CHAMA
Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Singida kimemuagiza mkuu wa Wilaya ya
Mkalama kuwaondoa kwa nguvu wavamizi wa hifadhi ya pori la
Kipamba/Munguli wanamoishi na wananchi wa jamii ya Kabila la
Wahadzabe.
Wavamizi
hao kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Shinyanga, Simiyu na Singida,
wanadaiwa kufyeka pori hilo na kuchoma moto kwa shughuli
za kilimo na ufuagaji, hali iliyosababisha adha kubwa kwa jamii
hiyo ambayo huishi kwa kutegemea mizizi, asali, matundapori na nyama
kama chakula chao kikuu.
Agizo
hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana
Msindai baada ya kuitembelea jamii hiyo inayoshi kwenye pori lililopo
umbali wa zaidi ya Km 120 kaskazini mashariki mwa mji wa Singida.
Amesema
ingawa kumekuwepo na tishio la baadhi ya wananchi
kukinyima kura chama chake kwenye chaguzi mbalimbali iwapo
wavamizi hao wataondolewa, lakini CCM haiwezi kukubali uharibifu huo
wa mazingira uendelee na wahadzabe kukosa vyakula vya asili kwa
kuogopa kupoteza kura.
0 comments:
Post a Comment