Baadhi
ya wananchi wakiwa wamehamishia makazi yao chini ya mti uliopo kwenye
korongo kijiji cha Handa mpakani mwa Wilaya ya Chemba na Singida
Vijijini mara baada ya nyumba zao kuchomwa moto na askari polisi na wale
wa kikosi cha kupambana na ujangili kwa madai ya kuvamia hifadhi ya
msitu wa mgori (PICHA NA HILLARY SHOO).
Huyu
ni mmoja wa watoto walionashwa na kamera yetu akiwa amelala hoi kwa
kukosa chakula na huduma zingine, baada ya nyumba zao kuchomwa moto
wakati wa operesheni ya kuwahamisha katika kitongoji cha Kazamoyo kwa
madai ya kuvamia hifadhi, hata hivyo wananchi hao wameisha katika eneo
hilo kwa zaidi ya miaka nane toka mwaka 2005 , lakini sheria ya kuingiza
eneo hilo kwenye msitu wa hifadhi ya mgori ilifanyika mwaka 2007,
(PICHA NA HILLARY SHOO).
.Unyanyasaji dhidi ya wananchi wakithiri wilayani Singida
Na Hillary Shoo, Singida
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wametakiwa kufika katika
kitongoji cha Kazamoyo kijiji cha Nguamuhanga tarafa ya Mgori Wilayani
Singida vijijini na kujionea unyanyasaji dhidi ya wananchi wakati wa
zoezi la kuwaondoa katika hifadhi ya msitu wa mgori.
Hayo
yamesemwa juzi katika kitongoji hicho na baadhi ya wananchi walioamua
kuhamia kwenye korongo na kuishi chini ya miti kama digidigi kunusuru
maisha yao kutokana na vipigo kutoka kwa wa kikosi cha kupambana na
ujangili Wilaya ya Singida na askari polisi.
Wamesema
ni vyema kituo hicho wakafika mapema ili kuona jinsi ambavyo binadamu
wanavyoishi maisha ya shida ta taabu kwenye eneo hilo kufuatia amri ya
mkuu wa Wilaya ya kuhamisha kwa muda mfupi.
Wamesema
eneo hilo wameishi zaidi ya miaka nane na kujenga makazi bora bila
matatizo yoyote, lakini jambo la ajabu ni baada ya Wilaya ya Chemba na
Sngida kuwekeana mipaka na kuonekana kuwa wako Singida.
“Wakati
tuko kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba, tuliishi bila matatizo lakini
baada ya kuhamia singida ndipo mambo yalianza kubadilika na kuambiwa
kuwa tuko eneo la hifadhi, hii ni ajabu sana , Wilaya moja tuliishi
vizuri hii nyingine haitutaki sasa tuende wapi.” Alihoji mmoja wa kina
mama.
Licha
ya kukosa huduma muhimu kama vile maji, mahema, vyoo baadhi ya kina
mama na watoto walionekana wakiwa katika huzuni klubwa huku wengine
wakiangua vilio baada ya kuwaona waandishi wa habari wakidhani kuwa ni
askari.
Hata
hivyo eneo hilo lina mbu wengi, jua kali na mbaya zaidi hivi sasa ni
msimu wa mvua katika maeneo hayo, je swali la kujiuliza wataishije hapo
wananchi hao zaidi ya 1,000 ambao nyumba zao zimechomwa moto.
Hata
hivyo Mkuu wa Wilaya ya Singida Qeen Mlozi amesema zoezi hilo
linaendelea sanjari na kuhakikisha wanaondoka kwenye korongo hilo
walimojificha.
Hivi
karibuni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
alitembelea eneo hilo la kusitisha zoezi la kuwahamisha mpaka pale
kamati ya kudumu ya huduma za kijamii ya baraza la madiwani
watakapokutana kutoa maamuzi sahihi juu ya wananchi hao.
Hata
hivyo agizo hilo la Naibu Waziri limepingwa vikali sana na mkuu wa
Wilaya ya Singida Mwalimu Qeen Mlozi kwamba Nyalandu hana mamlaka
kisheria ya kusitisha zoezi hilo, na kwamba anayeweza kumwamuru
kusitisha zoezi ni Mkuu wa Mkoa pekee na si vinginevyo.
Na Mo Blog
0 comments:
Post a Comment