Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akizungumza kwenye hafla ya ufungaji
wa mafunzo ya ufugaji bora nyuki iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa SIDO mjini Singida.Kulia ni meneja wa SIDO mkoa wa Singida, Shoma
Kibende.
Meneja
wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibende akitoa taarifa yake kwenye hafla
ya ufungaji mafunzo ya ufugaji nyuki iliyofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa SIDO mjini Singida.Wa pili kulia (aliyeketi) ni mkuu wa
wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akimkabidhi mfugaji wa nyuki cheti cha
kumaliza mafunzo ya ufugaji bora nyuki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
mjini Singida.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(aliyeketi katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wafugaji Nyuki waliohitimu mafunzo ya ufugaji bora wa
Nyuki.Wa kwanza kushoto (walioketi) ni meneja wa SIDO mkoa wa
Singida,Shoma Kibende na kulia ni mwenyekiti wa wafugaji Nyuki (jina
halikuweza kupatikana).(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Serikali
wilayani Singida, imewahimiza wajasiriamali na wafanyabiashara kujenga
utamaduni wa kutangaza bidhaa zao kwenye vyombo vya habari ili pamoja na
mambo mengine, waweze kujipatia soko la uhakika.
Wito
huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya hiyo Queen
Mlozi,wakati akizungumza kwenye hafla ya ufungaji mafunzo ya ufugaji
bora wa nyuki na uchakataji wa asali.
Akifafanua
amesema ushindani mkubwa wa biashara uliopo hivi sasa,mfanyabiashara
atakayefanikiwa ni yule tu ambaye atatangaza biashara yake kikamilifu.
Mlozi amesema biashara bila matangazo,ni sawa na mtu asiye na biashara kwa sababu bidhaa zake,hazitajulikana.
Amesema
pamoja na kujitangaza huko,kwanza wahakikishe bidhaa zao zina kuwa na
ubora unaohitajika na pia wahakikishe wanashiriki maonyesho
yanayoandaliwa na SIDO kanda ya kati.
Awali
meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibende, amesema kuwa SIDO inao
mpango wa kuwaelimisha wafugaji na kuhakikisha uzalishaji wa zao la
asali unazingatia ubora tangu mahali zao linapoanzia.
Kibende amesema ubora huo unaanzia eneo la ufugaji,uvunaji na ufungashaji,upatikanaji wa masoko ya ndani na ya nje ya nchi.
“SIDO
imeona umuhimu wa kutoa mafunzo haya kwa kuzingatia kwamba walengwa
tayari wameanza shughuli za ufugaji nyuki,ununuzi na uuzaji wa zao la
asali”,alifafanua zaidi meneja Kibende.
Picha na Mo Blog
Picha na Mo Blog
0 comments:
Post a Comment