Home » » Matatani kwa kumbaka kikongwe

Matatani kwa kumbaka kikongwe



POLISI mkoani Singida inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Wibia, Saidi Hamisi (30) kwa tuhuma za kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka themanini, mkazi wa Kijiji cha Matongo, Wilaya ya Ikungi, mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa jeshi hilo mkoani Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku na kumtaja aliyembaka bibi kizee huyo kuwa ni Saidi Hamisi.
Aidha, Kamanda Kamwela alifafanua pia kwamba tukio hilo la ubakwaji wa bibi kizee huyo lilitokana na ulevi wa kupindukia kwa mtuhumiwa.
Kamishna msaidizi huyo alisema “mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kutokana na kuwa wakiishi nyumba moja na bibi huyo hivyo alipokunywa pombe na kulewa ndipo alipoona aende akamalize matatizo yake kwa jirani yake huyo,” alisema.
Kwa mujibu wa maelezo ya jamaa wa karibu wa mtuhumiwa huyo, inasemekana kwamba baada ya mtuhumiwa kumaliza kitendo hicho aliamua kuendelea kulala na bibi kizee huyo mpaka asubuhi ili aweze kuendelea tena na kitendo hicho asubuhi kabla ya kuondoka kwenda kuendelea na shughuli zake nyingine.
Aidha, Kamanda Kamwela alisisitiza kuwa majira ya saa 7:15 usiku wananchi walitoa taarifa kwenye kituo cha polisi ndipo jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumhoji.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, bibi kizee huyo amepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi ili kujiridhisha iwapo amefanyiwa kitendo hicho cha kinyama na mjukuu wake na kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa.

Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa