MH. TUNDU LISSU AFANANISHA KESI YAKE NA MKASA WA YOHANA MBATIZAJI.

Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama cha CHADEMA Mh. Tundu Lissu (mwenye fimbo) akiingia kwenye viwanja vya kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida kwa kuhutubia wananchi.Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) muda mfupi kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa jimbo la Singida mjini. Wa kwanza kulia ni mke wake.Mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha CHADEMA na ambaye ni mdogo wake Tundu Lissu Christina Mughwai, akisalimia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Tundu.Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA) Mh. Tundu Lissu akihutubia wakazi wa jimbo la Singida mjini.Mbunge wa jimbo...

PICHA NA HABARI: CHADEMA KUPITIA MH. TUNDU LISSU YAIBUKA KIDEDEA KESI YA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI.

Wakili wa waleta maombi Wanaccm Godfrey Wasonga akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Tundu Lissu hayajatangazwa. Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge.Mbunge wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu akifutwa machozi na mke wake wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo,ni halali.Baadhi wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi...

TUNDU LISSU ASHINDA KESI YA KUPINGA UBUNGE WAKE

  Hoja zote za upande wa mlalamikaji zatupwa. Maofisa Jeshi pamoja na kikosi maalum waudhulia maakamani. Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, ameshinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake mjini Singida kupinga ushindi uliomweka madarakani Hukumu imetolewa na Jaji Moses Mzuna anayetoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.  Leo mahakamani wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari walijitokeza kwa wingi sana katika eneo la mahakama. Idadi ya Polisi pia ilikuwa kubwa, ndani na nje ya mahakama.Kilicho...

Hukumu Ya Tundu Lissu leo Ijumaa

 Na Elisante JohnSingida, KESI inayomkabili mbunge wa Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, iliyofunguliwa mjini Singida kupinga ushindi uliomweka madarakani, itatolewa leo ijumaa (Aprili 27, mwaka huu). Hukumu itatolewa na Jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu. Kesi hiyo imekuwa kivutio sana kwa wananchi wengi wa mkoa Singida na nchini kwa ujumla, kutokana na umaarufu wa mbunge huyo machachari. Jaji anayesikilia shauri hilo mjini Singida, anatoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro. Walalamikaji wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama...

BODI ZA ZABUNI SINGIDA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA YA MWAKA 2004.

Mwanasheria Mwandamizi wa PPAA Esthery Nyagawa akitoa mada yake kwenye warsha iliyohudhuriwa na wazabuni, wahasibu na maafisa ugavi (hawapo kwenye picha) iliyohusu  utatuzi wa migogoro katika ununuzi wa umma chini ya sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2004 na sheria mpya ya mwaka 2011. Baadhi ya wazabuni, maafisa ugavi kutoka serikalini na wahasibu waliohudhuria warsha iliyohusu utatuzi wa migogoro katika manunuzi ya umma. (Picha zote na Nathaniel Limu).Na Nathaniel Limu.Mwanasheria Mwandamizi wa mamlaka ya rufaa za zabuni za umma (PPAA) Esthery Nyagawa, amezihimiza bodi za zabuni kuwa makini wakati wa uteuzi wa zabuni ili kujijengea...

WAJASIRIAMALI SINGIDA WANUFAIKA NA MRADI WA KUWEZESHA BIASHARA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Kone (kushoto) akitembelea maonyesho ya wajasiriamali mara baada ya kufungua sherehe za utoaji zawadi kwa washindi wa mashindano ya mpango huo zilizofanyika katika ukumbi wa chuo cha FDC mjini Singida.Na.Mwandishi wetuAkiongea Mkuu wa mkoa amesema kuwa washiriki hao walinufaika na mtaji wa Sh. 2,800,000, BDG ilitumia kigezo cha ustawi wa biashara na uandishi mzuri wa michanganuo katika kuwapatia wajasiriamali hao fedha hizo.Aidha amesema tangu mpango huo uanzishwe mwezi Agosti 2008, umewapatia wajasiriamali nchini, mtaji wenye thamani ya Sh. Bilioni 15 hadi kufikia Agosti mwaka jana.Kone amepongeza wajasiriamali...

WANANCHI WA SINGIDA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPANDA MITI WAKATI WOTE.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania Mchungaji Joseph Mitinje akipanda mti kwenye viwanja vya kanisa la FPCT kisaki nje kidogo ya mji wa Singida.(Picha na Nathaniel Limu).Na Nathaniel Limu.Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania (CIT) Mchungaji Joseph Mayala Mitinje, amewahimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kupanda miti wakati wote badala ya kusubiri April mosi siku ya upandaji miti.Mchungaji Mitinje ametoa wito huo wakati akishiriki kupanda miti kwenye viwanja vya kanisa la FPCT la kata ya Kisaki Manispaa ya Singida ambapo amesema kila mtu hivi sasa ni shahidi...

