa viwandani, kufanya mazoezi na kupunguza vilevi na sigara hivyo wagonjwa wa kisukari hawana togauti na watu wengine isipokuwa wao hushauriwa kufuata kanuni hizo kwa umakini mkubwa.

Dokta Kabala amewakumbusha kutumia dawa kwa kufuata usahuri wa daktari wao pamoja na kuhudhuria kliniki za kisukari kwakuwa kliniki hizo zinawasaidia katika kushauriana namna bora ya kuishi kwa kufuata masharti wananyopewa pamoja kuelimishanzaidi juu ya ugonjwa huo.

Naye Daktari bongwa wa macho Mkoani Singida Dokta Ngh’ungu Kuzenza amesema utaratibu huo unasaidia kuzuia au kupunguza madhara ya ugonjwa wa kisukari kwakuwa wengi watatambuliwa kabla hawajafikia hatua ya kupofuka.

Dokta Kuzenza ameongeza kuwa changamoto kubwa ni watu wengi kutopima ugonjwa wa kisukari mapema mpaka wanapougua na hivyo kujikuta wameshaathirika macho ndipo hutafuta huduma.

Kwa upande wake mmoja kati ya wagonjwa wa kisukari 76 waliopata huduma ya kibingwa ya macho Bi Asha Selemani Waziri Mkazi wa Iguguno ameema serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuwapima macho ili waweze kupata tiba mapema.

Bi Waziri ameiomba serikali kuendelea kuweka utaratibu wa kuwapima wagonjwa wa kisukari magonjwa mbalimbali kama moyo na figo huku akiwashauri wagonjwa wa kisukari kufuata ushauri wanaopewa na  wataalamu wa afya.



DC MTATURU AZINDUA UHABARISHO WA MAFUNZO YA KUIJENGEA UWEZO JAMII KATIKA KUIBUA NA KUPANGA MIRADI YA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka
 Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi

Na Mathias Canal, Singida

Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo.

Mradi huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo endapo zitapatiwa upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba wananchi ambapo amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina vituo 39 tu vya kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60, Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna nyumba za walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji wa majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo majosho 20 ni mabovu.

Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo Asasi mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa tofauti na usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua ikiwemo kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi.

Dc Mtaturu alisema kuwa Mradi huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie matakwa ya kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa ya kufanikisha maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee.

Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo kuwa ni wananchi wote wa kijiji cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100 kutoka kila kijiji ambao watachaguliwa ili kuendesha zoezi la kutengeneza bajeti ya mpango wa kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku tatu mfululizo na watu mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi mengine wapatao 20.

Alisema kuwa Jumla ya gharama zote za kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii katika kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika vijiji kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni hamsini (50,000,000/=).

Makyao alisema katika awamu hii ya vijiji kumi vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa kati ya lengo la watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.
KAWAIDA...! DC MTATURU AZINDUA UHABARISHO WA MAFUNZO YA KUIJENGEA UWEZO JAMII KATIKA KUIBUA NA KUPANGA MIRADI YA MAENDELEO Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi Na Mathias Canal, Singida Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo. Mradi huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi. Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo endapo zitapatiwa upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba wananchi ambapo amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina vituo 39 tu vya kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60, Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna nyumba za walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji wa majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo majosho 20 ni mabovu. Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo Asasi mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa tofauti na usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua ikiwemo kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi. Dc Mtaturu alisema kuwa Mradi huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie matakwa ya kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa ya kufanikisha maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee. Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo kuwa ni wananchi wote wa kijiji cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100 kutoka kila kijiji ambao watachaguliwa ili kuendesha zoezi la kutengeneza bajeti ya mpango wa kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku tatu mfululizo na watu mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi mengine wapatao 20. Alisema kuwa Jumla ya gharama zote za kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii katika kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika vijiji kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni hamsini (50,000,000/=). Makyao alisema katika awamu hii ya vijiji kumi vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa kati ya lengo la watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.

SINGIDA: ENEO LA UZALISHAJI UMEME WA UPEPO NCHINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Dodoma
Maeneo ya Kititimo na Kisaki mkoani Singida yametajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo mazuri nchini yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya upepo.  
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani amesemwa hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu sawali la Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa lililohoji ni lini mradi huo utaanza kuzalisha umeme huo mkoani humo.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Kalemani amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa ikifanya tafti kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo utaanza ifikapo Aprili 2017 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2019 baada ya majadiliano kati ya TANESCO na kampuni ya Wind East Africa Ltd kukamilika mwezi Desemba 2016” amesema Naibu Waziri Kalemani.
Kupitia tafiti hizo, Naibu Waziri Kalemani amesema kuwa kampuni binafsi ya Wind East Africa Ltd yenye Wabia watatu ambao ni Six Telecoms (Tanzania), kampuni ya Kimataifa ya Aldwych ya nchini Uingereza pamoja na moja ya wajumbe wa Benki ya Dunia (IFC) ambao utagharimu jumla ya kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 264.77.
Aidha, Naibu Waziri Kalemani kampuni nyingine inayoonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kufua umeme wa upepo ni mkoani Singida kuwa ni Geowind Ltd ambayo ipo tayari kuzalisha umeme wa Megawati 50 eneo la Kititimo ambapo kampuni hiyo tayari ina eneo la hekta 1,450, mradi huo unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 136 na kukamilika mwaka 2018.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa