Kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 28 na 33 mfanyabiashara za machinga mjini Singida,Bakari Kavite,mwili wake umeokotwa leo (31/10/2012) saa moja na nusu akiwa amejinyonga kwenye nyumba ya sinema ya Furaha jirani na hotel yenye hadhi ya kitalii ya Stanely motel.Amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya.Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa,ameahidi kutoa taarifa baadaye kuhusiana na tukio hilo.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Askari na Wakazi wa Singida wakibeba mwili wa Marehemu kuupeleka Hospital kwa ajili ya uchunguzi.Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.
Mo B...
MKULIMA WA SINGIDA KIZIMBANI KWA TUHUMA KUMNAJISI MWANAE WA DARASA LA PILI.

Na Nathaniel Limu.Kijana mmoja mkulima wa kijiji cha Ughandi ‘B’ tarafa ya Mtinko jimbo la Singida kaskazini, amepandishwa kizimbani akituhumiwa kumwingilia kimwili mtoto wake wa kike anayesoma darasa la pili.Kijana huyo ni Juma Abrahaman na umri wake ni miaka thelathini (30).Mwendesha mashitaka Geofrey Luhanga amedai mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Singida Flora Ndale, kuwa mnano Septemba 9 mwaka huu majira ya jioni, mshitakiwa Juma kwa makusudi, alimwingilia kimwili mtoto wake wa kike kitendo anachojua wazi kuwa ni kinyume na sheria.Akifafanua amedai kuwa mshitakiwa alimwita mtoto wake (jina tunalo) chumbani kwake na kisha kumfanyia...
SIRUNGONET YAANZA KUENDESHA MIDAHALO
na Jumbe Ismaily, Singida
MTANDAO
wa asasi za kiraia wilaya ya Singida vijijini (SIRUNGONET) umetangaza kuanza
kuendesha midahalo ya mikakati ya kupunguza umaskini na kuongeza kipato kwa
jamii kwenye jimbo la Singida Kaskazini, Singida Magharibi na Singida
Mashariki.
Mratibu
wa Sirungonet wilayani hapa, Sombi Sombi, alisema jana kuwa leo wataanza
mdahalo katika kijiji cha Itaja, tarafa ya Mgori.
Alisema
Oktoba 23, wataendesha mdahalao kijiji cha Puma, kilichoko jimbo la Singida
Magharibi kuanzia saa tatu asubuhi ambapo wananchi watapata fursa ya kutoa
maoni yao wakati saa sita mchana wananchi wa kijiji cha Dung’unyi katika jimbo
la Singida Magharibi watapa nafasi ya kutoa maoni yao pia.
Aidha,
mratibu huyo alisema lengo la midahalo hiyo ni kuimarisha mahusiano kati ya
wananchi na wabunge...
MWENDO KASI WASABABISHA KIFO CHA MCHUNGAJI JACKSON HUSENA KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI SINGIDA.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) ya ajali iliyoua mchungaji wa kanisa la Pentekoste.
(Picha na Nathaniel Limu).Na Nathaniel Limu.Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia kisha kupinduka mkoani Singida.Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Kamishina msaidizi Linus Sinzumwa, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku katika eneo la mzunguko mjini Manyoni barabara kuu ya Dodoma-Mwanza.Amesema wakati wa tukio hilo wachungaji wa kanisa la Pentekosti walikuwa...
MFUKO WA BIMA SINGIDA WAWATAKA MADIWANI KUHAMASISHA WANANCHI KUHUSU FAIDA ZA MFUKO HUO.
Maafisa wa mfuko wa taifa wa biwa ya afya (NHIF) wakiwa ofisini kwao katika majengo ya chuo cha VETA mjini Singida,Kulia ni afisa msimamizi wa ofisi ya mkoa wa Singida na kushoto ni afisa matekelezo Isaya Sheikifu.(Picha na Nathaniel Limu).Nathaniel Limu.Madiwani wa halmashauri ya wilaya na manispaa ya Singida, wamehimizwa kuongeza kasi ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF), ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kupata tiba hasa kipindi hali zao kiuchumi zinapokuwa sio nzuri. Wito huo umetolewa na Afisa Matekelezo wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Singida Isaya Sheikifu wakati akizungumza kwenye...
WANANCHI SINGIDA KUANZA KUTOA MAONI JUU YA KATIBA KUANZIA OKTOBA 17-27, 2012.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya ujio wa tume ya kukusanya maoni ya Katiba kwenye wilaya hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).Na Nathaniel Limu.Tume ya mabadiliko ya katiba, inatarajia kuanza kukusanya maoni ya wananchi wa wilaya ya Singida kuanzia oktoba 17 hadi 27 mwaka huu.Akitoa taarifa ya ujio wa tume hiyo wilayani humo kwa waandishi wa habari hiyo Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi amesema wilaya hiyo yenye halmashauri mbili, tume hiyo itaanza kukusanya maoni kwenye kata kumi za halmashauri ya manispaa ya Singida kuanzia Oktoba 17...
MKAZI WA SINGIDA AJIUA BAADA YA KUMKATAKATA VISU MPENZI WAKE AKIFIKIRI AMEMUUA KUFUATIA KUSHINDWA KULIPA MAHARI.
Mhudumu wa chuo cha VETA mjini Singida Maria Chilinde akiwa wodini katika hospitali ya mkoa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kukatwa katwa visu na mchumba wake.(Picha na Nathaniel Limu).Na. Nathaniel LimuKijana mmoja mkazi wa mkoa wa Dodoma aliyetambulika kwa jina moja la Oscar anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24, amejiuwa kwa kutumia pazia la dirisha.Oscar amejiuwa oktoba 13 mwaka huu usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya kumkatakata vibaya mchumba wake Maria Chilinde (25).Maria ni mhudumu wa chuo cha VETA Mjini Singida, na amepata dhahama hiyo kwenye nyumba anayoishi...
WAZIRI MAGUFULI APONGEZA WAANDISHI KWA KUCHANGIA KUKARABATIWA KWA KIPANDE CHA BARABARA IRAMBA.
Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kipande cha barabara (kilometa 33) zinazorudiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya CHICO ambayo inadaiwa awali kuijenga chini ya kiwango. Kampuni ya CHICO inajenga kipande hicho kwa gharama zake pamoja na mkandarasi mshauri. Gharama ya ujenzi wa kipande hicho kinachoanzia katika kijiji cha Misigiri hadi Shelui ni zaidi ya shilingi bilioni 80.Meneja wa TANROADS mkoa wa Singid Mhandisi Yustaki Kangole akitoa taarifa yake ya ujenzi wa kipande cha barabara kinachoanzia kijiji cha Misigiri hadi Shelui kilometa 33. Kipande hicho kinarudiwa kujengwa na kampuni ya kichina CHICO baada ya awali...
TANROADS SINGIDA YALAMBA SH BILIONI 4
Na Nathaniel Limu, Singida
WAKALA wa Barabara (TANROAD) mkoani Singida,
umetumia zaidi ya Sh bilioni 4.4, kugharamia matengenezo ya barabara kwa
kiwango cha udongo na chagarawe.
Hayo yalisemwa juzi na Meneja wa TANROADS mkoani hapa, Mhandisi Yustaki Kagole,
wakati akitoa taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Paseko Kone.
Kagole alisema, matengenezo hayo yalifanyika katika kipindi cha mwaka
2011/2012, ambapo matengenezo ya kawaida ya kilomita 637, yamegharimu zaidi ya
Sh milioni 897.
"Matengenezo ya vipindi maalumu ya kiliomita 102, yamegharimu zaidi ya Sh
bilioni 1.8 na matengenezo ya sehemu korofi yenye urefu wa kilomita 48.2, nayo
yamegharimu zaidi ya Sh milioni 640.6,” alisema.
Alisema mategenezo madogo kwa ajili ya kulinda na kutunza madaraja tisa,
yamegharimu...
‘POLISI OMBENI VIBALI TANROADS’
na Halima Jamal, Manyoni
KUTEUA
kwa jeshi a polisi vituo vya vizuizi bila kupata kibali cha Wakala wa
Barabarani (TANROADS), kumesababisha uharibifu wa barabara za lami zinazojengwa
kwa gharama kubwa.
Hayo
yamesemwa jana na Meneja wa TANROADS mkoani Singida, Yustaki Kangole, wakati
akitoa taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, ambaye
ameanza ziara ya siku mbili kukagua hali ya barabara.
Alisema
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani, limekuwa na tabia ya kuchagua
maeneo yasiyofaa kwa ajili ya kuegesha magari makubwa kwa ukaguzi wao.
Aidha
Kangole alisema ni vema jeshi hilo likaishirikisha TANROADS katika kuchagua
maeneo ya ukaguzi wa magari ili uharibifu wa barabara hizo zinazojengwa kwa
gharama kubwa usiendelee kutokea tena.
Meneja
huyo aliyataja maeneo...
Magufuli Ateta Na Makandarasi
,+Magufuli+aliwataka+kutekeleza+mradi+huo+kwa+kuzingatia+makubaliano.jpg)
Akizungumza na uongozi wa kampuni ya CHICO (hawapo pichani), Magufuli aliwataka kutekeleza mradi huo kwa kuzingatia makubaliano John Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya CHICO Magufuli akikagua barabara inayokarabatiwa na kampuni ya CHICO kutoka nchini China baada ya kujenga chini ya kiwango mwaka 2008 Meneja TANROADS mkoa Singida Yustak Kangole akitoa taarifa ya marudio ya ujenzi wa barabara Sekenke-Shelui, km 33.3, kwa waziri
Singida. Oktoba09,2012. Makandarasi.....WIZARA ya Ujenzi imewakumbusha Wakandarasi nchini kujenga barabara zinazolingana na thamani ya fedha, iliyopo kwenye mikataba yao....
MH. DIANA CHILOLO AWABWAGA WAPINZANI WAKE NAFASI YA MWENYEKITI WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA UWT (CCM) MKOA WA SINGIDA.
Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT mkoa wa Singida kwa kumchagua tena kuwa mwenyekiti wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Chilolo alipata kura 431 dhidi ya kura 451 zlizopigwa.Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa UWT CCM mkoa wa Singida akitoa maelekezo kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi huo.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata (waliokaa mbele anayesikiliza simu) na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT mkoa wa Singida.Kulia kwake ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Diana Chilolo.Baadhi...
HANJE BANARBAS AUKWAA TENA UENYEKITI WA CCM SINGIDA VIJIJINI KWA MIAKA MITANO IJAYO.
Mgombea nafasi ya uenyekiti wa CCM wilaya ya Singida vijijini Hanje Narumba Barnabas akijinadi kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM (hawapo pichani) huku akiwa amebeba biblia mkononi.Hanje alitetea nafasi yake hiyo baada kupata kura 607.Mwenyekiti mteule wa CCM wilaya ya Singida vijijini Hanje Narumba Barnabas akiwa haamini kama kweli katetea nafasi yake kutokana na upinzani mkali kwenye uchaguzi huo.Baadhi ya wajumbe 1,200 waliohudhuria mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM wilaya ya Singida vjijini.(Picha na Nathaniel Limu).Mkutano mkuu wa uchaguzi CCM wilaya ya Singida vijijini umemchagua tena Hanje Narumba Banarbas, kuwa...
GHARAMA ZA MRADI WA UMEME ZAFIKIA MIL. 101/-
na Jumbe Ismaily, Singida
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, limesema gharama za mradi wa umeme
kutoka Mtinko hadi Ikhanoda zimepanda kutoka sh milioni 23 mwaka 2004 hadi
kufikia sh milioni 101 mwaka huu.
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa Singida, Maclean Mbonile, alisema hayo alipozungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema
mradi huo ulioanza mwaka 2003 ulitarajiwa kukamilika mwaka 2004, lakini
haukuweza kukamilika kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
Alizitaja
sababu zilizokwamisha mradi huo kuwa ni vifaa vyote vya mradi kupelekwa kwenye
miradi mingine, licha ya taarifa zake kuonyesha kuwa vimepelekwa kwenye mradi
huo.
Aidha,
alisisitiza kutokana na mradi huo kukaa muda mrefu bila kukamilika, watendaji
wa shirika hilo wamekuwa...