MATAMASHA YA MICHEZO SINGIDA YATAKIWA KUELEKEZWA HADI NGAZI ZA VIJIJINI.

Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya makocha wa michezo mbalimbali (hawapo kwenye picha) kutoka baadhi ya shule za sekondari za mkoa wa Singida. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Singida Allan Jumbe. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Elimu kupitia michezo (TTU)mkoa wa Singida Anord Bugado na wa kwanza kulia ni Katibu CWT mkoa wa Singida Said Mselemu. Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akimkabidhi cheti mmoja wa walimu wa shule za sekondari waliohudhuria mafunzo ya siku saba ya michezo mbalimbali. (Picha na Nathaniel Limu). Na Nathaniel...

Mtumishi wa Usalama Taifa ajinyonga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Celina Kaluba Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa mkoa wa Singida amejinyonga hadi kufa, akiwa kwenye eneo lake la kazi, kwa kutumia shuka. Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Celina Kaluba, alimtaja mtumishi huyo kuwa ni Azaria Mbaga (47), mkazi wa Sabasaba mjini Singida. Kamanda Kaluba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 9, mwaka huu saa 8:30 usiku katika kibanda kinachotumiwa na walinzi wa ofisi hiyo, iliyopo eneo la Bomani, mjini Singida. Alisema kuwa, muda mfupi baada ya kujinyonga, wenzake walifanikiwa kuuona mwili wake ukiwa umening’inia ndani ya banda hilo, majira ya saa 9:30 usiku, na...

RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA PASAKA KWA WAZEE WA KAMBI YA SUKAMAHELA WILAYANI MANYONI.

 Katibu tawala mkoa wa Singida (kulia) akikabidhi mbuzi watatu wakiwa ni zawadi kutoka kwa Rais Kikwete kwa wazee wasiojiweza wa kambi ya Sukamahela wilayani Manyoni. Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan (kulia) akikabidhi dumu la mafuta ya alizeti moja ya zawadi zilizotolewa na Rais Kikwete kwa wakazi wa kambi ya wazee ya Sukamahela. Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan (kulia) akimvisha shati mmoja wa wakazi wa kambi ya wazee ya Sukamahela. Katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete, kwa wakazi wa kambi ya Sukamahela...

BALOZI SEIF IDD APIGA TAFU SKULI YA SEKONDARI YA MASISTA YA MITUNDURUNI MKOANI SINGIDA.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mchango wa shilingi 1,000,000/- Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Mh. Dianna Chilolo kwa ajili ya uendelezaji wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Masista ya Mitundu Mkoani Singida. Mchango huo aliukabidhi VIP Karimjee Mjini Dar es salaam kutekeleza ahadi aliyoitowa wakati alipotembelea Ujenzi huo Tarehe 7/2/2012 Huko Singida akiwa mlezi wa Mkoa huo Kichama.Othman Khamis Ame – Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekabidhi mchango wa Shilingi Milioni Moja { 1,000,000/-} kwa ajili ya uendelezaji wa Ujenzi...

Kesi Ya Tundu Lissu:Yaibua Makubwa

Josephat isango- Singida.Kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA jana iliibua mambo mapya, baada ya mshitakiwa Tundu Lissu kutoa waraka Mahakamani ulioandikwa na John Chiligati kuomba ufafanuzi namna TLP ilivyoshiriki katika uchaguzi Mkuu wa 2010.Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo Tanzania daima inayo, yenye kumbukumbu namba CCM/OND/559 Vol.II/10, ya tarehe 23/03/2011. John Chiligati aliomba kujua kama kweli TLP iliweka mawakala katika Jimbo la uchaguzi wa singida mashariki, au kama mihuri iliyotumika ya TLP ilikuwa ni sahihi au ni ya kughushi, Kufuatia barua hiyo, barua nyingine ya majibu kwa Chiligati, iliyotolewa...

PINDA AONGOZA UPANDAJI MITI SINGIDA

 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akipanda mti kwenye chanzo cha maji katika kijiji cha  Ilongero, Singida Aprili 1, 2012 ikiwa ni siku ya kitaifa ya upandaji miti.  Aliyesimama kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Vincent Perseko Ole Kone. Wanafunzi wakipanda  miti katika chanzo cha maji cha kijiji cha Ilongero, Singida ambako waziri Mkuu Mizengo Pinda aliongoza shughuli hiyo Aprili 1, 2012 ikiwa ni siku ya kitaifa ya upandaji  mitiWaziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua kisima  kirefu cha maji baada ya kuongoza upandaji miti katika kijiji cha Ilongero , Singida Aprili 1, 2012 ikiwa ni siku ya kitaifa ya upandaji iti Kushoto...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa