Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya makocha wa michezo mbalimbali (hawapo kwenye picha) kutoka baadhi ya shule za sekondari za mkoa wa Singida. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Singida Allan Jumbe. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Elimu kupitia michezo (TTU)mkoa wa Singida Anord Bugado na wa kwanza kulia ni Katibu CWT mkoa wa Singida Said Mselemu.
Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akimkabidhi cheti mmoja wa walimu wa shule za sekondari waliohudhuria mafunzo ya siku saba ya michezo mbalimbali. (Picha na Nathaniel Limu).Na Nathaniel Limu.
Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan ameagiza matamasha ya michezo mbalimbali yaelekezwe hadi ngazi ya vijijini ili pamoja na mambo mengine, wakazi wa maeneo hayo waweze kupata fursa ya kuibua vipaji vyao.
Hassan ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya makocha wa michezo mbalimbali wa shule za sekondari za mkoa wa Singida.
Amesema kumekuwa na mazoea yasiyopendeza ya kufanyia matamasha ya michezo sehemu za mijini tu kitendo ambacho kimekuwa kikiwanyima wakazi wa vijijini fursa mbali mbali ikiwemo kuibua vipaji vyao.
Kwa upande wa serikali ya mkoa wa Singida,katibu tawala huyo,alisema imejipanga vizuri kwa lengo la kuhakikisha michezo inautangaza mkoa kikamilifu.
Hassan amesema kupitia uongozi wa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, mkoa unaendelea kuiandaa shule ya sekondari ya Mandewa manispaa ya Singida ili ianze kupokea wanafunzi wenye vipaji vya michezo kutoka sehemu mbalimbali za mkoa.
Mafunzo hayo ya siku saba yaliyofanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya chama cha walimu mkoa wa Singida, yaliandaliwa na mradi wa elimu kupitia michezo kwa shule za sekondari (TTU) za mkoa wa Singida.
Mradi huo unafadhiliwa asilimia 75 na Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya Finland kupitia shirika lisilo la kiserikali la LiiKe.
0 comments:
Post a Comment